Je wazo langu hili likoje?

Francis Mawere

JF-Expert Member
Nov 17, 2015
958
830
Mambo vp wana Jf?

Mtu mmoja alisema kila kitu hapaduniani kishafanywa ila wewe fanya lakini fanya kwa uzuri yaani “DO IT BETTER”

Siku moja niliamua kwenda gulioni kununua Shuka kwa ajili yakutandika kitanda changu. Katika kuchagua chagua nikaona Shuka zuri kweli kweli, hakika lilinipendeza machoni kwa rangi zake zenye maua mazuri na ndipo nikaamua kulinunua kwa bei ya kawaida mno(Tsh 6000).

Nilipofika nyumbani baada ya kutoka huko ghulioni nikalifua nakulianika ili niweze kulituamia. Kwa kua mimi ni mpenda UTANASHATI, nikapata wazo zuri juu ya lile Shuka, na wazo hilo lilikua kama ifuatavyo:-

Niliwaza ya kwamba Shuka lile lenye rangi nzuri na maua yakuvutia nilipeleke kwa fundi anishone mashati mazuri yapatayo matatu kwa kua shuka lile lilikua na ukubwa wakutosha. Basi hasubuhi ilipofika nikabuni mitindo tofauti tofauti ambayo mimi napenda nikampelekea fundi wangu ili anitengenezee, hakika fundi Yule aliweza kunitengenezea mashati yale kama nilivyo tarajia tena kwa gharama ndogo tuu ambayo sikutarajia(Tsh4000 kila shati jumla ni 12000). Mpaka hapo umepata picha ya nini nataka kukupatia na sasa tuendelee,

Ikafika Siku ya kuvaa Shati lile nlilobuni mwenyewe na kutiwa nakshi na fundi wangu. Kila mtu aliye niona ile siku alinisifu kua nmependeza na amini usiamini nlikutana na mzee mmoja wa makamo akiniita wewe kijana njoo hapa nami nikasogea kumsikilaza na akaniambia.. Kwa kweli kijana shati lako limenivutia mno nikupatie shilingi ngapi ili nilichukue? Mara akatoa noti mbili nyekundu mfkoni kwake na kunipa ili nimpatie shati lile, lakini chakushangaza nilikataa ofa ile ndipo mzee Yule akaongeza tena noti nyingine nyekundu basi nikaona isiwe tabu nikaamua kumpatia mzee Yule shati lile BURE kabisa.

Kwa tukio lile la Yule mzee kupenda shati langu, nilijifunza nakugundua kitu mara moja, nikagundua kuwa UBUNIFU NILIO NAO NI WAKIPEKEE, na ndipo nikaamua kufanya kweli. Mama yangu na shangazi yangu walikua ni mafundi wakushona nguo, hivyo basi.. baba yangu alinunua Charehani zipatazo tatu ila kwa sasa charehani hizo hazitumiki kwa kuwa mama yangu na shangazi yangu hawajishughulishi na ushonaji tena, hivyo mashine hizo zipo tuu stoo.

WAZO

Kwa kutambua kipaji changu ni cha PEKEE, nmeamua kuitumia fursa hiyo ili kujiongezea kipato na kuwapatia vijana wenzangu ajira na kuachana na bahasha mkononi kila siku maofisini kutafuta kazi. Nimekwenda kuchukua mashine zile tatu ambazo ziko stoo nyumbani kwa baba nkazileta Mjini na teyari nmekwisha pata mafundi watatu ambao ni vijana waliokua tuu mtaani wakikalia vipaji vyao katika vibaraza wakipiga umbea usio na maana. Mfukoni mwangu nina mtaji mdogo sana ambao nilidunduliza kipindi nikiwa chuoni ila naamini kwa kidogo hicho nikichanganya na na wazo langu na jitihada zangu nitatimiza kile nilichokipanga. Kwa sasa mimi na mafundi wangu tunatarajia kufungua office mpya kwa ajili yakutengeneza nguo za jinsia zote kwa kutumia local resource kama hayo mashuka tunayoyaona au kuyapata katika mitumba.

Ni wazi kua kwa upekee huo nitafanya kweli nakua tofauti na wabunifu wengine ambao kila siku wameshikilia ubunifu kupitia VITENGE, ni matumaini yangu umejifunza kitu kutoka kwangu.

Je unalionaje wazo langu?
 
Hongera wazo zuri, shida ya mafundi ni uaminifu tu... Yaaani uongo na ujanja ujanja mwingi, ukiweza kupambana na Hilo utafika mbali sana, nakutabiria utakua na Kiwanda kikubwa cha Nguo Miaka kidogo ijayo.
 
Nashkuru ndugu, Ameen,
 
Ni wazo zuri sana kijana.Umeona fursa,ukaweka ubunifu halafu ukachanganya na rasilimali zilizopo una kila sababu ya kutoka kimaisha.Ongeza ujuzi hata wa ku-manage hao mafundi,utafutaji wa masoko na ukuzaji wa mtaji nk.
 
