Je, Wanaoshangilia na Kupongeza Bajeti Wanajua Wanashangilia Nini? , Au Tunashangilia Ujinga?! .

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
53,337
120,836
042301d96ce598d1b63fe51c91a92ca3.jpg

Wanabodi

Kwanza naomba nami nianze kwa kuishangilia na kuipongeza hii bajeti kwa sababu tuu watu walipiga makofi, kushangilia na kupongeza, as when you are in Rome, do as the Romans does!, lakini naomba kukiri kuwa mimi sio mchumi, hivyo sijui hata watu waliokuwa wakishangilia bajeti, wanashangilia nini?!.

Hivyo nimekuja hapa na swali kuhusu bajeti ambalo haliko based kiuchumi bali ni swali la logic tuu kuhusu bajeti yetu, kwanza tukubaliane, bajeti hii sio realistic budget, ni unrealistic kwasababu bado ni bajeti tegemezi kama bajeti zilizotangulia ambazo tunapanga kutumia fedha ambazo hatunazo, tukitegemea makusanyo ya kodi zaidi, misaada na mikopo, kisha tunaidhinisha matumizi ya fedha ambazo haziko mkononi, mwisho wa siku, fedha ambazo zimepangwa na kuidhinishwa na Bunge, zinashindwa kupatikana, lakini kitu cha ajabu kabisa, serikali yetu inakuja na matumizi makubwa ajabu ambayo, japo ni muhimu, kama ununuzi wa ndege kwa kulipa cash, lakini matumizi hayo, hayakuwa budgeted for, hayakupangwa, hayakuombwa, na hayakuidhishwa na Bunge!. Sasa kama kile tuu kilichopangwa na kuidhinishwa, hakikupatikana hicho kikubwa, kisichopangwa wala kuidhinishwa, kimetokea wapi?!.

Hoja zangu hapa ziko based on kitu kinachoitwa a common sense logic na sio economic indicators, nikijiuliza inawezaje kupanga kutumia kitu ambacho hauna, kisha unashindwa kutekeleza kile ulichokipanga kutokana na ukosefu wa fedha za utekelezaji, lakini ripoti ya CAG wako inakuja na taarifa ya matumizi makubwa ambayo hayakuidhishwa!, hizo fedha za matumizi makubwa hayo, zimetokea wapi?!

Tangu kutangazwa kwa bajeti mpya ya serikali, nime note watu wengi wakiishangilia na wakipongeza bajeti hii, mimi ambaye sio mchumi ninajiuliza hivi washangiliaji hawa wanajua wanashangilia nini? na wapongezaji wanapongeza nini?!, au nao wanashangilia tuu kwa sababu watu wanashangilia, na kupongeza tuu kwa sababu watu wanapongeza, lakini in reality hawajui wanashangilia nini au wanapongeza nini?.

Mkiwa kwenye grupu la watu, mnapata kitu kinachoitwa "a group pschology" inayotokana na "group mentality". Mfano ni wakati mtu akihutubia halafu akaibuka mtu mmoja akianzisha kupiga makofi ya kupongeza, automatically hujikuta wote mnapiga makofi bila hata kujijua, na wengine wala hawajui ni makofi ya nini au msemaji amesema nini!.

Unawezaje kuishangilia bajeti mpya kubwa kuliko bajeti ndogo iliyotangulia ambayo hiyo ndogo tuu imeshindwa kutekelezeka hata nusu tuu?!, vyanzo vya mapato ni vile vile, sasa hii budget kubwa zaidi, mtaitekeleza kwa kutumia nini?.

Ikitokea baadhi ya wapongezaji na washangiliaji, wanapongeza tuu na kuishangilia tuu kwa sababu tuu watu wamepiga makofi, lakini wakawa hawajui wanashangilia nini, jee ikiwekwa hoja kuwa wanashangilia kitu wasichokijua, jee huku kutakuwa sio kuishangilia kijinga?!. Yaani itoke bajeti hewa ya kwanza ishindwe kutekelezwa kutokana na ukosefu wa fedha huku vyanzo vya mapato vikiwa ni vile vile, halafu inaletwa bajeti kubwa zaidi kuliko ile iliotangulia na kushindikana, halafu watu wanashangilia?!. Watu hawa wanashangilia nini?!.

Wachumi wetu humu tusaidieani akina sisi tusiojua uchumi kwa kutuelimisha kuhusu bajeti hii, ili kama ni kuishangilia, basi angalau tushangilie huku tukijua tushangilie nini!.

Bajeti ya 2016/17 ilikuwa ni Trilioni 29. Tukashindwa kuitekeleza kwa kutekeleza asilimia 34% tuu ya mipango ya kibajeti kutokana na ukosefu wa fedha tulizo ahidiwa!. Sasa hii taarifa ya CAG inayoonesha tumefanya manunuzi makubwa ya ndege kwa cash money unbudgeted, bila kuidhinishwa na Bunge, fedha hizi zimetoka wapi?!.

Halafu watu wanashangilia na kupiga makofi? !. Bajeti iliyopita ni Trilioni 29, tukashindwa kuitekeleza!, Bajeti ya sasa ni Trilioni 31, vyanzo vya mapato ni vile vile, what are the chances ya kuitekeleza bajeti hii mpya?!.

Kitendo cha kupanga bajeti na kushindwa kuitekeleza ni kujikwaa, kushindwa kuitekeleza ni kuanguka, hivyo kibajeti kwa mwaka 2016, Tanzania tumejikwaa tukaanguka!. Bajeti ya mwaka huu 2017, tumeamkia hapo hapo tulipoangukia na kuendelea na safari ya bajeti mpya katika mduara ule ule bila kuangalia ni wapi tulipojikwaa mwanzo, bali tumeangalia tuu pale tulipoangukia!. Sasa bajeti hii, tumeamka na kuendelea na safari, bila kuangalia tulipojikwaa mwanzo, hivyo ni hakika tutakapofika pale pale tulipojikwaa mwanzo, tutajikwaa tena na tutaanguka tena!. Hili ni jambo la kuishangilia?!.

Najiuliza kuhusu hawa waheshimiwa wabunge wetu mule ndani Bungeni kweli wote wanajitambua wako mule kufanya nini?! au wengine mule ni washangiliaji tuu na wapiga meza huku hawajui wanashangilia nini?!.

Mimi nilidhani kabla wabunge wetu hawajaishangilia hii bajeti mpya, wangepaswa kwanza kuibana serikali, kwa kuuliza ni kwa nini imeshindwa kutekeleza bajeti iliyopita, iliyopangwa na kuidhinishwa na Bunge na bado ikashindwa kuitekeleza, lakini wakati huo huo serikali imeibuka na matumizi makubwa ya kibajeti ambayo, hayakupangwa, hayakuombwa na hayakuidhinishwa na Bunge hili, hiyo fedha imetoka wapi?, nani huyo mwenye mamlaka hayo ya kuidhinisha matumizi makubwa hivyo bila kibali cha Bunge letu? na sasa serikali imekuja na mipango gani kuhakikisha bajeti hii kubwa zaidi haitashindwa kutekelezeka kama hii iliyotangulia?!.

Watu wenye busara wanapojikwaa na kuanguka, hawajiinukii tuu na kuendelea na safari kwa kuangalia tuu walipoangukia, bali hurudi nyuma kidogo kuangalia pale walipojikwaa ili wasije wakajikwaa tena pale pale na wakaanguka tena!.

Kama bajeti hii imetangazwa bila kuelezwa sababu ni kwa nini tumeshindwa kuitekeleza bajeti iliyopita, na wakati huo huo serikali kuja na matumizi makubwa ambayo hayakuidhinishwa na Bunge, jee tulijikwaa wapi?. Kwa nini serikali ifanye matumizi ya manunuzi makubwa bila kibali cha Bunge?. Jee tatizo ni makusanyo ya kodi, kumaanisha pesa zipo ila tumeshindwa kuzikusanya tukiimarisha ukusanyaji tatizo litakuwa limeisha! , au uchumi ndio umeporomoka, hivyo hao walipa kodi hawapati hicho cha kulipia kodi?.

Dawa pekee kwa Bajeti ya Tanzania kuwa na bajeti nzuri, ni lazima sasa tupange bajeti yetu ambayo ni realistic na SMART, yenye smart objectives.

