Je vikosi vya KMKM ndo wale waliokua hawajui Kiswahili

Je vikosi vya KMKM ndo wale waliokua hawajui Kiswahili

Life2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,377
Reaction score
4,847
Endeleeni kupumzika kwa amani mashujaa/mashahidi wote mliomwaga damu yenu kwa ajili ya Ukombozi wa Watanganyika hakika Watanganyika wataandika ujasiri wenu mioyoni mwao.

Ni juzi tu tumemsikia mtekelezaji wa shughuli zote za serikali za kila siku Mwigulu Nchemba akikiri kwamba ni kweli ndugu zetu, watanganyika wenzetu waliuliwa makumi kwa maelfu na watu wasiojua kiswahili sijui walikua wanaongea lugha gani.

Je niulize Zanzibar kuna watu hawajui Kiswahili, kwanini lawama nyingi zinaenda kwa vikosi katili chinjachinja vya Kmkm, je kwanini Kmkm?

Je wahusika waliona vikosi vya kitanganyika vitashindwa kuua ndugu zao watanganyika na kuamua kuleta watu ambao hatuna undugu nao zaidi ya kuunganishwa na mchanga?

Je kwanini hawa jamaa walivaa roho za kikatili mnoo na kuua ndugu/watanganyika wenzetu wasiokua hata na manati?

Je wale wanaowatetea watawala makatili na vikosi vya mauaji wamelipwa kuendesha propaganda humu mitandaoni na je kama wamelipwa ni kiasi gani kinachozidi damu ya mtanganyika mwenzake?

Je vikosi vya ulinzi vya watanganyika vilikua wapi mpaka wageni/mamluki wa Kmkm wanapenya na kuanza kumaliza watanganyika wenzetu?

Je ni adhabu gani wanayostahili hawa chinjachinja wa watanganyika wenzetu.

Je kila mtu abaki na upande wake au bado watanganyika watachinjana?

Je na rais vinapotoka vikosi vya kmkm kwanini asiwe naye ni mtuhumiwa mkubwa baada ya majeshi yake katili kuja kwa watanganyika na kuanzisha chinjachinja?

Hakika wasiojua kiswahili wametumalizia ndugu zetu, wameua nguvu kazi ya taifa letu na wasomi tena vijana.

Mwenyezi Mungu wote waliohusika watawanyike kama moto wa miibani, watanyike kwa njia saba.

Wote tuseme Amen
 
Hili li mama sijuwi linatushinda nini WALAHI?!
TANGANYIKA INAKUFA MACHONI KWETU HUKU TUKIWA HELPLESS!
 
Hayo maswali ukimuuliza mwigulu anapata 0% hajibu hata swali 1 hapo katika maswali yote hayo yote anakula 0.. feki PM.. hata ukimuuliza yule comedian anaejifanya msemaji kumbe anafanya show za vichekesho ikulu G Msigwa nae anazungusha yai hajibu hata swali 1 hapo..
 
Back
Top Bottom