Wanabodi.
Hii ni thread ya swali "
Jee Aachwe Tuu Aendelee Kuropoka kwa sababu ndio "Taking The Bitter With The Sweet", au Tu Inject Busara Ndani ya Kichwa Chake ili achague maneno ya kuongea nini na wapi?!.
Declaration of interest. "Mimi Paskali ni mropokaji, ila kwa nafasi yangu ni ruksa kuwa mropokaji ila kuna positions huwezi kuwa mropokaji.
NB. Uropokakaji sio kutukana ni neno linalomaanisha kuongea maneno ya hovyo hovyo bila kujali the consequences of matamshi yako.
Angalizo.
Naomba kuanza na angalizo.
Simple Mind Discuss People.
Ordinary Mind Discuss Events
Great Mind Discuss Ideas.
Hii ni thread kuhusu ideas, naomba sana tusitaje jina la mtu yoyote kwa sababu hatujadili mtu bali tunahadili matumizi ya kutumia busara kuchagua kwa makini maneno ya kutumia katika kuongea, unaongea nini, wapi, na nani hivyo uchague maneno gani ya kuongea wapi ili kufikisha ujumbe husika.
Mropokaji ni Nani? .
Mtu anayeongea lolote popote, bila kujali anaongea nini na nani na huvyo atumie maneno gani, huyu ni mropokaji.
Jee ikitokea watu tukabahatika kumpata mtu safi mwenye uwezo wa kunyoosha kila palipopinda, na mwenye nía njema na dhamira safi lakini ni mropokaji, tumuache tuu aendelee kuropoka au tumsaidie ili apunguze uropokaji? .
Jee tumuache tuu aendelee kuropoka simply because he is the best on what he does, au tumsaidie afundishwe namna ya kuchagua maneno gani azungumze wapi na nani ili kufikisha ujumbe sahihi na ndio maana taifa linagharimia watu mahirI kwa jina la speech writers ili wamuandikie nini cha kusema wapi, sasa hawa watu wanafanya nini?.
Au kwa vile dawa chungu ndio iponyeshayo ugonjwa, Tanzania kama taifa lazima tukiri tunaugonjwa, amepatikana daktari bingwa wa kutibu ugonjwa wetu ila dawa zake chungu kwa kudunga sindano zenye maumivu makali, kutoa vidonge vichungu kumesa na hata kutumbua majipu bila ganzi, tatizo pía ni mropokaji!, hivyo tuuchukulie huo uropokaji ndio tamu ya chungu ya dose yake, tuvumilie tuu, tumeze tupone? .
Sasa ili tupone, do we have to take the bitter with the sweet!, or to choose to take only the sweet na kumeza lakini the bitter tuteme? . Ule msemo wa wape wape vidonge vyao, una apply hapa, jee hivi ndio vidonge vyenyewe tunavyotakiwa kumeza au kutema ni shauri yetu au Tanzania ni yetu sote hivyo tunajukumu kusaidia? .
JF Has A Duty!.
JF we have a duty of care to help out this situation kwa kusema the right thing to do and how to go about it.
Atafutiwe Waalimu! .
Jee watafutiwe waalimu wa somo la busara kujaribu kuingiza busara japo kidogo ndani ya kichwa cha mtu huyu ili atumie kwenye matamshi yake, au tuendelee tuu kumuacha akiropoka huku anashangiliwa na umati wa watu ilihali anaidhalilisha taasisi ile takatifu?.
Nani wa Kumfundisha na kumsaidia?.
Mwanzo wa mwaka nilishauri humu, jf tukiona tatizo mahali tusiishie tuu kutaja tatizo ili tuu watu wajue kuna tatizo, bali tupendekeze na njia za utatuzi.
Kwa tatizo hili la uropokakaji tumpatie waalimu watatu.
1. Yule Mama Anayemmudu.
Huyu mama ni mwalimu na saikolojia ya Kufundishia anaijua, bahati nzuri imetokea she is so humble and down to earth. Katakana na majukumu mapya, ameacha ualimu. Tumuombe andelee na ualimu wake kwa kufungua darasa kwenye kile chumba na kila wakati muafaka baada ya majukumu muafaka ampige somo la yule mwanafunzi mkubwa anayemmudu. Japo huku mtaani anatajwa kuwa ni mbishi, lakini hakuna kiumbe chochote kinachoweza kuleta ubishi kwenye yale, hivyo somo la busara litamuingia.
2. Yule Mama Msaidizi.
Hapa ni kujifunza kwa mifano, mbona mama Msaidizi wake anazungumza kwa heshima, kwa busara na kwa unyenyekevu wa hali ya juu. Wewe Mama Msaidizi, haijalishi unamuogopa vipi bosi wako, kuliko kumuacha aidhalilishe hiyo taasisi aliyopo, kama hauwezi Kumsaidia bosi wako achague maneno ya kuzungumza wapi na nani, unakuwa huna msaada wowote kwake zaidi ya kutumwa kumwakilisha, ukiona kuna maeneo anakosea, mbishie hodi uzungumze nae nyinyi wawili tuu peke yenu, maana kuna watu wakiwekwa kwenye kona, pamba za masikio zinafumka na busara inawaingia.
3. Kwenye Vile Vikao Vyenu.
Kwa vile kila kinachozungumzwa kwenye vile vikao Vyenu ni siri, then ninaamini kuna mijitu mibold mule inaweza kumkabili na kumsaidia, msikubali mfalme aadhirike kwa kauli za uropokakaji, mna jukumu la kumstahi ili kumsaidia, hiyo taasisi ni tukufu, na hapo mahali patakatifu hivyo yampasa mmiliki kuwa mtakatifu na atoe matamshi ya kitakatifu yenye utukufu ndani yake. Mtakatifu hauwezi kuwa mropokaji.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali.