Je, walokole wa enzi za miaka ya 90 bado wapo kwenye ule ubora wao?

masare

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
1,779
1,812
Hili ni swali la changamoto kuhusu ndugu zetu hawa Wakristu wa Madhehebu ya Kipentekoste maarufu kama "Walokole". Ikumbukwe kuwa Ulokole kwa hapa Tanzania ulishika kasi sana miaka ya '80 na mwanzoni mwa '90.

Enzi hizo ulikua ukisikia Mlokole basi ni Mlokole kwelikweli na hata akiwepo mtaani kwenu Mlokole mmoja tu basi alikua akijulikana kwa utofauti wake hususani ukilinganisha na Wakristo wa Madhehebu mengine.

Baadhi ya tabia, vitu au mazoea mengine ambayo yalionekana kama ni kawaida kwa Wakristu Walokole(wale wa enzi hizo) hawakufanya.

NAORODHESHA hapa baadhi tu (mengine wadau wataongezea)

-Ilikua ni nadra sana kusikia Mlokole anaumwa hata Malaria tu.
-Ilikua ni nadra sana kusikia familia ya kilokole iwe Mke, Mume au Watoto kuumwa ugonjwa wowote.
-Ilikua nadra sana Mlokole kuimba nyimbo za asili/za makabila.
-Ilikua nadra sana kukuta Mlokole akijihusisha na mambo ya michezo kama mpira wa miguu, basketball au "draft".
-Ilikua nadra sana kusikia Mlokole ana boyfriend/girlfriend (Ilikua ni uchumba ukifuatia na ndoa tu).
-Baadhi ya Walokole walikua hawali "kitimoto".
-Baadhi walikua hawatumii baadhi ya vinywaji hata kama ni non alcoholic.
-Ilikua ni marufuku kumkuta Mlokole Bar au kwenye sehemu yoyote ya Starehe hata. kama sehemu hiyo ni ya waziwaziwaziwazi/au hata kama anakunywa soda
-Ilikua hairuhusiwi kufunga harusi wakati mke akiwa mjamzito au ameshazaa mtoto.

.......nyingine ongezea

SWALI KUU; Je Walokole kama wa enzi hizo bado wapo hadi kizazi hiki cha "kidigitali"? Nauliza hivi kwasababu juzikati nilihudhuria ibada ya harusi kwenye dhehebu moja la Walokole (lenye msimamo mkali kuhusu mambo ya ndoa) lakini cha kushangaza nikaona jamaa anamuoa mke ambaye ana mimba kubwa tayari inayoonekana.

Nakumbuka Walokole wa enzi zile walifundisha kuwa Madhehebu mengine yanayoruhusu kufungisha ndoa wakati mke ni mjamzito au ameshazaa tayari ni kinyume na Biblia. Walokole walisisitiza kuwa hadi siku ya kufungishwa harusi ndio inaruhusiwa "kupeana tunda" na si vinginevyo.

Ni nini kimetokea hadi nduguzetu hawa Walokole wamebadili gia angani kuhusiana na mafundisho na ubora wao kama ule wa enzi za '90.

Karibuni kutiririka
 
Hawakuwa wanavaa vimini na kujiremba kwa namna ya kutamanisha kama siku hizi
ilikuwa ni haramu kwao kuweka dawa kwenye nywele.
 
Ndiyo, japo changamoto za maisha ya wokovu ya sasa ni nyingi. Na utandawazi huu, demu (mwana kwaya) unamtongoza kwenye simu, unakutana naye gest unamaliza kazi bila wapendwa wenzako kukushtukia.
Pia kutokana na ugumu wa maisha na kuongezeka kwa gharama za kuishi, inabidi mtu uwe mwizi mwizi ofisini, ni kudokoa vi pesa vya muajiri ili kusukuma maisha.
Kweli maisha ya sasa ya wokovu yana changamoto nyingi sana.
 
Hata mazingira yanabadirikaga mkuu ijapo kuwa kuna baadhi ya maeneo yamehifadhiwa.
 
Jinsi ulivyogundua hivyo ujue waliobaki ndio watakao urithi ufalme wa Mungu. Shetani ameliteka kanisa kuanzia kwa wachungaji. Hivyo usishangae kuona haya maana hata katoliki ya mwanzo haikuwa hivi. Ukumbuke mstari huu "waitwao ni wengi lakini wateule ni wachache".
 
Kwani wewe ulivyokuwa unaishi miaka ya tisini ndio unavyoishi leo?
 
Usishangae eti Walokole wamebadilika. Siku za mwisho zimekaribia sana.

Neno la Mungu kwenye 2 Tim 3:1-5 linasema:-
Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.

Kwa ufahamisho wako, SHETANI SASA HIVI ANA AJENDA MOJA KUU:-nayo ni:- Kuangusha watumishi wa Mungu. Wale mabinti unaowaona wakienda kanisani au kwenye huduma wakiwa nusu uchi wengi wao ni ma-agent (mawakala) wa shetani. Kazi yao moja kubwa waliyopewa na shetani ni kuingia kwenye ngono na watumishi wa Mungu. Binti anapewa 'dawa ya mvuto,' akienda kwa mchungaji/mtumishi na huo mvuto, kama huyo mtumishi/mchungaji hana nguvu nyingi za Mungu anajikuta ameshamtamani huyo binti. Na kwa vile Yesu alishasema ukimwangalia mwanamke kwa kumtamani tayari umezini, huyo mtumishi anayemtamani huyo binti anakuwa tayari ameshazini naye kwenye moyo wake. Kinachobaki ni kufanya tendo lenyewe mubashara tu.

Mchungaji/mtumishi akishalala na huyo binti 'ameisha' maana huyo binti anakuwa amewekewa mapepo lundo ili yamvae mtumishi atakayelala naye.

Habari ndio hiyo. Usishangae watu wamebadilika sana, hata wachungaji na watumishi ambao walikuwa na nguvu nyingi za kiroho miaka ya nyuma.
 
Back
Top Bottom