Peter Mwaihola
JF-Expert Member
- Jun 23, 2022
- 289
- 489
Huu ndio ule mwaka wa kufanikiwa ambao watu watasimulia kuhusu wewe.
Huu ndio ule mwaka ambao watu watakaa chemba wakiulizana "hata yule jamaa, mfupi, mwembamba amekuwa tajiri?".
Huu ndio ule mwaka mama yako atakuomba elfu kumi nawe utamtumia Laki 1 hapo hapo.
Huu ndio ule mwaka ambao utamuita mke, yule dada uliye muambia utamuoa miaka 10 iliyopita pasipo mafanikio.
Huu ndio ule mwaka ambao utajenga nyumba yako na utaacha kugongewa mlango na kudawa Kodi ya nyumba na hela ya umeme.
Huu Ndio ule mwaka utaenda hospitalini bila hofu ya kutoa hela ya kumwona Daktari.
Huu ndio ule mwaka utaacha kupita madukani Kuomba chenji "Chelechele" kwa ajili ya kutoa sadaka kanisani.
Huu ndio ule mwaka utaitwa mtu wa watu na Majina mengi Kama kiongozi, mkuu, boss...
Huu ndio ule mwaka utakao achana na kelele za konda wa Daladala na kuwa na jeuri ya kufungua buti ya gari lako na kugongesha milango, Mba! Mba!.
Huu ndio ule mwaka ambao masikio yako yatasikia sauti za faraja "Nakupenda sana mume wangu, mke wangu, baba yangu".
Huu ndio ule mwaka ambao watoto wako wataacha kusimamisha pua chakula kitamu kikinukia kwa jirani.
Anza kwa juhudi amini kuwa huu ndio mwaka wako wa kufanikiwa, Mungu anaenda kujibu maombi, Neema zinaenda kumiminika kwenye njia zako
Heri ya Mwaka Mpya