Je, vyombo vya habari vya kimagharibi vimesusia kombe la dunia Urusi??

Nature

JF-Expert Member
Nov 5, 2014
758
2,027
Inaonakana kama Vile .....

Maandalizi yamekamilika kwa Asilimia 95% kilichobaki ni Muda kufika na Michuano kuanza lakini inaonekana kama Vyombo vya habari viko kimya Sana Hasa zikiwa Zimesalia Siku 100 Kombe la dunia Kuanza...

Miaka ya Nyuma ilikuwa ikifikia Hatua kama Hii unakuta Vyombo vikubwa vya habari za Kimichezo kama Vile SKY, FOX, BBC, MSNBC, na ITV ni Matangazo kila saa na Promotion mbalimbali Mfano Kule South Africa, Na Mwaka 2014 kule Brazil....

Ila Awamu Hii inaonekana kama Kuna Ubaguzi vile yaani Pamoja na kuwa ni Mwaka wa World Cup lakini hata Michuano ya EUROPA LEAGUE inatangazwa kuliko World Cup ...

Au wanaona kwamba kuipa Promo World Cup awamu hii ni Kama kuitangaza sana Urusi kwa Dunia???

Sababu Ni Nini?

Mbona Kama Siasa Inaingizwa Michezoni??

World Cup Iko kwa Maslahi ya nani?
1b53ca62dd816a9b2a9b0f29892da5b6.jpg
 
Tulia ww bado mapema sana watu bado akili zao zipo kwny michuano ya ligi na uefa ngoja ifike May ndo utaona msisimko wa ilo kombe
 
Nadhani kwa vyombo vya Marekani shida ni kuwa timu yao haipo world cup mwaka huu. Suala la kuwa linafanyikia Urusi nadhani linakuja second to that.

Tatu, ambayo inapewa uzito na namba moja hapo juu, wamarekani na mpira wa miguu sio sana. So kama timu yao haipo basi hata mzuka wa wananchi ni mdogo. Na media zinaangalia watu wanataka nini
 
Ila kwel kombe la dunia la mwaka huu limepoa...nakumbuka la 2006,2010 na 2014 kulikuw na clips mbali mbali zinachezwa kweny matelevishen ili tu kulitangaza, lkn saiv wako kimya sana
 
Nachoona ni kwamba Russia wenyewe hawaipi uzito kombe la dunia,nakutana na wengi wao hawana hata mzuka,hawa majamaa wapo mbali na mpira
 
Sasa unataka Russia asaidiwe kutangazwa?
Ye si anajigamba Ana nguvu za kipiga kijiji chochte katika Dunia hii?
Sasa a nashindwa nn kujitangaza?
 
Back
Top Bottom