Kwenye vita dhidi ya shetani, Walokole wapo mstari wa mbele

Yuda Legacy

JF-Expert Member
Jun 21, 2023
534
1,746
Habari niende direct kwenye topic katika vita hii ya kumshinda shetani Walokole pekee ndio walio mstari wa mbele frontline katika vita hii ya kumpinga shetani hata ukiingia makanisa ya kilokole watu wapo fit kwenye Maombi wanaomba kwa nguvu MNO.

Kuliko makanisa yote na Huo ndio ukweli kwamba katika vita hii ya kumshinda shetani walio frontline ni Walokole Pekee na ndio maana Walokole wengi pia ukiwaangalia Kimwili wamechoka kwa sababu kwenye vita hii wako mstari wa Mbele kama ujuavyo katika vita yoyote ile watu walio frontline ndio huwa wamechoka sana kwa sababu mda wote wanakwepa mabomu,Visu, nk.

Hivi tanzania hii kuna watu wanaomba kwa nguvu kama Walokole?? Inabidi tuwape heshima yao Walokole maana wao ndio wanao simama Mbele ya vita mishale ya umasikini Kutoka kwa yule mwovu inawapata wao mishale ya uhaba wa chakula wao kwa Kifupi mlokole ni mwanajeshi wa Kristo alie halisi Asie choka choka.
 
Attachments

  • Screenshot_2023-09-17-07-52-04-02.jpg
    Screenshot_2023-09-17-07-52-04-02.jpg
    46.9 KB · Views: 4
Bahati nzuri utakuwa umesikia habari za Roho MTAKATIFU!

Kuna sala na Maombi na pia Ibada!

Ukweli ni kwamba Kila Mtu anayo Roho na kama ilivyo Roho basi Roho wa Mungu ndiye Baba wa Roho Zote!

Sisi sote ni watoto wa Mungu kwa kuwa Roho zetu zote zimetokana na Mungu!

Na kila Roho inapozaliwa ktk Mwanadamu inakuwa na KAZI MAALUMU KADIRI YA mpango wa Mungu!

Roho inayozaliwa na Mwanadamu inakuja kupoteza Dira yake kwa kuwa inapata tafsiri ya Mambo mengi tofauti tofauti kupitia responder au desk top ambayo ni UBONGO!

UBONGO unazidiwa na MAMILIONI YA TAARIFA ZINAZOINGIA KWA WAKATI MMOJA na hivo kuleta majawabu yasiyohitajika...na kwa muda mrefu baadae Mwanadamu hupoteza DIRA YAKE.. LOSS OF A PURPOSE OF LIFE!

Ili kupata Message sahihi na za Ukweli ni kuweza kuwasiliana na Roho MTAKATIFU ambaye yeye anayo ramani ya Maisha yako yote kupitia Roho yako!

HAPA UNAHITAJI UTULIVU MKUBWA SANA!!!

SALA ni kuongea na Mungu!

Mungu anatoa ujumbe ndani ya utulivu mkubwa sana!!!

Siyo kwa makelele!

Ndugu zetu wa Roma especially Mapadri wana kitu kinaitwa Re treat...au Mafungo!

Hizi hufanyika ndani ya Maeneo TULIVU SANA...pengine Bustanini au popote penye Utulivu sana!!

Positively,focused and meditatively you get the best out of yourself!

Makelele katika sala na Maombi yanatengeneza kitu kinaitwa Hallucination....na mwisho hupati kitu sahihi!

Ni mapicha picha tu!

Walokole wapunguze makelele!

Watulie!!

Waongee na Mungu anayesikia!

Kwa utaratibu!
 
Hapana mkuu mchawi anapokuja kukuroga anakuja na nguvu HAJI kirahisi rahisi kuna nguvu Iliyo mleta na Ukumbuke Mungu Ni mwenye Haki Sasa Kwa Sababu Ni Mungu Anayesikia Eti ndio uombe kwa uchovu chovu wakati huyo mchawi kuna nguvu Iliyo Mleta sijui kama utashinda.
 
Sikiliza wewe! Unatakiwa kupambana dhidi ya Shetani kwa kutumia akili nyingi. Na siyo kwa kupiga makelele hovyo, na kuzunguka na hayo mavipaza sauti yenu kila kona.
 
Ulokole ni ulevi kama ulevi mwingine, Mungu hahitaji kupigiwa kelele na maneno mengi ili asijue, anasikia hata kusali kimoyomoyo. Au Mungu wa walokole ana matatizo ya masikio? Yesu alifundisha kuwa usalipo usiwe kama wanafiki wafanyavyo ambao hudhani watasikilizwa kwa wingi wa maneno yao.....
Mkuu hamnaga vita ya kimya kimya ndio maana hata bunduki ukiifyatua lazima itoe sauti tena kali
 
  • Thanks
Reactions: apk
Habari niende direct kwenye topic katika vita hii ya kumshinda shetani Walokole pekee ndio walio mstari wa mbele frontline katika vita hii ya kumpinga shetani hata ukiingia makanisa ya kilokole watu wapo fit kwenye Maombi wanaomba kwa nguvu MNO.
Wengine wote wanahubiri makusanyo
 
Unasema ni maaskari waliochoka sana, halafu wapo mstari wa mbele.... unatarajia ushindi upi?
 
Sikiliza wewe! Unatakiwa kupambana dhidi ya Shetani kwa kutumia akili nyingi. Na siyo kwa kupiga makelele hovyo, na kuzunguka na hayo mavipaza sauti yenu kila kona.
Shetani haiitajiki akili kupambana nae bali neno la Mungu linalo kuja na sauti kali ya Mlokole ukitumia akili utaenda Kimwili jambo ambalo ni ngumu kumshinda shetani maana shetani ni Roho chafu iliyojaa laana nzito
Kasome waefeso 6:12
 
Fuata huu ushauri wangu ili umshinde Shetani kwa urahisi zaidi. Wewe pigana naye kwa kutumia akili nyingi tu. Utamshinfa.

Ila ukitumia hiyo njia ya kupiga makelele hovyo, wapita njia watakuona umechanganyikiwa eti.
 
Sikiliza wewe! Unatakiwa kupambana dhidi ya Shetani kwa kutumia akili nyingi. Na siyo kwa kupiga makelele hovyo, na kuzunguka na hayo mavipaza sauti yenu kila kona.
Utapambanaje na shetani kwa kutumia akili wakati hata theluthi tu ya akili zake humpati.
 
Back
Top Bottom