Je wanafanyaje!! Mobile money??

Bashatu

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2015
Posts
839
Reaction score
893
Wanabodi natumai hamjambo, mnaendelea kujenga viwanda.
Nimekuwa najiuliza maswali kuhusu huduma za kifedha kwa njia ya simu, mathalan M-pesa, tigo-pesa, airtel money zinavyofanya kazi.
Mimi napenda sana computerization, naomba majibu hapa.
Mimi Bashatu naenda m-pesa wakala, wakala anafanya yake, napata message na hapo hapo mtu nnayemtumia anapata message, anaenda kwa wakala, anapewa cash!! How does it work[emoji51] [emoji51]
Hilo sawa nijifanye nimeelewa. Je pale nnapoomba mkopo toka m-pawa, nkapewa mkopo huo, inamaana vodacom wanaweka hela kwa ajili ya kuwakopesha watu, ama kuna programming mechanism ambayo inawapa wamiliki wa mtandao uwezo wa kutengeneza sms kwa mteja anapoomba huduma ya kukopeshwa inayoonesha kuwa mwombaji amengiziwa kiasi cha pesa??
Mengine yoote yaache, naomba programmer mnieleweshe tafadhari.
Kuna kapuni ya mikopo kwa njia ya simu inaitwa The Branch, Je, nao wanaweka pesa kabla ya kuwakopesha wateja??, kama ndio, hizo soft money wanapata kutoka wapi/wanazinunua wapi?.
How do they do it??
Karibuni kwa majibu.
 
Mkuu mfano wakala wa mpesa au tigo ela anayokuwa nayo kwenye simu inaitwa float, anaiweka kupitia bank au mtu akija akatoa ela.
Yani ile ukimpa ela akuwekee 10,000, ujue hiyo 10,000 kaipunguza kwenye ela aliyoweka bank akatushiwa float kwenye simu au kuna mtu aliyekuja akamrushia float yeye akampa pesa halisi.
Inshort hakuna ela inayotengenezwa ni kwamba ela inayokuwa kwenye system ni sawa na pesa halisi iliyohifadhiwa mahali.
Unless kama unaongelea cryptocurrence kama bitcoins hiyo ni habari nyingine hiyo ni kuanzisha pesa...
 
Asante kwa maelezo. Kwa hiyo, system inaendeshwa na bank. Yaan wakala anaenda bank anadeposit, anapata float ambayo anaitumia kuuza.
Je pale vodacom anaponikopesha pesa kupitia m-pawa au Branch wanaponikopesha pesa na wanaenda bank kwanza kununua float?
 
System haiendeshwi bank, ila wametengeneza mfumi ambao uko linked na bank ambapo unaweza deposite ela ikaingia kwenye akaunt yao wakakupa float kama ambavyo siku hizi pia unaweza tuma ela kwenda bank kwenye account yako kupitia float uliyonayo kwenye simu.
Yani hakuna ela unayopewa ambayo hainvolve pesa ya kweli kwenye mzunguko.
Mfano umepewa mkopo 10,000 utaenda kwa wakala utamrushia 10000 kama float atakupa ela halisi, hiyo 10000 uliyomrushia wakala ujue iko sehemu kama pesa halisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…