Je, wajua? Wasio Waislamu hawaruhusiwi kukanyaga Makka?

Je, wajua? Wasio Waislamu hawaruhusiwi kukanyaga Makka?

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,563
Reaction score
7,321
Katika Nchi ya Saudi Arabia, Eneo la Makka inachukuliwa kuwa mji mtakatifu zaidi katika Uislamu. Ndiko kunakopatikana Msikiti wa Masjid al-Haram, ambako ipo Kaaba (Lile jiwe linalozungushiwa kitambaa cheusi ambalo waumini ulizunguka). Hapo ndio kitovu cha kiroho cha Uislamu, na Waislamu duniani kote huelekeza vichwa vyao huko wakati wa sala zao za kila siku duniani kote.

Kwa sababu ya umuhimu wake wa kidini, sheria ya Kiislamu ambayo Saudi Arabia inatekeleza, Saudia0 imeweka zuio la kuingia Makka kwa Waislamu pekee.

Iwapo asiye Muislamu akijaribu kusafiri kuelekea Makka kwa barabara, kuna vituo vya ukaguzi vinavyomuelekeza aelekee nje ya mji huo. Hata mabango ya barabarani yanaonyesha wazi njia za “Waislamu pekee.”

Sasa hapa kuna tofauti muhimu:

Wasio Waislamu wanaweza kutembelea Medina ambapo ndio Makka ilipo, lakini hawawezi kuingia katika eneo la Msikiti wa Mtume (hasa sehemu takatifu maalum). Hata hivyo, mji wa Madina kwa ujumla haujazuiwa kikamilifu kama ilivyo Makka.

Kwa ufupi:

Makka → Waislamu pekee ndio uruhusiwa kuingia
Madina → Wasio Waislamu wanaruhusiwa kuingia mjini, lakini si katika baadhi ya maeneo matakatifu ikiwemo Makka

Utakuwa unajiuliza wanatambuaje nani ni muislamu na nani si muislamu.

Jibu ni kuwa katika nchi ya Saudi Arabia, kuingia Mecca si suala la kusema tu kwa mdomo kuwa mimi ni muislamu au kuvaa kobazi na kibagarashia kama wapemba. La hasha ni suala la nyaraka na vibali rasmi.

Mfano: Mfumo wa Visa
Ikiwa ukitoka nje ya nchi, unahitaji visa maalum:

Visa ya Hajj: kwa ajili ya kwenda kuhiji kabla ya Idd kubwa.

Visa ya Umrah: Watu wengi hupendelea kufanya Umrah wakati wa mwezi wa Ramadhani kwa sababu ya fadhila kubwa ya kiibada. Pia hufanyika miezi mingine yote kulingana na ratiba na kibali cha visa.

Au kibali cha ukaazi (Iqama) kama Muislamu. Iqama = Kitambulisho cha ukaazi, kinachoonyesha hali yako ya kisheria, dini, na haki za kukaa nchini Saudi Arabia. Ukiwa na kibali hiki cha makazi kitaeleza wewe dini yako ni hipi.

Wakati wa kuomba visa, taarifa zako hujazwa rasmi, na mara nyingi dini huonekana kwenye kumbukumbu za pasipoti au mfumo wa maombi. Mamlaka huangalia hilo kabla ya kukuruhusu.

Ikiwa umeandikishwa kama si Muislamu, hutapewa ruhusa ya kuingia Makka, na utazuiliwa kuingia Makka.

Vizuizi Barabarani: Barabara zote za kwenda Makka zimejaa vizuizi au check points.

Ukiendesha gari kuelekea Makka, kuna vituo vya ukaguzi kabla hujafika mjini. Polisi huangalia:

1. Kitambulisho chako

2. Iqama (Vibali maalumu kwa wakaazi)

3. Aina ya visa

Kama huna kibali sahihi cha kukuruhusu kuingia makka, unaelekezwa kwenda kwenye barabara ya mchepuko. Hata mabango ya barabarani yanaonyesha wazi:

“Muslims only → Mecca”

“Non-Muslims → Bypass”

Katika kipindi cha Hajj, ulinzi huwa mkali sana. Kuna mifumo ya kidigitali, vibali maalum, hata utambuzi wa alama za vidole. Si rahisi kupenya bila ruhusa.

Vipi Kama Mtu Aseme Uongo?

Kitaalamu, mtu anaweza kudai ni Muislamu — lakini: Nyaraka lazima zilingane

Wakati wa ibada, itadhihirika haraka kama huna uelewa wowote wa taratibu. Wenzako wakiswali wewe utaduwaa, au wakitamka maneno wewe utakuwa kimya na itakuwa rahisi kugundulika. Walinzi wapo kila mahali

Kisheria, unaweza kufukuzwa nchini au kuadhibiwa

Kwa hiyo si suala la “wanahisi” au “wanabahatisha.” Ni mfumo wa kisheria, nyaraka, na udhibiti rasmi.

View: https://www.instagram.com/reel/DRMKk_FCDUx/?igsh=cjB5ZTRtNXU4NXdr
 
Vatcan unaenda tu maana unaweza kwenda kama mtalii,kuhiji,kufanya tafiti au kupata huduma za kiroho kikubwa nyaraka tu
 
Kama rahisi na nyinyi tengenezeni mji wenu hlf mueke sheria kama hizi
 
Naweza kwenda Vatican na kobaz zangu?
Unaweza vizuri tu.

Ila nyie Waislam ni wabaguzi sana. Makkah ulikuwa mji wa wapagani na ndiyo waliwakaribisha hapo mkawa mnaabudu pamoja hiyo jiwe. Matokeo yake mmegeuza kibao hamtaki wapagan au wasio Waislam kuingia Makkah.,ilhali ulikuwa mji wa Wapagan.
 
Naweza kwenda Vatican na kobaz zangu?
Ndiyo, Muislamu anaweza kutembelea Vatican. Hakuna vizuizi vya kidini vinavyomzuia Muislamu kuingia Vatican City au kutembelea maeneo kama St. Peter's Basilica au Makumbusho ya Vatican.

Hapa kuna mambo muhimu:

1. Visa na Kuingia – Kuingia Vatican City kawaida hufanyika kupitia Italia, kwa hivyo sheria za visa za Italia/Schengen zinatumika ikiwa ni lazima. Mara mtu yupo Roma, anaweza kuingia kwa uhuru kwenye eneo la Vatican.

2. Heshima kwa Sheria na Desturi – Wageni wa dini zote wanatarajiwa kuvaa kwa unyenyekevu, kuonyesha heshima, na kufuata miongozo ndani ya makanisa ya mji huo, basilika, na makumbusho.

3. Vituo vya Sala – Vatican haina misikiti, kwa hivyo Waislamu wanaotembelea kwa sababu za kiroho wanahitaji kupanga mahali pa kufanya sala mjini Roma.

4. Utalii na Kujifunza – Waislamu wengi hutembelea Vatican kwa sababu za kihistoria, kitamaduni, na usanifu. Vatican inafungua milango yake kwa wageni wa dini zote bila ubaguzi.

Kwa ufupi: Waislamu wanaweza kutembelea kwa uhuru, mradi wanaheshimu sheria na desturi za eneo.
 
KWahyo hakuna Kafiri hata moja alofika Makkah?
 
Ubinafsi tu wa waislamu. Sioni hata mantiki kwenye hilo.
 
Wengine hatutajutia kutokujanyaga Saudi Arabia au Mecca....
 
Back
Top Bottom