Bajeti Smart ni lazima iwe
Specific yenye vitu muhimu tunavyo vihitaji kutokana na kupanga vipaumbele vyetu. Mfano Tanzania inategemea kilimo, hivyo kipaumbele nambari moja ni maendeleo ya sekta ya kilimo.
Tunahubiri Tanzania ya Viwanda, what is the blue print ya Tanzania ya Viwanda yenye road map ya uelekeo with smart objectives?. Tunaanzisha Tanzania ya viwanda, kwanza ni viwanda vya nini, kwa malighafi gani?, kwa nguvu kazi gani?, kwa mitaji gani? Etc etc au ni Tanzania ya kauli za Viwanda?. Badala kwanza ya kujenga sekta ya kilimo ya kuzalisha malighafi ya viwanda, tunahubiri viwanda kutegemea wawekezaji kutoka nje waje na FDI? .
Jee mnajua viwanda vyote vya nguo nchini vinaagiza majora?. Jee mnajua hata ngano ya Bakhresa inaagizwa 100%?. Na hizo juices 80% ya pulp ni imported?.

Tumenunua Ndege, tunajenga reli ya SGR kwa mbwembwe wakati reli ya STD Gauge, tumeshindwa kui utilize to the full!. Tunajenga Barbara za juu kwa juu. Jee vitu hivi ni muhimu kama kufufua sekta ya kilimo?.

Measurable- Katika mahitaji yetu ya kibajeti, lazima tuwe na mipango inayopimika, jee kununua Ndege na kujenga Reli ya SGR italisaidiaje taifa ukilinganisha kama fedha hizo zingeelekezwa kwenye kilimo? . Tusifanye vitu kwa kutaka sifa tuu za kuonekanika lakini havina imediate economical value. Tutoe kwanza vipaumbele kwa sekta muhimu zitakazo inua uchumi wa taifa kwa haraka kama sekta ya kilimo, halafu ndio twendwe kwenye kutaka sifa na kuonekana kwenye hizo long term projects. Watu wanataka fedha mfukoni na mkononi kuleta chakula mezani sasa, watu wana njaa wanataka kushiba kwanza, mpaka SGR ianze kuleta faida, ni 20-30years to come, some of us would be long gone!.

Attainable-Kila tunachokipanga kwenye bajeti lazima kiwe ni kitu kibachowezekanika kupatikanika. Wewe mapato yako ni Trilioni 10? halafu unapanga bajeti ya trillion 31, wakati ukipanga hujui hizo trillion 21 utapata wapi, unafikia mwisho wa mwaka unajikuta ulifanikiwa kupata asilimia 34% tuu, kwa nini unakuja na bajeti kubwa kuliko ile ndogo iliyokushinda? . Nilidhani ni busara kupanga bajeti ya kile tuu tuna uwezo nacho, yaani cash budget ili iwe ni attainable na sio kutujia na bajeti hewa na sasa kutuongezea hewa, mwisho wa siku ni kuzidi tuu kutanua deni la taifa.

Realistic- Jee bajeti hii ya mwaka huu ni realistic au ni bajeti hewa kama ya mwaka jana? . Ili Tanzania tuweze kupata maendeleo ya kweli, we have to be real. Lazima tupange bajeti ukweli kutokana uwezo wetu wa kile tunachozalisha, haiwezekani tuendelee kutumia matumizi makubwa kuliko uwezo, ili hata kama ni kukopa, mikopo ndio itumike kwenye development budget lakini recurrent budget yetu yote kwa asilimia 100% inapaswa iwe ni kwa fedha zetu za ndani. Kitendo cha kutumia fedha zetu za ndani kununulia ndege na hii white elephant SGR wakati tumeshindwa kutimiza mahitaji muhimu, sio realistic kabisa kabisa kupanga vipaumbele vyetu.

Timely-Jee bajeti hii itatekelezwa katika muda muafaka? . Kama hii ndio the last quarter ya bajeti, na imetekezwa kwa asilimia 34% tuu, ni uthibitisho tosha kuwa hatuna timely objectives katika utekelezaji wa malengo yetu ya kibajeti, jee katika bajeti mpya, malengo ambayo hayajatekelezwa yamekuwa carried forward, au ndio abandoned na tumekuja na mengine mapya? .

