Je, Wakimbizi wakipewa uraia ni halali kubadilishwa kabila?

Maguge Maguge

JF-Expert Member
Sep 1, 2016
2,734
1,778
Habari za jumapili ndugu zangu!

Nina wiki sasa nikitafakari nilichokiona, kukifanyia utafiti kwa uhakiki na kukithibitisha.

Wakimbizi toka Burundi, walioko kambi za Mishamo na Katumba wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi walipewa uraia kabla ya uchaguzi, na hivyo kupata haki kuitwa watanzania, na walishiriki hata kupiga kura uchaguzi mkuu uliopita.

Kilichonishangaza ni pale ambapo, vyeti vya uraia, penye box la kabila walijaziwa kabila la Muha!

Je hii ni sawa?
 
Kiongozi hawawezi kua watusi au wahutu sababu hayo makabila Tanzania hayapo, wamewaita waha sababu wanafanana na warundi hata lugha wanasikilizana...
 
Ndiyo uelewe kwamba hakuna kitu kama Kabila Tanzania, hilo unaloita Kabila lilianzishwa na Mzungu kabla ya Mzungu halikuwepo, hata wewe ukitaka leo unaweza kuchukuwa kundi fulani na kuliongezea kwa wanaoitwa Wachaga au sijui Wagogo, Kabila ni man made!
 
Kwa mantiki hiyo unamaanisha hawakuwa wakimbizi basi maana kule walikotoka hilo kabila halipo
 
Ndiyo uelewe kwamba hakuna kitu kama Kabila Tanzania, hilo unaloita Kabila lilianzishwa na Mzungu kabla ya Mzungu halikuwepo, hata wewe ukitaka leo unaweza kuchukuwa kundi fulani na kuliongezea kwa wanaoitwa Wachaga au sijui Wagogo, Kabila ni man made!
Sasa, hii ina maana gani ikiwa kuna mahala lazima mtu utaje kabila?
 
Habari za jumapili ndugu zangu!

Nina wiki sasa nikitafakari nilichokiona, kukifanyia utafiti kwa uhakiki na kukithibitisha.

Wakimbizi toka Burundi, walioko kambi za Mishamo na Katumba wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi walipewa uraia kabla ya uchaguzi, na hivyo kupata haki kuitwa watanzania, na walishiriki hata kupiga kura uchaguzi mkuu uliopita.

Kilichonishangaza ni pale ambapo, vyeti vya uraia, penye box la kabila walijaziwa kabila la Muha!

Je hii ni sawa?
Ha ha ha inawezekana ni elimu ndogo ya afisa mwandikishaji kuhusu mambo ya cultural anthropology, hivyo anaandika vusivyokuwepo, au chuki kwa sisi waha kuwa sote ni warundi.

Nina hakika wapo waha wanakaa burundi hasa maeneo ya mipakani na hivyohivyo warundi kukaa tanzania maeneo ya mipakani.

Burundi ina makabila matatu tu, ambayo ni Wahutu-majority, Watutsi-wa pili kwa wingi na Watwa the minority.

Sasa kwa kuwa walipewa urai, ingekuwa busara kutambua kundi jipya watu kuongezeka. Watutsi tzania tunao, lkn sina hakika kama tuna wahutu na watwa. Hivyo kwa maoni yangu wangetambuliwa kwa makabila yao.

Pengine ukutwe walitishwa kuwa ukisema mhutu au mtwa utarudishwa kwenu, ni figisu tu za waandikishaji
 
Kiongozi hawawezi kua watusi au wahutu sababu hayo makabila Tanzania hayapo, wamewaita waha sababu wanafanana na warundi hata lugha wanasikilizana...
Lugha kusikilizana hakuhalalishi kuvunja utambulusho wa mtu, ndo elimu duni yenyewe kwenye elimu ya utambulisho wa mtu.

Kama lugha zikiingiliana unapoteza kabila la mtu, kwa nini hadi leo wapo wajita, wakerewe na wakara?
 
