Je, Wanaoshangilia na Kupongeza Bajeti Wanajua Wanashangilia Nini? , Au Tunashangilia Ujinga?! .

Jamaa kazingua hesabu gani hizi?
 
Katika kupanga lazima upange makubwa( aim high) ndo maana inaitwa makisio sio halisi
 
Budget ya Tanzania ni kama mtu kacheza tatu mzuka akaota atashinda million 100 akaanza na kupanga kabisa nitanunua hichi na kile na anaishi kwa raha kabisa akiwa ana matumaini wakati wowote nitapigiwa simu ya ushindi lakini mara ghafla anatumiwa sms umeshinda alfu 10 hapo anapanguwa mipango anacheza tu 3 mzuka. Kawaida ya budget unapanga kwanza matumizi ya kawaida halafu ukijuwa tunamudu matumizi ya kawaida unaweka propose miradi ya maendeleo kwa vipaumbele vyenu katika pesa iliyobaki kwa maana makusanyo ya uhakika zaidi baada ya hapo miradi mingine inawekwa kwenye list kwa kusema tukipata ziada tutafanya kitu hiki hii unakuwa una review budget kila baada ya miezi 3 kuona ulichotegemea kupata na ulichopata na hapo unarekebisha number zako kwa kuangalia kwanini hatukupata tulifikiri tutapata ukijuwa sababu ndio utajuwa miezi 3 mingine utapata nini mbona haya mambo basic sana. kuna fixed cost ambayo ni matumizi ya kawaida mishahara na mambo ya kila siku ya lazima ila vitu sio vya lazima japo viko katika matumizi ya kawaida unakata ili kufidia. Budget ya mwaka jana hatukuweza kutimiza % leo bila kujuwa kwanini tunaongeza number tutapata wapi vyanzo gani? kwa kweli sijui la kusema naona siasa katika ubora wake...
 
Uzi wa Mayalla umenikumbusha ngoma za mdundiko mitaa ya Gongolamboto unaweza ukakuta ngoma.hiyo inaelekea Chanika, watoto wakajiunga kuja kushtuka wako Chanika na hata hawajui ngoma ilikuwa inahusu nini. Asante Pascal Mayala kutukumbusha tu namna ya kufikiri
 
Ni bajeti nzuri ya kizalendo.Pato la mtanzania limeongezeka kwa shs laki moja
 
Kuna mambo mengie ni magumu mkuu yaani huwezi kupandisha petroli na diesel ukaacha mafuta ya taa bei ya chini kitachofuta ni mafuta yaa kuchangwa na diesel au petrol na wafanya biashara wenye tamaa.

Mimi nashauri badala ya kila mwaka kuanzisha vyanzo vipya vya kodi jambo ambalo sio baya, waangalie pia kipi kinakwamisha kufikia lengo la makusanyo ya ndani waliojiwekea. Binafsi naona bado kuna uzembe mkubwa kwenye ukusanyaji wa kodi unaofanywa naTRA. Wananchi wengi hawana elimu ya kodi hivyo kuna mapato kibao ya serikali ambaye yanapotea kwa wananchi kutokudai risiti za EFD.

Wafanya biashara wengi hawana tabia yakutoa risiti na hata ukiwadai baadhi yao wanato zile risiti za kitabu mpka uwe mjanja ukiwabana wanakupa za EFD. Sasa jiulize ni wananchi wangapi wanamuda huo ikiwa hata elimu ya kodi haija muingia, maana hata matangazo ya uhamasishaji siku hizi hamna TRA wameshindwa hata kuwatumia wasani kuhamisisha hili jambo.

Nashauri hili swala la kudai na kutoa risiti za EFD liwanyiwe kampeni kama ilivyokuwa kwa mifuko ya plastiki ndani ya mwezi mmoja tu naamini serikali itakusanya kodi nyingi sana iliyokuwa inapotea.
 
hii bajeti ni ngumu kuipongeza sababu iliyopita pesa nyingi hazikwenda sasa sijui hii watafanya miujiza gani ili ifanikiwe

Bajeti za aina hii hukumbushia kisa cha kina ZERO hawa:

Tunazurura kitaani huku stori zikiaendelea namwambia mzururaji mwenzangu ati mara pwa linaonekana burungutu, ndani kuna millioni. Tugawane! Mimi nasema lazma nichukue laki tisa, ndoto nimeota mimi. Ngumi zinaanzia hapo!
 
Hata mm nakumbuka mwaka 1992 tuliwahi kujikuta tupo chanika toka majumba sita

Dah nimekumbuka mbali Sana Aisee😀😀
 
Mkuu Pasco, kwanza salute kwako kwa kumiliki brain yenye uwezo wa kuwaangazia wengine waone vizuri mahali walipokuwa wanadhania wanaona vizuri kumbe walikuwa wakiona ukungu tu. Pili naunga mkono bandiko lako.
 
Unapo muagiza mkeo leo pika pilau, lazima umuachie Pesa ya mchele nyama, viungo...! Unaagiza lipikwe pilau huku unaandika BILA kuacha Pesa unategemea utaikuta pilau?? hhhhhhhhh...
 
Hata mimi nimewaza sana hii hesabu lakini nikaona kwa kuwa hesabu kwangu zilinipita kushoto
 
Na bajeti ya mwaka huu ni bajeti ya 5!. Iko vile vile, mambo yale yale ni bajeti tegemezi!. Why?.
P
 

No asilimia ndogo sana budget inafuatwa an mwaka guy map to yatashuka itakuwa asilimia ndogo sana labda 20% tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…