Nzilo
Senior Member
- Nov 24, 2013
- 180
- 58
Ni muda mrefu toka kuundwa kwa UKAWA ambayo siyo chama.... nilipata wakati mgumu sana kujua kama ni chama au ni shirikisho? lakini pia nilipata wakati mgumu baada ya kugundua kuwa hakukuwa na mkataba wowote wa muungano huu bali tu ni makubaliano... Suala lingine ambalo silipatii majibu ni reaction ya wateule wa Ubunge wa CHADEMA walioteuliwa na chama hicho kupeperusha bendera ya CHADEMA huku wakiwa na malengo makubwa na shauku kubwa baada ya kujihakikishia ushindi katika uchaguzi mkuu wa October, 2015 na huku wakiwa wamepotezewa muda wao na raslimali zao kwa juhudi zao za kuhakikisha wanateuliwa na wana CHADEMA watakapoambiwa na Mh. Mbowe kuwa wawapishe wagombea wenzao kutoka UKAWA...
Kitendawili kingine ninachokiona ni pale CDM km ikifanikiwa kuingia Ikulu.... Je, Ushindi wao utakuwa wa UKAWA au wa CHADEMA? na kama ni wa UKAWA muundo wa Serikali ya UKAWA utakuwaje kama katiba ya sasa ndiyo itakayowaongoza kuunda dola?