Tanzania tunamtindo wa kusifiana na kupigiana makofi hata kwenye failures, kama mwaka jana bajeti ilikuwa Trilioni 29 na zimeshindwa kupatikana, serikali hiyo hiyo ikaja na matumizi makubwa ambayo hayakuidhinishwa na bunge!, waziri kama huyu bado anafanya nini pale?!. Huu ni uthibitisho wa failures, sasa anakuja na bajeti nyingine ya Trilioni 31 watu wanashangilia?. Kweli tukijiita sisi Watanzania ni watu wa ajabu sana tutakuwa tunajikosea?!. Yaani tupange bajeti, iidhinishwe na Bunge, ishindwe kutekelezwa kwa ukosefu wa fedha, halafu serikali hiyo hiyo iibuke na matumizi mengine makubwa ya fedha ambayo hayakuidhinishwa na Bunge, na bado watu wanashangilia!.
Naunga mkono kwenye mazuri kupongeza hivyo ni haki ya wabunge kupongeza mazuri yaliyoletwa katika bajeti hii, lakini kama hatujiulizi pale tuliposhindwa tulishindwa nini na badala yake kuja na bajeti mpya kubwa zaidi bila mipango madhubuti ya kuonyesha tutapata wapi fedha za kuitekeleza bajeti hii?!. Jee huku kuishangilia bajeti ya fedha ambazo hauna, yaani kushangilia tuu mipango kuwa nitafanya hiki, nitakusanya hiki, haiwezi kuwa ni kama ile ndoto ya Alinacha?. Kiukweli huku kushangilia usichonacho, sio kuishangilia ujinga?!. Jee kuna ugumu gani kama tungejipanga kwanza kutumia kile tuu tunachokusanya, tukakusanya kwanza, kisha baada ya kuona tunaweza ndipo tukapanga kutumia tulicho nacho mkononi, na kama kuna chochote ambacho tumeahidiwa na nchi wafadhili kupitia General Budget Support, tusikipangie kwanza, tusubiri, tukabidhiwe na kupokea ndipo tupange kutumia, ili ulifika wakati wa kushangilia, tushangilia matokeo lakini sisi tunashangilia mipango?!.

Wewe unaishi nyumba ya udongo iliyoezekwa kwa nyasi na usafiri wako ni baiskeli, kisha jirani yako Apeche Alolo akajitokeza na kukuahidi kukujengea ghorofa na kukununulia Range Sports, kitu cha kwanza ni kuruka ruka kushangilia, au kujiuliza why and how?. Tuambizane ukweli jameni kwa uchumi wetu huu huu wa kijungu jiko, hii bajeti ya trillion 31 tunakwenda kuitekeleza vipi?.

Ili tupate maendeleo ya kweli, Watanzania lazima tujenge utamaduni wa kuwa wakweli, kwa kujenga nidhamu ya matumizi, lazima tuje na realistic budget, tupange kutumia kile tuu tulichonacho mkononi na sio tulichoahidiwa, serikali yetu iache kabisa hii tabia mbaya ya kufanya matumizi makubwa bila kuidhinishwa na Bunge unless ni dharura kweli au majanga!, lakini dharura ya pangaboi!, kweli kulikuwa na udharura huo?!.

Pia natoa wito kwa Watanzania wenzangu, sasa tujenge utamaduni wa kushangilia matokeo, yaani results oriented achievements na sio kushangilia ahadi tuu hadi sasa kila kijiji bado kinasubiri zile million 50 zake za kila mwaka huku walimu wetu wakisubiri zile laptops zao!. Tunashangiliaje mipango badala ya kushangilia matokeo?

Namalizia kwa kulirudia hili swali la msingi la uzi huu, Jee Wanashangilia Bajeti Hii, Wanajua Kweli Wanashangilia Nini au Wanashangilia Tuu kwa Vile Watu Wanashangilia, au ndio yale yale ya Watu Kushangilia Wasichojua, ikitokea Wakaletewa hata Ujinga Tuu, Watu wa Namna Hii si Watashangilia tuu?!.

Keshokutwa Jumatatu, wabunge wetu wanaanza kuchangia bajeti hii, natoa rai kwa Bunge letu tukufu kuruhusu matangazo ya moja kwa moja wakati wabunge wetu wakijadili bajeti hii, kama waliweza kuruhusu matangazo ya moja kwa moja ya bajeti, pia tupate fursa ya kuwasikia wawakilishi wetu wakichangia bajeti hii, hivyo Bunge letu tukufu kututendea haki sisi wananchi

Jumamosi njema
Paskali
 
Tabia hizi za NDIYOOO na kugonga meza kabla ya kutafakari ndio zimetusababishia sakata la makinikia ya dhahabu, kwa mfano; bajeti inapendekeza kufuta road licence na kuhamishia tozo kwenye petroli na mafuta ya taa; jamani kuna gari linalotumia mafuta ya taa?! Why punish hawa masikini?! Unamuona mbunge mzima anashangilia kama zuzu! Selfish interests zinatufanya tunajitoa akili ili kupitisha sheria na mikataba ya hovyo hovyo, no wonder tuliizika
rasimu ya katiba ya Warioba!! God save mother Tanganyika!!!
 
Bajeti hii inaweza kutupeleka pabaya mno kuliko watu wanavo fikiri haiwezekani sekta muhimu kama kilimo haijapewa kipaumbele afu pia unapoipandsha tozo kwene mafuta basi tegemea nauli ya kusafiri itapanda sion umuhimu wa kufuta kodi road license afu unaongeza kodi ya petrol
 
Ikitokea baadhi ya wapongezaji na washangiliaji, wanapongeza tuu na kuishangilia kwa sababu tuu watu wamepiga makofi, ukitokea wengi wa washangiliaji wakawa hawajui wanashangilia nini, ikiwekwa hoja kuwa wanashangilia kitu wasichokijua, jee huku kutakuwa sio kuishangilia ujinga?
Ndugu yangu na rafiki yangu Paskali nionavyo miye KUNA TATIZO katika kufikiria kwa watu walio wengi (na hata baadhi ya wabunge wamo kundi hili), TAKWIMU bila uhalisia ni SIFURI....Yaani kusema katika familia: NTAWANUNULIA watoto woote baskeli (huku uwezo wako kama mzazi huwezi kukidhi mahitaji muhimu nyumbani kama chakula) ni URONGO mtupu. Hiki ndicho ninacho kiona katika hii kitu inayoitwa BAJETI ya Serikali...
 
Wanabodi,

Kwanza naomba na mimi nianze kwa kuipongeza bajeti na kuishangilia kwasababu tuu watu walipiga makofi, as when you are in Rome, lakini naomba kukiri kuwa mimi sio mchumi, hivyo sijui hata watu walikuwa wakishangilia nini!. Hivyo nimekuja hapa na swali kuhusu bajeji ambalo haliko based kiuchumi bali ni swali kuhusu failures za utekelezaji wa bajeti tunazopanga kwa kutumia kitu kinachoitwa a common sense logic.

Tangu kutangazwa kwa bajeti mpya ya serikali, nime note watu wengi wakiishangilia na wakipongeza bajeti hii, mimi ambaye sio mchumi ninajiuliza hivi washangiliaji hawa wanajua wanashangilia nini au wanapongeza nini? . Unawezaje kuishangilia bajeti mpya kubwa kuliko bajeti ndogo iliyotangulia ambayo imeshindwa kutekelezwa?!. Ikitokea baadhi ya wapongezaji na washangiliaji, wanapongeza tuu na kuishangilia kwa sababu tuu watu wamepiga makofi, ukitokea wengi wa washangiliaji wakawa hawajui wanashangilia nini, ikiwekwa hoja kuwa wanashangilia kitu wasichokijua, jee huku kutakuwa sio kuishangilia ujinga?. Yaani itoke bajeti hewa ya kwanza ishindwe kutekelezwa halafu inaletwa bajeti kubwa zaidi halafu watu wanashangilia?!. Wachumi wetu humu tusaidieani akina sisi tusiojua uchumi kwa kutuelimisha kuhusu bajeti hii, ili kama ni kuishangilia, tujue tushangilie nini?.


Naunga mkono kwenye mazuri kupongeza hivyo ni haki ya wabunge kupongeza mazuri yaliyoletwa katika bajeti hii, lakini kama hatujiulizi pale tuliposhindwa tulishindwa nini na badala yake kuja na bajeti mpya kubwa zaidi bila mipango madhubuti ya kuonyesha tutapata wapi fedha za kuitekeleza, huku kuishangilia bajeti nakuita ni kuishangilia ujinga!.

Namalizia kwa kulirudia hili swali la msingi la uzi huu,;Jee Wanashangilia Bajeti, Wanajua Wanashangilia nini au ndio yale yale ya Kushangilia Ujinga wa Wasichojua?.

Keshokutwa Jumatatu, wabunge wetu wanaanza kuchangia bajeti, natoa rai kwa Bunge letu tukufu kuruhusu matangazo ya moja kwa moja wakati wabunge wakijadili bajeti, kama waliweza kuruhusu matangazo ya moja kwa moja ya bajeti, pia tupate fursa ya kuwasikia wawakikishi wetu wakichangia bajeti hiyo hivyo kututendea haki sisi wananchi

Jumamosi njema
Paskali
Mimi bado sijashangilia wala kuiponda maana sijaisoma kusema kweli. Niaionea uvivu maana NAHISI haina tofauti kubwa na zilizopita.
 
