Je Wajua Nchi Inayoongoza Duniani kwa Rushwa 2010?

Ameir Eshaq

Member
Jan 3, 2011
35
1
Je Wajua Nchi Inayoongoza Duniani kwa Rushwa 2010?

Nchi inayoongoza duniani kwa kula rushwa 2010 ni nchi ya Somalia, Africa ikifuatiwa kwa karibu na nchi za Myanmar, Afganistan na Iraq. Nchi zinazoongoza kwa kutokula rushwa ni Denmark, New Zealand na Singapore. Nchi sita za Africa kati ya nchi kumi zilizoorodheshwa kwa kula rushwa zaidi duniani 2010 ni nchi za Somalia,

  1. Sudan,
  2. Chad,
  3. Burundi,
  4. Angola na
  5. Equatorial Guinea.
Nchi ya Rwanda inaongoza Africa mashariki kwa kutokula rushwa, Tanzania ya pili ikifuatiwa na Uganda. Burundi ina rekodi mbovu ya rushwa afrika mashariki na Kenya japo iko nyuma ya Rwanda, Tanzania na Uganda, lakini ripoti inasema kwamba inafanya vizuri ktk kupambana na rushwa.

View attachment 20506
 
Mhhhh!!!! Tanzania kwa rushwa iko chini je Rushwa iliyokomaa inayoitwa UFISADI JE? TAKWIMU ZIPO? au ni terminology mpya! Mpka Downs itumalize ndo wajue nchi hii ni kiboko kwa ufisadi!! Rushwa inashughulikiwa UFISADI JE? 0
 
tupe source ya hizo data?mana nimebiisha.....................rushwa kubwa ka ya rada na bado hatujashika ukwanza kidunia?ah aha aah haiwezekani.
 
Siamini. Nimeishi Sudan, Kenya, Chad na Angola. Katika nchi hizo huenda Angola iko mbele ya TZ. Chad kulikuwa na rushwa lakini sasa rais wao ameweka ngumu ile mbaya. hivi nisemavyo mawaziri watatu wako ndani na mali zao kutaifishwa! Sudan....wala usifananishe na TZ. Sudan ilianza kujijenga mwaka 2005 baada ya kutia mkataba wa amani. Hivi sasa Khartoum ina taa za barabarani masaa 12 usiku, imejenga barabara pana zenye lane sita, ukirudi baada ya mwezi tu utaona mabadiliko makubwa. hawa Wazungu wana siasa zao. Huoni hata mauaji ya Arusha hayakutangazwa popote? Lau ingekuwa Sudan, Kenya etc ungesikia dunia nzima! hii ndio maana kwa nini dhahabu yetu inachukuliwa bure na makampuni ya kimataifa!!!!!!!!!!!! Amkeni. Nani anayezungumzia haki za binadamu saudia? Unajua kwa nini? Kwa sababu wazungu wapata mafuta ya chee. lakini Iran? kila siku unasikia 'haki za binadamu'
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom