Je, unaweza kununua eneo mwezini?

Je, unaweza kununua eneo mwezini?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
23,655
Reaction score
57,048
Baada ya mafanikio ya chombo cha India cha Chandrayaan-3 kufika mwezini, macho yote yameelekezwa mwezini sasa. Je, binadamu anaweza kuishi mwezini? Oksijeni inapatikana huko? Watu wengi wanauliza maswali hayo katika mtandao.

Kuna ripoti kwamba baadhi ya watu tayari wamenunua maeneo katika mwezi. Ni nani anayeuza maeneo kwenye mwezi? Je, ni halali kununua ardhi kama hii? Wanunuzi wanasema nini? Sheria zinasemaje?

Mfanyabiashara anayeishi Hyderabad na mnajimu, Rajeev mwenye umri wa miaka 50 ni mmoja wa wale wanaodai kuwa wamenunua eneo kwenye mwezi.

Aliambia BBC - alinunua mahali hapo mwaka wa 2002 kutoka kwa 'The Lunar Registry' yenye makao yake New York. Anasema kuwa alinunua ekari tano za ardhi karibu na eneo la 'Mare Imbrium' mwezini kwa rupia za India 7,000. 'Mare Imbrium' ni eneo liko kaskazini wa Mwezi.

The Lunar Registry ni kikundi cha kimataifa cha wanasheria. Kwenye tovuti ya kampuni hiyo inaeleza kwamba inafanya kazi ya kutafuta makaazi, kufanya utafiti na ubinafsishaji kwenye mwezi.

Rajiv aliiambia BBC jinsi alivyopata wazo la kuinunua eneo. "Miaka 20 iliyopita nilipokuwa nikifanya kazi nilikutana na tangazo kwenye mtandao. Linataja kuuza sehemu kwenye mwezi. Mwanzoni sikuamini. Lakini, baada ya kupata taarifa, nilinunua shamba la ekari tano,'' alisema.

Ameeleza kwa nini aliinunua. "Nilinunua mahali hapo kwani ni pazuri kwa wanadamu. Najua siwezi kwenda huko. Lakini, baada ya miaka 50 au 100, makao ya binadamu yanaweza kuanzishwa. Kisha maeneo yetu yatakuwa na manufaa," alisema.

Vilevile Lalit Mohta mwenye umri wa miaka 46, mtaalamu wa kompyuta kutoka Bengaluru, pia alinunua ekari mbili za ardhi mwezini. 2006 alinunua ekari hizo kutoka kwa kampuni ya The Lunar Registry kwa rupia 3000.

Anauita ni uwekezaji wa muda mrefu. Naye aliiambia BBC kwa nini alinunua mahali hapo.

"Najua siwezi kuishi mwezini sasa. Lakini, kwa majaribio kama ya chombo cha Chandrayaan-3, kuna matumaini kwamba makazi yatawezekana katika siku zijazo. Ardhi yetu inaweza kutumika wakati makazi yanaundwa huko."

Naye Rupesh Mason, mfanyabiashara mwenye umri wa miaka 49 kutoka Jammu na Kashmir, hivi karibuni alifichua kwa vyombo vya habari kwamba amenunua mahali kwenye mwezi.

Hadi sasa kumekuwa na taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa watu wengi wamenunua maeneo mwezini. Wengi wao wamenunua kutoka kwa The Lunar Registry.

Jina kamili la kampuni ya The Lunar Registry ni International Lunar Land Registry' (ILLR) - 'Masjala ya Kimataifa ya Ardhi ya Mwezi.' Ilianzishwa mwaka 1999.

ILLR inasema kufikia Julai 2019, watu 3,26,000 duniani kote wamejiandikisha kwa manunuzi ya ekari milioni 1.25 jumla za ardhi kwenye mwezi.

Hata hivyo, kampuni hiyo inaweka wazi kupitia tovuti yake kwamba wao sio wamiliki wa mwezi, bali wanasajili tu madai ya ardhi kwenye mwezi.

