eden kimario
JF-Expert Member
- Jun 13, 2015
- 10,356
- 16,400
Jiji kuu ni pyongyang
Serikali - kiongozi mkuu
Ufalme - gojoseon
Nchi hii ilijitangazia uhuru ikiwa bado chini ya utawala wa Japani 1/4/1919
Ukombozi kutoka utawala wa Japani ilikuwa ni 15/8/1945
Jamhuri kamili ilikuwa ni kati ya 15/8/1948 na 9/9/1948
Kwa mujibu wa sensa ya 2013 korea ya kaskazini ina watu milioni 24 na laki 8
Imepakana na korea kusini, china, na urusi
Fedha wanayotumia ni won ya korea kaskazini
Korea ya kaskazini ni matokeo ya ugawaji wa korea baada ya vita kuu ya pili ya dunia
Korea ilikuwa koloni la Japani tangu mwaka 1910 hadi 1945
Kwenye mwaka wa mwisho wa vita kuu ya pili ya dunia
Jeshi la Urusi liliwafuata Wajapani kaskazini mwa ras ya korea huku Wamarekani wakiingilia kusini mwa ras ya korea
Mazungumzo ya kuiunganisha tena korea baada ya uvamizi wa Wajapani yalikufa baada ya vita baridi kuibuka kati ya kaskazini iliyokuwa imekombolewa na Urusi na ile ya kusini iliyokuwa imekombolewa na marekani
Mwisho wa siku kila mmoja alianzisha serikali yake kulingana na itikadi itikadi za waliowasaidia kuikomboa mikononi mwa wajapani ambao ni Urusi na Marekani
Warusi walitaifisha tasnia na ardhi wakaacha serikali ya kikomunisti kazkazini
Huku Marekani ikiacha uchumi wa kibepari katika serikali ya kusini
Katika vita ya korea iliyofuatia korea ya kaskazini ilidumu kwa sababu ya msaada wa kijeshi kutoka china
Mpaka leo serikali ya korea kaskazini inamiliki viwanda karibu vyote nchini humo huku asilimia kubwa ya pato la taifa ikipelekwa katika jeshi ambalo ni jeshi kubwa duniani
Nchi hiyo inakamata nafasi ya 9 katika nchi zilizo na teknolojia kubwa ya kijeshi duniani
Lakini hali ya wananchi wa vijijini ni mbaya kutokana na upungufu wa chakula
Korea kaskazini hutoa misaada ya vyakula na makazi kwa raia wake kwa bei nafuu kwa msaada wa serikali huku elimu na huduma za afya zikitolewa bure
Raia wa korea kaskazini haruhusiwi kutoka nje ya nchi hiyo bila kibali maalum cha serikali au kuingia nchini humo bila kibali maalum
Kodi ya mapato ilifutwa rasmi nchini humo mwaka 1974
Jeshi la korea kaskazini lina jumla ya askari milioni 1 laki 1 na elfu sita
Kwa hiyo ni moja kati ya nchi tano duniani zilizo na jeshi la kudumu lenye askari zaidi ya milioni huku wao wakiongoza
Nchi hiyo ililipua bomu la kwanza la nyuklia mwaka 2006 na inasemekana mpaka sasa wamepiga hatua kubwa kijeshi duniani kwa sababu pato la taifa karibu asilimia 80 huelekezwa jeshini
Unaweza kuongezea na wewe jinsi uijuavyo korea kaskazini