Je Wewe Unatoa machozi gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Wewe Unatoa machozi gani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Obi, Oct 12, 2010.

 1. Obi

  Obi JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2010
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 376
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kuna Story nimeipata kwa rafiki yangu naomba tuijadili kwa maslahi ya Taifa letu lenye rasilimali nyingi lakini ni masikini wa kutupwa.

  Nikiwa kati ya WATU waliohudhuria mikutano ya kampeni hasa ya
  urais,nimeona mengi,nimesikia mengi,ahadi kemkem,tam,nzuri na zenye
  kuvutia na kama JK,SLAA au LIPUMBA mmoja wo akishinda na kutekeleza
  ahadi zake basi TANZANIA itakuwa kama Boswana au kama sio kuifikia
  Afica kusini. Sina sababu ya kuzitaja ahadi kwani wengi wenu mwazijua.

  Ni saa 12:30 za jioni siku ya ijumaa,natoka ofisini kwangu JMOO
  nakwenda posta ili kupanda gari la kuelekea mbezi nyumbani
  kwangu(mbezi ya kimara).Abiria ni wengi kama kawaida,wezi wamo,ila
  kuna magari ya kwenda mbezi ya buku(elfu moja) naingia na muda si
  mrefu gari inajaa na kuondoka,wote tumekaa,foleni ni kama kawaida
  kwani inaanzia faya na huku gari likiwa limefunguliwa radio moja ya chama
  tawala.Watu tupo kimya na aliyesimama ni konda tu.

  Mara hiyo radio ikaanza kutangaza sera za mgombea urais wa chama
  tawala,ahadi nyingi,kile mara hiki najua mwazijua sina shida ya
  kuzitaja ila ni moja tu ambayo nitaitaja ambayo imenipelekea kuandika
  UJUMBE huu kwenu,ni ile ya KUNUNUA BAJAJI 40 KWA WAMAMA
  WAJAWAZITO,hapo ni saa 1:30 za jioni na hatujavuka magomeni.

  Mara baada ya huyo mgombea kutaja hiyo ahadi,nikasikia sauti kutoka
  nyuma ya gari ikisema “ZIMA RADIO YAKO AU BADILISHA STESHENI”ni sauti
  ya kike tena mwanamama mjamzito.Dereva alizima radio,tukawa kimya kila
  mtu nahisi alikuwa anajiuliza kwanini huyu mama kasema radio izimwe au
  ibadilishwe stesheni,ukimya ulitawala ndani ya gari.Tukiwa tunaanza foleni
  ya ubungo pale mahakama ya ndizi au bigbrother, na ikiwa ni saa 2:07
  za usiku,nikasikia sauti ya mwanamama mwingine(sio mjamzito) ikisema
  “KAMA MIMBA ZINGEKUWA ZINABEBWA KWA ZAMU HUYU KIKWETE ASINGETAMKA
  MANENO HAYO” nikashtuka nikageuka nyuma nikakutana uso kwa uso na yule
  mama mwenye mimba,mimba yake ilikuwa ni kama ya miezi nane tena
  ilikuwa kubwa(namaanisha tumbo ni kubwa sana).

  Tukiwa tupo stand ya mkoa na gari likiwa limesimama na ni saa 2:45
  usiku kumbuka nimetoka posta saa 12:30 za jioni.Yule mama mjamzito
  akasimama akaanza kusema “MIMI SITOMPA KURA KIKWETE KWA JAMBO
  HILI,NILIKUWA NIMPE ILA KWA JAMBO KAMA ILI SIWEZI KUMPA” huku akilia na
  kutokwa na machozi,yule mama mwingine aliyesema “kama mimba zingekuwa
  zinabebwa kwa zamu huyu kikwete asingetamka maneno hayo” akaanza
  kumbembeleza yule mama mjamzito akimsihi akae.Nilimtazama kila mtu
  ndani ya gari sura zilibadilika zikawa sura za majonzi.

  Nikatoka kwenye daladala(kimawazo) nikaleta taswira ya BAJAJI
  nikamuweka yule mama nyuma na mimi nikawa dereva,nikafikiria umbali wa
  kilometa 50 toka kijijini kwetu kule kanyigo kuja hospital,barabara
  imejaa mashimo,nikawaza tumbo la yule mama akiwa yuma na uchungu na
  babaji ikiwa inayumba kwenye mabonde ya barabara,”NILILIA”
  nilishutushwa na honi nyingi za magari ambazo zilikuwa zikilipigia
  daladala letu kwa kutotembea, kwani kila mtu alikuwa kwenye mawazo ya
  yule mama(nahisi hivyo) na dereva alijisahau kwa kumuonea huruma yule
  mama.Nilikuwa karibu na dereva nikamuuliza vp?,akajibu “WE ACHA TU”uku
  akitoa leso na kufuta machozi na kuanza kuendesha gari.

  Ni saa 3:07 usiku tupo kimara tunaanza foleni ya kimara stopover,watu
  wote wapo kimya hakuna aliyeshuka mpaka sasa na konda kakaa kwenye
  mlango ameinama,kila mtu kainama,huku wengine wakifuta mafua,na yule
  mama mjamzito akionekana ana hasira na machozi yakimtoka
  yenyewe.Nikajiuliza ina maana watu wote tunakwenda mbezi?,pia huyu
  mama vp mbona kambadilisha kila mtu ndani ya daladala? Katumwa
  nini?.Nikasikia sauti ya baba mmoja kutoka katikakti ya gari akisema
  shusha konda hapo,konda akasema wapi?,baba akajibu hapo
  hapo,Mmmmmmmmm?,”Samahani konda nilikuwa nashuka bucha nimejisahau”
  alisikika yule baba akisema,Mmmmmmmmm?.Ndipo nilipoona kila mtu karudi
  katika hali yake ya kawaida na wengine wakashuka hapo kama watu sita
  hivi.Nikajiuliza je walikuwa wanawaza nini? Mpaka wapitishwe
  kituoni?.Je walikuwa katika taswira kama yangu?,au uchovu wa kazi?

  Kati ya wale walioshuka pale njiani(sio kituoni) baba mmoja akasema
  akimwambia yule mama mjamzito “POLE SANA MAMA NA MIMI NAKUAHIDI
  SITOMPA KURA KIKWETE”akateremaka.Tunavuka stopover na ni saa 3:30
  usiku,kila mtu kaanza kusema lake”KIKWETE HANA AKILI”alisikika baba
  mmoja,”KIKWETE NI MGONJWA” alisikika dada mmoja,”WANAIGEIZA NCHI YA
  FAMILIA KWANI HAPA TUNATAWALIWA KIFALME” alisikika kaka mmoja.Ni saa
  3:45 nashuka kibanda cha mkaa na niliposimama nikawwambia abiria “HUYO
  NDIO RAIS WENU HATA AKIWA CHIZI SI MLIMCHAGU WENYEWE” nikajibiwa na
  konda “SHUKA UKO NA NENDA ZAKO”,Mmmmmmmm hata konda?

  Nikiwa njiani nakwenda kwangu nikawa natafakari “JE YALE MACHOZI YA
  MAJI YALIYONDONDOKA NDANI YA DALADALA LEO”je ni ya bure tu?,na je “IPO
  SIKU YATALIPWA”?,na je “IPO SIKU YATAGEUKA KUWA NI MACHOZI YA DAMU”?
  nisingependa tafakari yangu ya mwisho itokee.

  Je wewe unatoa machozi gani au maneno gani?,je machozi ya furaha? Au
  ya uzuni kama yule mama mjamzito?au maneno ya kumtukana rais wako kama
  wale watu kwenye daladala.Kazi kwako. Nikipata nauli kabla ya UCHAGUZI
  nitakwenda kanyigo nimuulize babu “JE BABU UMESHAWAI KUONA KICHUGUU
  CHA SENENE”?.
  Tusimpe Mbu kazi ya kutibu Malaria???????????????????
   
Loading...