Je utakubali???

Kutokana na mazungumzo yako...Sijasema umesema kuna sehemu umeandika, nilipo highlighted kule ulikuwa umesema elimu ni mhumu sana, afu pale pale maneno yako yanasema vingine....Sa kama elimu ni muhimu kama unavyo sema, yanini tunabishana hapa...Au unataka tujaze maneno mengi tu :A S shade:
Mkuu elimu inasaidia kwenye maisha, (hata ambae hana elimu kama amefika level fulani, ina maana huenda angepata elimu angefika level ya juu zaidi).

Lakini kutokuwa na Elimu sio kwamba mtu atashindwa maisha ya ndoa (kumbuka kwenye ndoa hatutafuti mtu wa kuandika thesis, au lecturer wa kufundisha jambo fulani) ni kutafuta mwenza wa kushare maisha (ambapo hapa zinazotakiwa ni basics ambazo mtu yoyote mwenye malezi bora na busara anajua jinsi ya kuishi na mwenza)

Katika maisha ya watu wawili kutokuwa na elimu hakumaanishi kwamba maisha ya wawili yatakuwa sio bora
 
Mapenzi na elimu havina uhusiano lakini wakati mwingine inabidi vitazamwe kwa undani...
Mmoja wenu akiwa na elimu ndogo sana kuliko mwenzie lazima kutakua na gap kubwa sana kwenye mitazamo ya maisha cause mmoja atakua ana upeo wa darasa la 7 mwingine ana upeo wa masters,vipaumbele vya maisha vitatofautiana kulingana na elimu na hapa ndo matatizo yataanza..
Kwa mtazamo wangu ni bora mwanamke ambaye hajasoma kuolewa na mwanaume aliyesoma than vice versa..
Wanaweza kuoana kama mwanaume amejijenga kimaisha lakini ndoa itakua na migogoro sana..

akili unayotumia kwenye kitabu ni tofauti na ile unayopambana nayo kwenye maisha!Na usifikiri kuwa na elimu ya juu basi ndo utaweza kupambana na maisha vizuri kuliko asio nayo ama ipo ndogo.
 
Mkuu elimu inasaidia kwenye maisha, (hata ambae hana elimu kama amefika level fulani, ina maana huenda angepata elimu angefika level ya juu zaidi).

Lakini kutokuwa na Elimu sio kwamba mtu atashindwa maisha ya ndoa (kumbuka kwenye ndoa hatutafuti mtu wa kuandika thesis, au lecturer wa kufundisha jambo fulani) ni kutafuta mwenza wa kushare maisha (ambapo hapa zinazotakiwa ni basics ambazo mtu yoyote mwenye malezi bora na busara anajua jinsi ya kuishi na mwenza)

Katika maisha ya watu wawili kutokuwa na elimu hakumaanishi kwamba maisha ya wawili yatakuwa sio bora
Hapa naona hutuelewani...we unachukulia elimu ndo maisha wakati sisi tuanchukulia elimu ni kuondoa ujinga.

Maisha na elimu ni vitu tofouti kabisa hata wanyama wana enjoy katika maisha yao na wakati hawana akili.

Kuishi maisha mazuri na mabaya ni mipango ya mungu, na elimu kama ingekuwa haina faida mungu asinge shusha vitabu vya dini ili watu wavisome...Mtu ambaye hajasoma vitabu vya dini ni vigumu sana kutenda mazuri.

Na mtu asiye soma ni vigumu sana asiwe mjinga, lazima ana kasoro tu...Therefore, ni bora kumuepusha binti yangu na watu wanamna hio :bounce:
 
Hapa naona hutuelewani...we unachukulia elimu ndo maisha wakati sisi tuanchukulia elimu ni kuondoa ujinga.
Wewe sasa naona umeanza kunichanganyia habari (sijui ni kwa makusudi au labda huelewi..) hivi ni wapi nimesema elimu ndio maisha, na nani alikwambia kupata elimu ndio umeondoa ujinga (na hapa usichanganye knowledge na education), ndio maana nikasema (kwenye context ya mume na mke kuishi vizuri) ni syllabus gani, level gani au college gani ambayo inafundisha busara, heshima na kuishi vema na mpenzi wako, au watu ambao hawajaenda shule, au hawajui kusoma na kuandika hivi hawana knowledge (uelewa) wa kuweza kuishi pamoja na mwenza wao ?

Maisha na elimu ni vitu tofouti kabisa hata wanyama wana enjoy katika maisha yao na wakati hawana akili.
Nani kasema elimu na maisha vipo sawa, sasa na hapo tunakuja kwenye akili naona tumetoka kwenye elimu sasa.., swali bado lipo pale pale knowledge ya kuweza kuishi na mpenzi wako inapatikana vipi, kwa alikwenda shule au kwenye vitabu kwahio wasiojua kusoma hawana hii knowledge ?

Kuishi maisha mazuri na mabaya ni mipango ya mungu, na elimu kama ingekuwa haina faida mungu asinge shusha vitabu vya dini ili watu wavisome...Mtu ambaye hajasoma vitabu vya dini ni vugumu sana kutenda mazuri.
Sasa hapa naona umeanza kuhamisha goal posts na kuleta issue nyingine tofauti kabisa.., hata kama nikisema ninaamini na unachosema (hivi kujua / kufahamu dini ni mpaka ujue kusoma vitabu vya dini, hivi mafundisho ambayo watu wanapata kutoka kwenye imani zao hayawezi yakapatikana through medium ya maongezi ?, Alafu kwenye dini na kutenda mazuri (hivi wapagani wote ni watenda mabaya ?)

Na mtu asiye soma ni vugumu sana asiwe mjinga, lazima ana kasoro tu...Therefore, ni bora kumuepusha binti yangu na watu wanamna hio
Kasoro wote tunazo (zipo tofauti tofauti) na kila mtu ni mjinga kwenye nyanja tofauti mimi naweza nikawa mjinga kwenye mambo ya uchumi wewe unaweza ukawa mjinga kwenye issue za biashara yule anaweza akawa mjinga kwenye mambo ya IT.., ila uelewa wa kuishi vizuri na watu na kuendesha familia kwa upendo na mapenzi (haupatikani kwenye vitabu)
 
Back
Top Bottom