je wajua kama Osama yu hai!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

je wajua kama Osama yu hai!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ginner, May 8, 2011.

 1. G

  Ginner JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 1,139
  Likes Received: 263
  Trophy Points: 180
  Taarifa zinazozidi kutamba katika vyombo vya habari mbali mbali nchini na vya kimataifa kuhusu kifo cha osama bin laden kilichokea usiku wa kuamkia jumatatu ya tar 2 katika jiji tulivu la Abbotabad nchi Pakistan katika operation maalum ya makomandoo wa kimarekani ....kutokana na tafakari za watu mbali mbali,wanaharakati wa chama cha upinzani cha marekani republican..wanazuoni wamaswala ya kisiasa.kijamii na kiitelegensia..inaonesha kuna uwezekano mkubwa kwamba Gaidi namba moja duniani Osama Bin Laden huenda akawa Hai chini ya ulizi mkali ya vikosi vya usalama vya marekani...

  Sababu zifatazo ndipo zilizopelekea hitimisho la kuwapo hai kwa osama....kwanza ni kutoka kwa mashahidi waliokuwapo katika kasri ile siku ya tukio...mtoto wa osama alikaririwa akisema baba ake (alikamatwa akiwa hai) na baada ya apo wakampiga risasi na kufa...kunauwezekano makomandoo hao wakawa wamefaki kitendo cha kumpiga risasi ili mtoto huyo adanganyike na kushuhudia kifo cha baba ake kwa waandishi

  Pili...kitendo cha kumzika kwa haraka tena baharini ni jambo linalotiliwa sana shaka..kitendo hiki kimefanyika ili kuwafunga mdomo wanaharakati watakaotaka kuuona mwili wa Osama ukiwa kaburini...pamoja na wao wamerekani wakidai wamemzika baharini ili kaburi lake lisitumike kama eneo la kuabudia kwa wafuasi wake

  Tatu...kitendo cha ikulu ya marekani kusita kutoa picha za tukiolilo husika katika kumkamata kwa osama,,,,picha izi zimekuwa gumzo na siri kubwa katika serikali ya marekan...kuna uwezekano mkubwa kwamba picha izo zikawa zinaonesha kuwa osama amekamatwa hai na hakuuwawa kaka ripoti za ikulu zilivo tamka apo awali..ivyo kitendo cha kuzitoa picha izo zingepingana kwa kiasi kikubwa na taarifa za awali za serikali ya martekani.

  Na jambo la mwisho......kukamatwa kwa osama akiwa hai kulikuwa na advantage kubwa kuliko kikutwa akiwa amekufa kwani wangemtumia kupata taarifa nyingi za mashambulio ambayo yangeweza kutokea katika mipango ya al qaeda....

  Hivyo basi kunauwezekano mkubwa sana osama akawa hai ila katika ulinzi mkail ya vikosi wa kimarekani akihojiwa ili kupata taarifa mbali mbali juu ya matukio ya kigaidi yaliyopangwa kutokea...

  Je ni kwann wamerekani wanataka kuujulisha ulimwengu kuwa Osama kafariki........
  Jawabu ni hili....endapo ingetambulika kuwa osama amekamatwa mateka na wamerekani....bac wafuasi wake ambao ni zaidi ya maelfu duniani kote wangeweza kuwateka watu mashuuri wamarekani na kuahidi kuwazika wakiwa hai au wamwachie Osama....hivyo izo ndo sababu zinazofanya waamerika wazuge kama adui yao amekufa ili watu waipotezee na habari yake iishie hapo...nini maoni yako....!!!!!!
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  Bila shaka unamuongelea Osama yule muendesha pikipiki ya miguu matatu pale soko la ndizi Mabibo
   
 3. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  Naota naota nadanganywa na watemi wasio na mpango
   
 4. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,638
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Akiwa hai inakusaidia nini wewe Mtanzania wa Tandale? Yaani wewe umejiunga humu JF leo hii na post ya kwanza tu unakimbilia kuweka ufu na uhai wa Osama, hata hujaonyeshwa choo cha humu JF kipo wapi! Bisha hodi kwanza, subiri ukaribishwe, tumia masaa kadhaa kulijua jukwaa na tools zake, tumia walau siku tatu kusoma watu uliojiunga nao wakoje kiuelewa. Sio unatoka kuazima gazeti la "risasi mchanganyiko", unaona habari na kukimbilia kujiunga JF. Jukwaa hili ni la wasomi, wapuuzi wachache hawawezi kukosekana, utawajua tu ukitulia. baada ya hapo ndipo ujue kama hili jukwaa ni la kiwango chako au maji marefu. Kama vipi nenda kaweke hizo news FB na GPL.
   
