Je, Wewe ni mume au una mume wa aina gani kati ya hawa, reality

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
AINA NANE ZA WANAUME HATARI...

1-Asiependa kufanya kazi akisubiri alishwe na mke.
Huyu ni hatari kwa sababu hatokuwa na ujasiri wa kumkemea mke pale anapokosea kwa kukhofia mke asije kasirika na kusitisha huduma ya kuilisha familia.

2.(ONJAONJA)
Huyu ni mwanamume anaependa kuoa na kuacha bila ya sababu,huyu ni hatari kwa sababu anazichezea sheria za Allah na kuwadhalilisha wanawake,talaka inakubalika ktk Uislamu lkn imewekwa ktk nafasi ya mwisho ikiwa hatua zote muhimu zimeshindikana.Kuoa na kuacha bila ya sababu za msingi hakukubaliki ktk Uislamu.

3-LENINISMY.
Huyu ni mwanamume anaemnunulia mkewe vitu vya aina mbalimbali kisha anaanza kujitangaza nje.
Huyu ni mtu hatari kwa sababu kitendo cha kumpa mtu kitu kisha ukaanza kujitangaza kinaharibu malipo na kinathibitisha kwamba lengo lake lilikuwa si kupata radhi za Allah bali ni kutafuta sifa kwa watu.

4-(ASIE NA WIVU)
Huyu ni mwanamume alieridhia mkewe achezewe na wanamume wengine au Mkewe aoneshe mapambo yake kwa wanamume wengine.
Na hili tunalishuhudia ktk jamii utakuta mwanamume anamruhusu mke atoke ndani ya nyumba akiwa amevaa mavazi yasiyostiri mwili hatimae anawapa mtihani wale wanamume barabarani.Asiekuwa na wivu haingii peponi.

5 .(MWENYE MANENO MACHAFU)
Huyu ni Mwanamume ambae anapokorofishana na mkewe hukimbilia kutoa maneno machafu kama vile kumwita mke "Mbwa"Nguruwe"nk.

6-ALJAAHIL(MJINGA)
Huyu ni Mwanamume asietaka kujifunza mambo ya dini yake,na kwa ajili hii utakuta hamudu kuilea familia ktk maadili anayoyaridhia Allah mtukufu.

7-WOLF'S
Huyu ni mwanamume mwenye kutumia pesa yake na vitu vingine kwa fujo khaswa pale anapopokea mshahara wake.
Israafu ktk matumizi ni haramu.

8-MSHIRIKINA
Huyu ni mwanamume ambae alieiweka mbele shirki ktk mambo yake hata mtoto wake akiumwa MALARIA atampeleka kwa mganga wa kienyeji.

Huyu hafai kabisa kwa sababu anachokifanya ni kitu kizito na akifa kabla ya kutubia atastahiki kuishi milele Motoni.....


JE WA KWAKO YUKO KATIKA AINA IPI
1473164982788.jpg
 
mimi sipo kwenye hayo makundi, na sifa yangu ya kipekee kushinda wanaume wote hapa dunian
 
Back
Top Bottom