Je unavitambua vyuo vikuu bora duniani?

Je unavitambua vyuo vikuu bora duniani?

Msuya Jr.

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2013
Posts
1,691
Reaction score
901
Je unavitambua vyuo vikuu bora duniani?
Chuo kikuu cha Oxford kimeibuka kidedea katika orodha ya vyuo vikuu bora duniani ya Times Higher Education. Hi ni mara ya kwanza kwa chuo kikuu cha Uingereza.

Oxford imeisukuma katika nafasi ya pili, California Institute of Technology, ambayo imekuwa ikiongoza orodha hiyo kwa miaka mitano iliopita .

Katika orodha ya vyuo vikuu bora barani Afrika, chuo kikuu cha Cape Town kimeibuka wa kwanza kutoka Afrika kusini kwenye orodha hiyo ya Times Higher Education.

Inadhihirisha umahiri wa taifa hilo, ambalo vyuo vyake vikuu 6 vipo katika nafasi za vyuo vikuu 15 bora kikwemo chuo cha Witwatersrand katika nafasi ya pili, Stellenbosch nafasi ya tatu, tChuo kikuu cha KwaZulu-Natal katika nafasi 5 na chuo kikuu cha Pretoria katika nafasi ya sita.

_91344200_66780b9e-d537-49ad-b8ed-80d5923bfb9d.jpg


Makerere kilichopo Uganda ndiyo chuo kikuu nje ya Afrika kusini kufanikiwa kuwa atika nafasi ya nne.

Vyengine ni chuo kikuu cha Ghana katika nafasi ya 7, na chuo kikuu cha Nairobi katika nafasi ya 8.

Orodha ya Times Higher Education duniani inapima vitu kama mafunzo, utafiti, na mtazamao wa kimaaifa - kwa mfano, idadi ya wanafunzi wanaotoka nje na wafanyakazi.

Nico Cloete, mkurugenzi wa taasisi ya Higher Education Trust na mratibu wa utafiti wa elimu ya juu na Advocacy Network in Africa, anasema taasisi hizo nne katika orodha ya Afrika - Cape Town, Makerere, Nairobi na Ghana - "zimeidhinisha mipango ya kuwa vyuo vikuu vinavyoongoza kwa utafiti" nchini mwao na vimeshuhudia "ongezeko kubwa kwa wanaofuzu kwa ushahada ya uzamifu na kuunda taasisi za utafiti katika miaka mitano iliopita". Je unavitambua vyuo vikuu bora duniani? - BBC Swahili

[HASHTAG]#Ila[/HASHTAG] naskia elimu ya uganda ni hafifu sana ukilinganisha na ya kwetu, sasa najiuliza inakuwaje makerere washike nafasi ya 4 kwa africa ikifuatiwa na nairobi university , huku chuo chetu cha udsm kulishosheheni maprofeseri tukiwa hatumo hata kumi bora,
embu wadau inakuwaje hapo.
 
Unasikia? Fanya utafiti mwenyewe ili kujiridhisha kama elimu ya Kiganda ni duni. Msomi hua hasikii.. anajionea.
 
Sina Imani Na tafiti hii,Vipo vyuo vingi tu naona Yaleeee ya miaka 10 iliopita
 
WaTZ tutasubiri sana dah hii nchi time will tell
 
Islamic university ya Moro mbona haipo hapo?
 
Back
Top Bottom