 5. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  acha uongo wewe, kama hajafa sasa si tufanyeje?
   
 6. N

  Nancy70 Member

  #6
  May 8, 2011
  Joined: Dec 7, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bora umeliona hilo Jabulani.
   
 7. G

  Ginner JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 1,139
  Likes Received: 263
  Trophy Points: 180
  Ndugu jabulani usiishi kwa mazoea......sio mgeni jf nipo tangu enzi za ujana wako....nimebadili tu account kwa sababu za kiusalama.
   
 8. G

  Ginner JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 1,139
  Likes Received: 263
  Trophy Points: 180
  Mkuu wa chuo ni cheo kikubwa zaidi ya akili uliyonayo.....sikutegemea uwe unafikiria puani...ukiwa kama msomi lazma ujua matukio ya kidunia yanavyo endelea...usikae tu ukabweteka usijue dunia inavo kwenda..wasomi hatupo ivo
   
 9. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #9
  May 8, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,212
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Yani umeniboa sana! ila nashukuru umejibiwa vizuri we mgeni!

  Unajua kila kukicha jf inazidi kupata umaarufu, huyu binadamu atakuwa kaambiwa kuna mtaandao sumu kwa waovu yani hauangalii sura wala jina la mtu! unachana watu liveeeee!!!!! akakurupuka nakujisagili leo.
   
 10. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,638
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Ulikuwa unatumia ID gani ili mods waifute ya mwanzoni kuokoa memory space kwenye server? Sasa kama wewe ni mkongwe humu, sikutegemea uanzishe thread zinazofanana na ambazo zilishaanzishwa wiki yote iliyopita. Watu wanakaa kubishana uhai na uzima wa Osama wakati mtu alishaswaliwa na pilau ilishaliwa huko Pakistani. Al-Qaeda na Taleban wamekiri kuuawa. Mtoto wa marehemu amekiri kumuona baba yake akipigwa risasi kichwani na kifuani; bado kuna watu wanasema ni risasi feki. Sawa, zinaweza kuwa feki; sasa sisi humu tutajadili haya hadi lini? Kwa nini tusichangie hot news nyingine zinazojiri ndani na nje? Tubadili upepo jamani, ya Osama si hot tena. Heri ungeweka ya huyo mrithi wake aliyekoswakoswa kulipuliwa juzi!
   
 11. Nico1

  Nico1 JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  mi nadhani kifo kipo kwa ajili ya mwanadamu haina haja ya kuendelea kubishana amekufa au laa kama watu mashuhuri duniani tayari wameionja
  mauti kv BENITO MUSOLIN,ALDOLF HILTILA,nk vipi leo huyu jamaa kwani yeye kaandikiwa kuishi milele?
  amekufa !amekufa tu kama hautaki kuamini subili utamuona akiwa hai.
   
 12. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  sio kwamba wewe ndio unafikiria puani? Kwa sababu kichwa cha thread yako kinaonyesha ni confirmed osama yupo hai, lakini ukisoma habari yako ni suspicious news kwamba osama yupo hai, kitu kingine hadi kundi lake la kigaidi limethibitisha kifo chake ndio maana nakwambia uache uongo.
   
 13. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #13
  May 8, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  I ain't got no time to waste here. Gone.
   
 14. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #14
  May 8, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  nadhani ndiye haswa amzungumziae huyu jamaa. lkn kama ni OBL jamaa keshaliwa na samaki. labda cha kuuliza ni kama hao samaki waliomla bado wako hai au nao washauawa! OBL ni historia. na kwa alivyotufanya Bongo sioni kwa nini mtu yeyote amlilie
   
 15. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #15
  May 8, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Hiyo sababu ya pili ndio inaumiza zaidi kichwa na haiingii akilini..
   
 16. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #16
  May 8, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Achana na Osama jali ya Bilali :israel::israel:
   
 17. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #17
  May 8, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Ahahahaah!!
   
 18. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #18
  May 8, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hapa mi naona kila mtu aamini jinsi anavyoona yeye..
   
 19. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #19
  May 8, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  - "A silent fool is counted wise"
  niipenda signature yako..:happy:
   
 20. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #20
  May 8, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Karibu mgeni..

   
Loading...