Ndiyo uelewe kwamba hakuna kitu kama Kabila Tanzania, hilo unaloita Kabila lilianzishwa na Mzungu kabla ya Mzungu halikuwepo, hata wewe ukitaka leo unaweza kuchukuwa kundi fulani na kuliongezea kwa wanaoitwa Wachaga au sijui Wagogo, Kabila ni man made!
Siyo kweli mkuu, soma tena cultural anthropology
 
Ha ha ha inawezekana ni elimu ndogo ya afisa mwandikishaji kuhusu mambo ya cultural anthropology, hivyo anaandika vusivyokuwepo, au chuki kwa sisi waha kuwa sote ni warundi.

Nina hakika wapo waha wanakaa burundi hasa maeneo ya mipakani na hivyohivyo warundi kukaa tanzania maeneo ya mipakani.

Burundi ina makabila matatu tu, ambayo ni Wahutu-majority, Watutsi-wa pili kwa wingi na Watwa the minority.

Sasa kwa kuwa walipewa urai, ingekuwa busara kutambua kundi jipya watu kuongezeka. Watutsi tzania tunao, lkn sina hakika kama tuna wahutu na watwa. Hivyo kwa maoni yangu wangetambuliwa kwa makabila yao.

Pengine ukutwe walitishwa kuwa ukisema mhutu au mtwa utarudishwa kwenu, ni figisu tu za waandikishaji
Mambo hubadilika na walimwengu pia hubadilika vizazi, sasa huko mbele yakijitokeza ya kutaka kuwatambua watawatambuaje?
Au ndo itakuwa hata waha nao watambuliwe kama waliopewa uraia?
 
Lugha kusikilizana hakuhalalishi kuvunja utambulusho wa mtu, ndo elimu duni yenyewe kwenye elimu ya utambulisho wa mtu.

Kama lugha zikiingiliana unapoteza kabila la mtu, kwa nini hadi leo wapo wajita, wakerewe na wakara?
Umeona eee!
Wanyamwezi na wasukuma wanasikilizana, lakini mbona wote hawaitwi kwa kabila moja?
 
Ha ha ha inawezekana ni elimu ndogo ya afisa mwandikishaji kuhusu mambo ya cultural anthropology, hivyo anaandika vusivyokuwepo, au chuki kwa sisi waha kuwa sote ni warundi.

Nina hakika wapo waha wanakaa burundi hasa maeneo ya mipakani na hivyohivyo warundi kukaa tanzania maeneo ya mipakani.

Burundi ina makabila matatu tu, ambayo ni Wahutu-majority, Watutsi-wa pili kwa wingi na Watwa the minority.

Sasa kwa kuwa walipewa urai, ingekuwa busara kutambua kundi jipya watu kuongezeka. Watutsi tzania tunao, lkn sina hakika kama tuna wahutu na watwa. Hivyo kwa maoni yangu wangetambuliwa kwa makabila yao.

Pengine ukutwe walitishwa kuwa ukisema mhutu au mtwa utarudishwa kwenu, ni figisu tu za waandikishaji
Tanzania hatuna kabila la watutsi wala wahutu, hao wote wamekuwa wakijipachika ukabila wa waha na wahaya ili kama kinga ya kutokamatwa na maafisa uhamiaji. Wewe ni mtutsi kwa sababu nakujua.
 
Na mi nakujua wewe si mganda? Ha ha ha mhaya buana!

Watutsi, waha, wahutu, wahangaza, watwa ni makabila ambayo yapo magharibi mwa ukanda wetu.
 
Bob hapo hakuna namna lazima wajiite ivo tu kwamfano wale Watutsi wafugaji waliopo Tz wanajiita WASUKUMA hii noma sana
 
Tanzania hatuna kabila la watutsi wala wahutu, hao wote wamekuwa wakijipachika ukabila wa waha na wahaya ili kama kinga ya kutokamatwa na maafisa uhamiaji. Wewe ni mtutsi kwa sababu nakujua.
Ukiwa buha, ni ngumu sana kumpata mhutu, lkn kumpata mtutsi ni rahisi sana.

Uzuri umesema wanajipachika, which means kuna ukweli wanauweka kando kwa kuogopa kusemwa vibaya.

Soma hapa
Ethnic groups in Burundi - Wikipedia
 
Back
Top Bottom