Je, wajua kuwa Mlima mrefu kuliko yote Duniani sio Everest?

Tomahawk

JF-Expert Member
Apr 12, 2015
234
218
Mara nyingi tumefundishwa kuwa mlima mrefu kuliko yote Duniani ni mlima Everest unaopatikana uko bara la asia. Lakini wataalamu hawasemi mlima uo ni mrefu kuliko yote Duniani kama unapima milima kutokea kwenye usawa wa bahari. Ukweli ni

kwamba kuna aina mbili za upimaji milima, njia ya kwanza ni kupima mlima toka usawa wa bahari na njia ya pili ni kupima mlima kutoka kwenye kitovu cha Dunia(earth center).

Hivyo ukipima mlima toka usawa wa bahari mlima mrefu kuliko yote unakuwa mlima Everest ila ukipima mlima kutokea katikati mwa Dunia mlima Chimborazo uliopo nchini Ecuador ndio unakuwa mlima mrefu kuliko yote Duniani.

Hivyo ingekuwa vyema kama wangesema mlima mrefu kwa aina za upimaji. Mlima kilimanjaro umepimwa tokea usawa wa bahari.

Jisomee => Ken Jennings Shocker: Mt. Everest Is Not the Highest Point on Earth
 
Mkuu urefu hupimwa pakiwa na reference point. Na njavojua lazima vipimo vyote vianziea kwenye level moja( sea level). Hivi unawezaje kupima urefu wa mtu ikiwa kasimama kwenye kigoda. Huo utakuwa ni urefu wa mtu plus urefu wa kigoda. Kwa kifupi everest ndo mlima mrefu hiyo haina ubishi. Na chimborazo ni kwa mujibu wako wewe na sio kwa mujibu wa sayansi
 
Kwa style hiyo ya kupima kutoka kwenye core ya dunia basi Joti ni mrefu kuliko mlima kilimanjaro!
 
Kwa kipimo ulichosema hata mlma usambara ungewekwa hapo katkat mwa dunia ungekuwa mrefu kulko yote dunian
 
Ahsant kwa somo nmepata changamoto hapo nlkuwa najua n mlima everest tu sikujua hko kgezo cha Pl let me learn more
 
Mkuu urefu hupimwa pakiwa na reference point. Na njavojua lazima vipimo vyote vianziea kwenye level moja( sea level). Hivi unawezaje kupima urefu wa mtu ikiwa kasimama kwenye kigoda. Huo utakuwa ni urefu wa mtu plus urefu wa kigoda. Kwa kifupi everest ndo mlima mrefu hiyo haina ubishi. Na chimborazo ni kwa mujibu wako wewe na sio kwa mujibu wa sayansi
Kuna tatizo hapa la kutaka kutoutambua mlima Kilimanjaro kuwa ni mrefu kuliko yote
 
Haya masomo ya miandiko ni shida sana ingekua theory za physics tungesema em kokotoa kidogo sasa hapa inakuja hadithi tena za katikati ya dunia...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom