Lancashire
JF-Expert Member
- Sep 20, 2014
- 14,081
- 10,455
Bado kuna uhutu na ututsi
Unafikiri kwanini bado kuna uhutu na utusi? sababu ni nini? Sorry kwa maswali nahitaji kufaham tu
Bado kuna uhutu na ututsi
Wazee hebu nipeni ufafanuzi kidogo.jana katika pitapita kwenye azam tv nikakutana na channel ya taifa ya Rwanda naona wamejoin.swali sasa je ile lugha tofauti na English ilyokuwa inazungumzwa pale ni kitusi au kihutu maana nimesikia huko Rwanda kuna makabila mawili tu.naombeni msaada hapa kwenye huu uzi nielimike maana najuwa jamaa wa pande hizo mko hapa.
Unafikiri kwanini bado kuna uhutu na utusi? sababu ni nini? Sorry kwa maswali nahitaji kufaham tu
hahahaha...kweli ignorance is rampant. Mmarekani anajua mpaka raisi wako analalia shuka gani ikulu FYI. Ukitaka kujua, soma Wikileaks ndo utajua. Taarifa zote wanazo mkononi, hawakurupuki aisee...wako makini sana.
Mkuu wakati mwingine mnaweka chumvi mno kuhusu uwezo wa Merikani katika masuala ya Ujasusi - tusidanganye watu hapa - huu umahili wa Ujasusi wa Merikani mnao hubiri members humu kila siku unatoka wapi - wangekuwa wakali Magaidi wa Kisaudia na Misri wasingeingia Merikani kirahisi wakaji enroll kwenye shule za kufundisha Urubani wamekaa huko kwa miezi kadhaa bila ya kushtukiwa, walifikia hatua ya kwenda kuangalia ndege ndogo za kunyunyizia dawa wakati wenyewe hawana mashamba Merikani hata kitendo hicho hawakushtukiwa kabisa!! Kila mwezi wanatumiwa fedha lukuki kutoka Saudia majasusi wa Merikani wala hawashtuki, haya ndege za abiria zimetekwa moja baada ya nyingine zinakaa angani kwa masaa huku transponder zake zimezimwa waongoza ndege aridhini hawashtuki, zinafikia hatua ya zinabaizwa kwenye majengo Airforce hipo kimya kabisa licha ya abaria kutoa taarifa mapema kwa ndugu zao kupitia mobilephone kuwa ndege hizo zimetekwa na magaidi hakuna lililo fanyika!!!
Mkuu Murutongore leo hii unawezaje kusema Merikani ana uwezo wa kujua Rais wetu analalia shuka gani sijui! Merikani hawako smart kivile; chukulia mfano wa pili: Kama wengekuwa mahili Osama hasingeishi Pakistani kwa miaka bila ya kugundurika, Merikani wanaweza masuala ya kunasa mawimbi ya mawasiliano yawe ya sauti au data nk, lakini linapokuja suala la kutumia binadamu ambalo ni crucial katika nyanja za ujasusi, hilo hawaoni ndani kabisa! - na watu wajanja wanakula hela zao kiulaini kabisa kwa kuwapatia false information au information zilizo pitwa na wakati, narudia kusema kwamba kufanikiwa kwao ni kwa nadra sana hata masuala ya wikileaks yamajaa kunaswa kwa mawasiliano ya cable, satellite, telestrial ni mara chache kutumia binadamu/moles kwa kutoa taarifa kwa Balozi zao kwa kuwatumia ma handler wao nk.
Chukulia Bin Laden kwa mfano, Wamerikani wenyewe ndio walimfudisha mbinu za Ugaidi wakati wa Vita kati ya Warusi na Wafughanistan, alifundishwa ufundi wote wa kutegeneza milipuko hatari, kunasa mawasiliano nk ndio maana Osama alikuwa hatumii simu ya aina yoyote iwe za kawaida au za satellite maanake alishajua mbinu zinazo tumiwa na Wamerikani katika masuala ya Ujasusi, bila ya Ofisa wa Jeshi wa Pakistani kusaliti Serikali ya Pakistani kwa kufahamisha Merikani sehemu alipo jificha Osama Merikani hisingegundua Osama alipo jichimbia - sasa kama kweli wana uwezo wa kijasusi mbona Osama alikuwa anatamba miaka nenda rudi?
..Spain wanataka hata Wamarekani nao wachunguzwe kwa makosa waliyoyafanya ktk vita vya Iraq.
..nadhani hicho ndicho kilichopelekea huyu mama kuwa na msimamo huo dhidi ya Spain.
..suluhisho ni kumfikisha Karenzi ktk mahakama inayomtuhumu, na kumpatia kila msaada wa kisheria kusafisha jina lake
cc murutongore, jMali, Bukyanagandi