Jenerali wa US aitabiria vibaya Ukraine

Jenerali wa US aitabiria vibaya Ukraine

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
10,509
Reaction score
16,734
Generali mstaafu wa jeshi la Marekani Mark Kimmitt, amesemea kazi ya Ukraine ya kukomboa maeneo yanayokaliwa na Urusi ni kubwa sana. Amesema maeneo hayo yametenganishwa kwa kilomita karibu 20 kufikia ngome halisi za Urusi lakini ameziita kilomita hizo kuwa moto mkali usiopenyeka.

Amefafanua kwa kusema Urusi ilitumia vizuri muda na matangazo ya Ukraine kwamba inajitayarisha kurudisha mapigo na kukomboa miji iliyotekwa.Muda huo Urusi uliutumia kujenga ngome ambazo si rahisi kwa jeshi la Ukraine pamoja na silaha inazopokea kuzipenya.

Ngome za urusi ni pamoja na mitego ya kuvishika vifaru vya ukraine,nyaya za seng'enge,mabomu ya kutegwa ardhini na nyuma kabisa ni mahandaki yaliyojengwa kwa mfumo ya zig zag ambako ndiko waliko askari wa Urusi wakiwa na uwezo wa kulenga shabaha kutoka mbali.

Inaaminika kushindwa kupenya ngome hizo za Urusi kutavuta muda wa vita ambayo ni fursa muhimu ya Urusi kuwakamua kiuchumi nchi za NATO na yeye kupata kuhema.

Kauli hiyo ya generali Mark Kimmitt imekuja wakati raisi Biden ametoboa siri katika mahojiano yake na waandishi wa habari kuwa sababu ya Marekani kutaka kupeleka mabomu yaliyoharamishwa kutumika vitani kwa Ukraine ni kutokana na nchi yake kuishiwa na marisasi ya mizinga ya 155mm.

Akasema wataipa Ukraine mabomu hayo haramu mpaka hapo watakapokuwa wamezalisha silaha zaidi za kuipatia Ukraine.

1689054263497.png
 
Mwambie Jenerali Mstaafu kwamba Russia ilishauteka mji wa Kyiv lakini akaweza kutupwa huko alikotupwa,
Urusi ilishalitawala eneo la Ukrean lenye ukubwa wa nchi za Newzerland lakini wakaweza kufurushwa kote sasa ni finishing tu., inawezekana sana na huko kuliko baki., tokea counteroffensive Ukrain wana gain maeneo yaliyoporwa hakuna loose yoyote ni mbele mbele mbele tuu., Urusi ni laini sana vita ya ardhini Urusi imeshindwa toka siku ya kwanza.
 
Sawa, Uzuri sisi tuko ushirombo Shinyanga wao Wapo dar kwahiyo wanaziona barabara za chini na za juu alizojenga Magufuli. Sisi ni akina nani tubishe et hakujenga wakati tuko !MBali yaani mpaka tuoneshwe picha , picha zenyewe zinahitaji maelezo .
Irrelevant and off topic maybe the author is suffering from schizophrenia.
 
Mwambie Jenerali Mstaafu kwamba Russia ilishauteka mji wa Kyiv lakini akaweza kutupwa huko alikotupwa,
Urusi ilishalitawala eneo la Ukrean lenye ukubwa wa nchi za Newzerland lakini wakaweza kufurushwa kote sasa ni finishing tu., inawezekana sana na huko kuliko baki., tokea counteroffensive Ukrain wana gain maeneo yaliyoporwa hakuna loose yoyote ni mbele mbele mbele tuu., Urusi ni laini sana vita ya ardhini Urusi imeshindwa toka siku ya kwanza.
uko wapi bwanshehe.Utabiri wa generali unakwenda sawasawa na wafuatiliaji wengine wa mwenendo wa vita na maneno ya majenerali wa Ukraine wenyewe kuwa hakuna maendeleo ya maana.
Hii inaweza ikawa ndio mwisho wa kusaidiwa kijeshi Ukraine hasa ukitilia maanani kuwa zaidi ya robo ya vifaru vilivyotolewa msaada vimeripuliwa au vimeharibiwa na haviko tena mstari wa mbele.
 
Irrelevant and off topic maybe the author is suffering from schizophrenia.
Putin: “Russia has not yet needed to use cluster munitions, but if they are used against the country, it has the right to mirror action”.

Kharkiv on February 28: one of the many cases of Russian use of Smerch cluster munitions in densely populated residential areas.
 
Mwambie Jenerali Mstaafu kwamba Russia ilishauteka mji wa Kyiv lakini akaweza kutupwa huko alikotupwa,
Urusi ilishalitawala eneo la Ukrean lenye ukubwa wa nchi za Newzerland lakini wakaweza kufurushwa kote sasa ni finishing tu., inawezekana sana na huko kuliko baki., tokea counteroffensive Ukrain wana gain maeneo yaliyoporwa hakuna loose yoyote ni mbele mbele mbele tuu., Urusi ni laini sana vita ya ardhini Urusi imeshindwa toka siku ya kwanza.
Yaani unavyoongea kwa madaha nakuhakikishia ungekuwa karibu na zelensky ungekula kerbu ya mkoundou usingeamini wenzio wanaugulia maumivu wewe unaleta ushabiki wa simba na mbao fc
 
Cluster bombs , F-16 na ATACMS zinaenda kumaliza vita mapema huko Ukraine.

Kama Urusi ana akili basi bora aondoke tu sasa hivi maana logistics and supplies zake zitachakazwa kutokea mbali na askari wake wkose mahitaji muhimu ya kivita na kibinadamu.
 
Back
Top Bottom