Je wanafunzi wenye mimba wakubaliwe darasani

Je wanafunzi wenye mimba wakubaliwe darasani

ishuguy

Member
Joined
Nov 3, 2007
Posts
76
Reaction score
10
Hivi wanafunzi wa primary/secondary skuli wanaweza kuingia darasani wangali wajawazito? badala ya kufukuzwa kama ilivyosasa,kwani ni haki yao ya msingi kupata elimu.
Vijana wengi walio katika mahusiano ya kimapenzi hawajui hali ya wenziwao katika mahusiano hayo. wengi katika mahusiano ya kimapenzi huanza kufanya mapenzi salama, lakini baadae kuacha kutumia kinga baada ya kuzoeana,hapo ndipo wanakuwa katika hatari ya kupata mimba na magonjwa mengine ya zinaa.
Na hapo ndio huwa ngumu kwa wapenzi hao kuenda kupima hali zao.
 
sasa hao watoto si watachochewa kufanya ngono, kama watakuwa na uhakika wa kuingia darasani na matumbo yao
 
Hiyo ni sawa na kuwapa hao watoto go ahead ya kuchapa ngono..
mtoto umleavyo ndivyo akuavyo....
 
Nivyema zitumike kila njia kudiscourage mapenzi na hata mimba ktk umri mdogo hasa adhabu kali kwa wanaowapa mimba na hata wale wanaowaweka kwenye mazingira shawishi eg. Mama kumtaka mwanae wa kike kigori kumsaidia kazi ya kuuza grocecy etc. Lakini si sahihi kumyima huyu mtoto haki ya kupata elimu.

Elimu ni haki ya msingi na kila mtu lazima apate, kupata ujauzito kunaweza tu kumuathiri muda wa kuhitimu shule yake lakini asifukuzwe. Tutakuwa tunajiweka mbali sana na malengo ya milenia ya kufuta ujinga au kushawishi sana watoto kutoa mimba jambo ambalo ni kinyome cha imani na maadili kama tutaendelea kuwaondolea baadi ya haki zao za msingi kwa kigezo tu cha ujauzito.

Tutumie kila njia kuhakikisha hili halitokei ila baada ya kutokea haina maana tuwanyime haki hawa watoto.
 
Back
Top Bottom