Aksnte sana Rafiki kwa mchango wako.
 
Hili ndio jambo vijana tunatakiwa kufanya kwa sasa badala ya kuwaza kuajiriwa tujaribu kufikiria vipaji tulivyo navyo ndani yetu. Hongera sana mkuu.

Sijui nikuibie wazo au lina copyright tayar
 
ha ha ha ha Mkuu hili ni wazo huru so kila mtu achukue na aongeze maufundi atakavyo ili atoke
 
Mambo vp wana Jf?

Mtu mmoja alisema kila kitu hapaduniani kishafanywa ila wewe fanya lakini fanya kwa uzuri yaani “DO IT BETTER”

Siku moja niliamua kwenda gulioni kununua Shuka kwa ajili yakutandika kitanda changu. Katika kuchagua chagua nikaona Shuka zuri kweli kweli, hakika lilinipendeza machoni kwa rangi zake zenye maua mazuri na ndipo nikaamua kulinunua kwa bei ya kawaida mno(Tsh 6000).

Nilipofika nyumbani baada ya kutoka huko ghulioni nikalifua nakulianika ili niweze kulituamia. Kwa kua mimi ni mpenda UTANASHATI, nikapata wazo zuri juu ya lile Shuka, na wazo hilo lilikua kama ifuatavyo:-

Niliwaza ya kwamba Shuka lile lenye rangi nzuri na maua yakuvutia nilipeleke kwa fundi anishone mashati mazuri yapatayo matatu kwa kua shuka lile lilikua na ukubwa wakutosha. Basi hasubuhi ilipofika nikabuni mitindo tofauti tofauti ambayo mimi napenda nikampelekea fundi wangu ili anitengenezee, hakika fundi Yule aliweza kunitengenezea mashati yale kama nilivyo tarajia tena kwa gharama ndogo tuu ambayo sikutarajia(Tsh4000 kila shati jumla ni 12000). Mpaka hapo umepata picha ya nini nataka kukupatia na sasa tuendelee,

Ikafika Siku ya kuvaa Shati lile nlilobuni mwenyewe na kutiwa nakshi na fundi wangu. Kila mtu aliye niona ile siku alinisifu kua nmependeza na amini usiamini nlikutana na mzee mmoja wa makamo akiniita wewe kijana njoo hapa nami nikasogea kumsikilaza na akaniambia.. Kwa kweli kijana shati lako limenivutia mno nikupatie shilingi ngapi ili nilichukue? Mara akatoa noti mbili nyekundu mfkoni kwake na kunipa ili nimpatie shati lile, lakini chakushangaza nilikataa ofa ile ndipo mzee Yule akaongeza tena noti nyingine nyekundu basi nikaona isiwe tabu nikaamua kumpatia mzee Yule shati lile BURE kabisa.

Kwa tukio lile la Yule mzee kupenda shati langu, nilijifunza nakugundua kitu mara moja, nikagundua kuwa UBUNIFU NILIO NAO NI WAKIPEKEE, na ndipo nikaamua kufanya kweli. Mama yangu na shangazi yangu walikua ni mafundi wakushona nguo, hivyo basi.. baba yangu alinunua Charehani zipatazo tatu ila kwa sasa charehani hizo hazitumiki kwa kuwa mama yangu na shangazi yangu hawajishughulishi na ushonaji tena, hivyo mashine hizo zipo tuu stoo.

WAZO

Kwa kutambua kipaji changu ni cha PEKEE, nmeamua kuitumia fursa hiyo ili kujiongezea kipato na kuwapatia vijana wenzangu ajira na kuachana na bahasha mkononi kila siku maofisini kutafuta kazi. Nimekwenda kuchukua mashine zile tatu ambazo ziko stoo nyumbani kwa baba nkazileta Mjini na teyari nmekwisha pata mafundi watatu ambao ni vijana waliokua tuu mtaani wakikalia vipaji vyao katika vibaraza wakipiga umbea usio na maana. Mfukoni mwangu nina mtaji mdogo sana ambao nilidunduliza kipindi nikiwa chuoni ila naamini kwa kidogo hicho nikichanganya na na wazo langu na jitihada zangu nitatimiza kile nilichokipanga. Kwa sasa mimi na mafundi wangu tunatarajia kufungua office mpya kwa ajili yakutengeneza nguo za jinsia zote kwa kutumia local resource kama hayo mashuka tunayoyaona au kuyapata katika mitumba.

Ni wazi kua kwa upekee huo nitafanya kweli nakua tofauti na wabunifu wengine ambao kila siku wameshikilia ubunifu kupitia VITENGE, ni matumaini yangu umejifunza kitu kutoka kwangu.

Je unalionaje wazo langu?

Ningetarajia kuona kazi ulizofanya kama sample
 
Back
Top Bottom