Je, wakimaliza kununua wapinzani kitafuata nini?

Je, wakimaliza kununua wapinzani kitafuata nini?

nwapenda makamanda,ila hii ya kununua wapinzani sitaiamini hii kitu mpaka kufa…lol
 
Upinzani si chama bali ni watu wenye mawazo tofauti,kila sehemu upo hata ndani ya wajionao ni wamoja kuna upinzani,
Hivyo basi upinzani hautakufa milele,hata wakinunua chama kizima
Hata ndani ya ndoa upinzani IPO [emoji1] [emoji1]
 
Nakujib swali la kwanza, kuwa ccm inajiamin maana serikali n ccm, jesh ni wao, mahakama ni wao, usalama ni wao, n.k
Sasa kwann wasijiamin
 
Mkuu tujiulize kwanza. Kwanini wananulika
Umeuliza vema kbsa.Kosa la Chadema ni kuingiza Mamluki 2015 na kuacha vijana waliokulia bavicha.Ukiangalia Siha,Ukonga,Monduli wote waliojitoa walikuwa ccm walijitoa 2015.Cha kusikitisha Ss Monduli wanampigia chapuo Fredy Lowasa ambao ni walewale wasio na mizizi ya chadema.Swali ni je mfano Monduli hakuna vijana au watu walijenga chama toka zamani enzi ya Dr Slaa wa 2008?
 
Wakimaliza kununua wapinzani,wataanza kuua rai wasiyo na hatia.
 
Kama ni wapinzani kweli kweli, kwanini wakubali kununuliwa? Una ushahidi wa kununuliwa kwao?
 
Naamini sasa wataenda kununua Kero zetu zitusumbuazo na hapo ndo watakapokuwa wanafanya kile tukitakacho.

Ila nasikiyika itakuwa ishaingia 2020. So tutaongeza wengine lukuki. Hii Biashara ya utumwa itazidi kuendelea tu.
 
hakuna kitakachofuata maana hawawezi kumaliza kununua wapinzani
 
Umeongea vyema sana mkuu ila kuna mahali umeteleza najua wewe ni binadamu ila ukianza kutoa hoja za ajira na mikopo hapo unakosea hakuna serikali iliyojitahidi kutoa mikopo ya elimu ya juu kama hii mzee na malalamiko yamepungua sana ama kwasababu sasa hivi wamejua njia za kuthibiti hii nasema kwasababu ni mnufaika na huwezi kukwepa kulipa popote duniani
.
.
La pili kuhusu ajira nimeangalia takwimu za miaka kumi ya mtangulizi wa raisi huyu aliepo madarakani na za mtangulizi wake nimeona miaka kumi ya jk ni miaka miwili na nusu ya huyu so hoja ya ajira usiingize na kwa taarifa yako issue ya ajira ni global issue leo hii shirika la takwimu south africa wameonyesha un employnment rate imepaa sana kutoka 26% mpaka 27%
.
.
Kinachoniumiza ni kuharibu upinzani ambao ndio uliomleta raisi huyu madarakani bila upinzani imara asingetokea magufuri imara nadhani hapo ndio kunatatizo

Sawa MKUU kama ndiyo hivyo Kwa nini CCM kila MTU anaikataa? Nipe sababu ninaamini kwamba ni chama chenye dola, na tunataka kila raia wafurahie matunda ya utawala wa awamu ya Tano sio kupambana na Polisi. Nisaidie jibu tafadhali.
 
Naamini sasa wataenda kununua Kero zetu zitusumbuazo na hapo ndo watakapokuwa wanafanya kile tukitakacho.

Ila nasikiyika itakuwa ishaingia 2020. So tutaongeza wengine lukuki. Hii Biashara ya utumwa itazidi kuendelea tu.
Ingekuwa hivo kinondoni na Siha zingekuwa mbali kimaendeleo.
 
Back
Top Bottom