BBC iliwasiliana na shirika hilo ili kujua ni kwa msingi gani usajili huo unafanyika. Lakini hakukuwa na majibu kwa barua pepe wala simu hadi muda wa makala haya yanaandikwa.

Sheria zinasemaje?

“Je, kampuni binafsi au watu binafsi wanawezaje kuuza eneo ambalo ni mali ya binadamu wote?”

Mataifa Wanachama wa Umoja wa Mataifa yameingia makubaliano juu ya vitu vya anga, ukiwemo Mwezi. Mkataba huo unaoitwa 'Mkataba wa Umoja wa Mataifa na Kanuni za Anga za Juu' umetiwa saini na zaidi ya nchi 100 ikiwemo India.

“Maliasili zote angani, ukiwemo mwezi, ni mali ya binadamu kwa ujumla. Kifungu cha 2 cha mkataba huo kinasema kwamba, "hakuna nchi itamiliki rasilimali hizi kwa nguvu au kwa njia nyingine yoyote."

Lakini katika makubaliano haya ya 1967, haijasemwa popote kwamba watu binafsi hawana haki ya kumiliki eneo katika mwezi. Kuna ripoti katika vyombo vya habari kwamba mtu mmoja aitwaye Dennis Hope kutoka Amerika aliwahi kutangaza kuuza eneo kwenye mwezi na kupitia mauzo hayo alipata pesa nyingi .

N Raghunandan Kumar, mkurugenzi wa Planetary Society of India, anasema kwamba kununua eneo kwenye mwezi kutoka kwa watu binafsi au mashirika ni kupoteza pesa.

Umoja wa Mataifa unasema kwamba utajiri wa anga ni wa wanadamu wote. “Je, kampuni binafsi au watu binafsi wanawezaje kuuza eneo ambalo ni mali ya binadamu wote?” alihoji.
 
Hakuna mwanadamu aliyewahi kufika kwenye mwezi na jua,hata huko mars wameishia kupabatiza jina tuuu!ni ngumu sana kuishi mwezini,mwezi unatembea haujasimama!
Dunia IPO Kwa ajili yetu hatuendi kokote tupo hapa mpaka kifo.
 
Kwa hapa Tanzania mimi ndio muwakilishi wa hii kampuni. Kama unahitaji eneo lililopimwa unapata na hati ya serikali za mitaa. Tunauza viwanja kuanzia robo heka, nusu heka mpaka heka 5 na unasema kama unataka eneo kwa ajili ya makazi au biashara. Kama unahitaji njoo pm 🙄
 
Pesa hazina kazi huko duniani
Huku Tanzania pesa imefichwa
 
Dunia imejaa wajanja na wajinga kupindukia. sasa unanunua eneo mwezin? akili Gani hizo
Ni uwekezaji wa kubahatisha,labda inaweza kutokea baadaye sana ikawa dili kupata eneo huko,kwahiyo watu wanawekeza labda baadaye watapata faida kubwa
 
Ili uweze kununua ardhi mwezini ni lazima taifa lako liwe limefanya juhudi za kufika huko na kuweka alama.
Pale chombo kinapotua na eneo zima linalofanyiwa uchunguzi na wanasayansi wa nchi yako ndio eneo unaloweza kutangaza kulimiliki.
Mifano ya umiliki wa maeneo yasiyokaliwa na watu hapa Duniani kama mapande ya ardhi ya ncha ya kaskazini na ile ya kusini ni mifano tunayoweza kuitolea mifano.
 
Hakuna mwanadamu aliyewahi kufika kwenye mwezi na jua,hata huko mars wameishia kupabatiza jina tuuu!ni ngumu sana kuishi mwezini,mwezi unatembea haujasimama!
Dunia IPO Kwa ajili yetu hatuendi kokote tupo hapa mpaka kifo.
Kwani dunia imesimama?
 
Back
Top Bottom