Je, watanzania wanatoa sapoti wanapotetewa au kusemewa?

Je, watanzania wanatoa sapoti wanapotetewa au kusemewa?

MURUSI

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
4,575
Reaction score
8,911
Nadhani hili ndio tatizo kuu nchi, hii yaani watu wanaamini kuwa wameletwa Duninia.kusemewa na kutetea na kwamba kuna watu special walio kuja duniani kuwatetea. Haya makato mapya mfano wafanyakazi wanayoa sapotu? Jibu ni hapana. Je, raia wanatoa sapoti? Jibu ni hapana.

Naendelea kushauri Mbowe na mtu mwingine yoyote yule mwemye nia ya kutetea watu akae kimya. Watanzania ni aina ya mazezeta, ni watu wasio jitambua chini ya jua hawa ukiwatetea utaumia mwenyewe, Sio watu wa kutetea.

Kama wafanya kazi wamekaa zaidi ya miaka 6 bila nyongeza ya mshahara na hawakufanya chochote kile sembuse tozo?

Waachwe kama hawawezi jitetea basi.

Nazani kama watu hawatoi sapotu basi hawana haki ya kuongea lolote lile.
 
Umemaliza kila kitu, kila mtu akomaye kivyake mpaka akili itukae sawa.

Sisi tupo kinafki zaidi kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake
 
Wenzetu Kenya wapo na ushirikiano, wanaelimu bora.Tanzania mnaambiwa elimu bure 🏃,muda wote mupo Instagram Kwa umbea wa diamond na zuchu
 
Watafanya nini nchi hii ambayo haina demokrasia? Watu wakiandamana watapasuliwa vichwa na kutenguliwa viuno.
 
Tozo za benk zimewagusa wafanyakazi, ila TUCTA wapo, CWT wapo, TUGHE nao wapo nk.

Umeskia hata kimojawapo kimetest mitambo? Hii nchi unafiki + ubinafsi ndio vipaumbele.
 
Back
Top Bottom