Wanabodi,

Kwanza naomba na mimi nianze kwa kuipongeza bajeti na kuishangilia kwasababu tuu watu walipiga makofi, as when you are in Rome, lakini naomba kukiri kuwa mimi sio mchumi, hivyo sijui hata watu walikuwa wakishangilia nini!. Hivyo nimekuja hapa na swali kuhusu bajeji ambalo haliko based kiuchumi bali ni swali kuhusu failures za utekelezaji wa bajeti tunazopanga kwa kutumia kitu kinachoitwa a common sense logic.

Tangu kutangazwa kwa bajeti mpya ya serikali, nime note watu wengi wakiishangilia na wakipongeza bajeti hii, mimi ambaye sio mchumi ninajiuliza hivi washangiliaji hawa wanajua wanashangilia nini au wanapongeza nini? . Unawezaje kuishangilia bajeti mpya kubwa kuliko bajeti ndogo iliyotangulia ambayo imeshindwa kutekelezwa?!. Ikitokea baadhi ya wapongezaji na washangiliaji, wanapongeza tuu na kuishangilia kwa sababu tuu watu wamepiga makofi, ukitokea wengi wa washangiliaji wakawa hawajui wanashangilia nini, ikiwekwa hoja kuwa wanashangilia kitu wasichokijua, jee huku kutakuwa sio kuishangilia ujinga?. Yaani itoke bajeti hewa ya kwanza ishindwe kutekelezwa halafu inaletwa bajeti kubwa zaidi halafu watu wanashangilia?!. Wachumi wetu humu tusaidieani akina sisi tusiojua uchumi kwa kutuelimisha kuhusu bajeti hii, ili kama ni kuishangilia, tujue tushangilie nini?.


Naunga mkono kwenye mazuri kupongeza hivyo ni haki ya wabunge kupongeza mazuri yaliyoletwa katika bajeti hii, lakini kama hatujiulizi pale tuliposhindwa tulishindwa nini na badala yake kuja na bajeti mpya kubwa zaidi bila mipango madhubuti ya kuonyesha tutapata wapi fedha za kuitekeleza, huku kuishangilia bajeti nakuita ni kuishangilia ujinga!.

Namalizia kwa kulirudia hili swali la msingi la uzi huu,;Jee Wanashangilia Bajeti, Wanajua Wanashangilia nini au ndio yale yale ya Kushangilia Ujinga wa Wasichojua?.

Keshokutwa Jumatatu, wabunge wetu wanaanza kuchangia bajeti, natoa rai kwa Bunge letu tukufu kuruhusu matangazo ya moja kwa moja wakati wabunge wakijadili bajeti, kama waliweza kuruhusu matangazo ya moja kwa moja ya bajeti, pia tupate fursa ya kuwasikia wawakikishi wetu wakichangia bajeti hiyo hivyo kututendea haki sisi wananchi

Jumamosi njema
Paskali
Katika hii bajet mpya kwa ushangiliaji ule, nahisi wabunge wa ccm wanajua nini kinakwenda kufanyika ili itekelezeke, na watakuwa baadhi yao wanaoaminika walitonywa. Huenda fedha 70% ya bajet iliyopita ambazo hazikutolewa na serikari plus zitakazokusanywa 17/18 kiasi 40% zitatekeleza bajet shangiliwa na hapo tutaambiwa serikali imefanikisha. Ni mawazo tu, wataalamu wa fedha tuambìeni kama ìnawezekana.
 
Katika hii bajet mpya kwa ushangiliaji ule, nahisi wabunge wa ccm wanajua nini kinakwenda kufanyika ili itekelezeke, na watakuwa baadhi yao wanaoaminika walitonywa. Huenda fedha 70% ya bajet iliyopita ambazo hazikutolewa na serikari plus zitakazokusanywa 17/18 kiasi 40% zitatekeleza bajet shangiliwa na hapo tutaambiwa serikali imefanikisha. Ni mawazo tu, wataalamu wa fedha tuambìeni kama ìnawezekana.
Umekielewa ulichoandika au na wewe ni mmoja wa washangiliaji
 
Mimi naomba matangazo ya moja kwa moja na upande wa pili ili tuweke rekodi sawa!
Kuna watu walishangilia mpaka wakainuka kwenye viti....

Ili mambo yakienda vibaya tusiwahukumu wasiohusika
 
Back
Top Bottom