Jee muda ni mali kwetu watanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jee muda ni mali kwetu watanzania?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by pmwasyoke, Aug 8, 2010.

 1. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Mwenzenu ninakwazwa sana na muda wa kuanza makusanyiko/shughuli mbalimbali hapa kwetu:

  Harusi/send off nyingi nilizohudhuria kadi za mialiko zinaonyesha kuanza tafrija saa 12.30 au saa 1 jioni, lakini maharusi/wahusika wataingia ukumbini saa 2.30 au saa 3 usiku. Vikao vya harusi au maendeleo ya kijamii ndio usiseme - ukifuata muda uliotajwa utajiadhibu.

  Mara mbili nimehudhuria kwenye kumbi ambako wanamuziki mashuhuri walitumbuiza - waliandika onesho linaanza saa 3 usiku, kihalisia wasanii hao walionekana saa 7 na saa 8 za usiku.

  Mifano ni mingi - jamani, kwa nini tusipange muda na kuuheshimu? Kuna athari mbaya tele kiuchumi za kutoutawala muda vizuri.
   
 2. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Halafu utakuta ratiba ya kuanza mathalaan reception ya harusi imechelewa, lakini MC ndio kwanza anajisahau ile mbaya: manamaliza saa nane za usiku! na ndani kuna watoto wadogo wa miaka 4 - 5 wanasimamia harusi!
   
Loading...