Je utakubali kuwa na mimi siku tukikutana?

usogawa hovyo mbegu zako,
mkulima hodari utunzaye jembe lako.

Hahahahaaaaaaa! Hapo tu ndo UMENIKOSHA!!!! LOL! Jembe shurti kutuzwa, sio KILA KICHAKA LINALIMA, VINGINE VITALIFANYA LIWE BUTU BURE!!!! LOL! CHEZEA MISITU YA UOTO WA ASILI WA CONGO EQUATORIAL REGION!!!!!! JEMBE LINAZAMA HADI MPINI NAO NDANI!!! LOLEST![/QUOTE]

umeona enh! si kila mahali wewe unachimba tu mwisho jembe linapata kutu na kukatika mpini bureeee........... tena hizo mbegu inabidi uziheshimu lol! so unazimwaga kama Bishanga na Asprin utegemee zitatosha. lol!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kama una taka kumpenda au kupendwa na mtu ambaye huja wai kumuona usitarajie makubwa na hayo maneno ya uta kubali au atakataa yasahau kabisa maana unaweza kuvunjika moyo au kuugua kama ata sema kinyume na unavyo tegemea!

Usitegemee makubwa!
 
wangu wa moyoni, shaka ondoa juu yangu
hufu yako mwandani, yaumiza mtima wangu,
nakupenda mwandani, kijana wa rika langu
kaa chini utulie,mie ndo wako msiri.

snowhite na Kongosho, wote wanajua mpenzi,
hata boss na Asprin jinsi nilivyodata kwako,
muulize cacico, ninavyopagawa juu yako
kaa chini utulie, mie ndo wako msiri.

najua hakika moyo wangu u radhi
asilan sikuachi, hata wanisute kama Bishanga.
najua lara 1 anajipanga, tubanane hapo hapo
nami namuhakikishia, atachuma mabichi hili kavu hapati.

kijana mzuri uliyeumbika, ufaaye ka mambo yote,
ujuaye kupanda na hata kushuka pia,
kwako wewe msiri, usogawa hovyo mbegu zako,
mkulima hodari utunzaye jembe lako.

Maneno matamu uliyosema hakika siwezi amini,
Usiku kucha sikulala nikiwaza hii bahati gani jamani,
Umenifurahisha uliponambia umedata na mimi kwa yakini,
Kweli nimefarijika kujua wengi wajua pamoja na Asprin

Amini nakwambia sasa nakuja kwa madoido na mbwembwe zote,
Nataka sasa tangazia hapa pamoja na Dunia yote,
Kwamba wewe ndiye wangu leo na maisha yangu yote,
Sitajali nikifa leo au siku nyingine yoyote

Kongosho na snowhite pamoja naye mrembo Preta,
Mwali naye Roulette wote kwa pamoja nawaita,
Mje mkiwa na tabasamu hapa si mahala pa kukunja ndita,
AshaDii dada yangu ushauri wako daima tutauchota
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom