Je unaujua ubao wa maajabu uitwao Ouija?

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
896
1,000
Habari wadau katika pita pita zangu nimekutana na makala moja inayozungumzia huu ubao unaoitwa Ouija. Hii ni kile kidogo nilichokipata unaweza ukaongeza nondo pia, twende pamoja:

Mwaka 1891 kulizuka fununu nyingi kuwa kuna ubao mdogo tu wenye uwezo wa ajabu kwani ulikuwa una uwezo wa kujibu maswali ya kipindi kilichopita, kipindi cha sasa hivi pamoja na kipindi kijacho kwa uhakika na usahihi mwingi sana. Kwa wakati huo ubao huu ulinunuliwa mpaka dollar 1.50 za kimarekani.

Ubao umechorwa herufi za alfabeti 26 zilizopangwa kwenye mfumo wa nusu duara, pia kuna namba 0 mpaka 9. Maneno Yes na No yapo kwa kuu kabisa ya pande mbili za ubao. Neno goodbye lipo kwa chini. Kuna kifaa kimoja kinachoitwa Planchette kina tobo katikati kifaa hiki hutumika kwenye kuonesha herufi zile wakati wa mawasiliano.

Ufanyaji kazi wake:
Watu wawili au zaidi hukaa kwa kuzunguka ubao huu huku wakiwa wameweka vidole vyao kuu ya Planchette, kisha wanaweza kuuliza swali na hii Planchette uonesha majibu kwa kuanza kutembea kuanzia herufi moja mpaka nyingine.

Kuna theories nyingi kuhusu existence ya ubao huu:

1. Business Expertises wanadai kuwa hii haina uhusiano wowote na nguvu za giza bali ni mbinu ya kibiashara tu ya Businessman Elijah Bond ambaye ndo mbunifu wa kitu hii.

2. Ni hawa jamaa wa Paranomal activities ambao wanadai Kuna Ouija ina uhusiano wa moja kwa moja na nguvu za giza kwa zaidi ya asilimia 90 kwani kile kitendo cha kuwasiliana na mapepo tayari inakuwa sio business tena bali ni ishu ya spiritual.

NB: mpaka sasa kuna video clips nyingi zinazoonesha mambo ya kutisha kuhusu jambo hili kwani inaonekana wazi kuwa unaweza kuwasiliana na roho ya wafu kupitia Ouija Board.

Asante sana wakuu
#Mshana_jr #Malcom_Lumumba na wengine.

1_gsg6eR-a3PAbdsaO4B61DA.jpeg

Sent using Infinix hot 4
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
7,363
2,000
TAFADHALI SANA MTU ASICHEZE NA UBAO HUU KWANI UTAFUNGUA MLANGO KWA ULIMWENGU WA ROHO CHAFU NA CHOCHOTE CHAWEZA KUTOKEA KUANZIA MAUZAUZA MABAYA HADI KUINGILIWA NA KUMILIKIWA NA MAPEPO!
 
Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
896
1,000
TAFADHALI SANA MTU ASICHEZE NA UBAO HUU KWANI UTAFUNGUA MLANGO KWA ULIMWENGU WA ROHO CHAFU NA CHOCHOTE CHAWEZA KUTOKEA KUANZIA MAUZAUZA MABAYA HADI KUINGILIWA NA KUMILIKIWA NA MAPEPO!
Asante sana mkuu Fazili Naomba utupe Info zaidi ndugu

Sent using Infinix hot 4
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
7,363
2,000
Asante sana mkuu Fazili Naomba utupe Info zaidi ndugu

Sent using Infinix hot 4
Ukianza kutumia ubao huu, ambao hupaswi kuwa peke yako, lakini kwa vyovyote, unafungua mlango au uhalali wa mapepo na roho chafu kuwasiliana na wewe na hata kuanza kutawala maisha yako. Ubao huu una herufi na namba ambazo mapepo hutumia pale unapoyauliza maswali mbalimbali ya uaguzi.

Kimsingi huu ni uaguzi kama ulivyo uaguzi mwingine isipokuwa inakuwa wewe mwenyewe ndio mwaguzi ukiwasiliana moja kwa moja na pepo la uaguzi. Kwa kawaida yeyote afanyaye uaguzi ana ushikirika na mapepo ya uaguzi kwa makubaliano maalumu na anajua namna ya kuweka mipaka ya ushirikiano huo kwa mkataba maalumu.

Lakini watu wachezao na ubao wa Oija wengi ni wageni na wasiojua namna ya kuwasiliana na ulimwengu wa giza na hawana kinga yoyote kimkataba. Hivyo ulimwengu dhalimu wa giza hutumia upenyo huo kuingia kwenye maisha ya mtumiaji wa Oija board na kuharibu maisha yake ikiwa ni pamoja na kuleta mauzauza, kupagawa na kumilikiwa kipepo kitu ambacho ni kibaya sana,

Weka ubao huu mbali kabisa na udadisi wa watoto kwani watoto hupenda kudadisi mambo ya kiroho kupitia ubao huu. Wala tusijaribu kuingiza udadisi huu wa Oija hapa Tanzania kama haujaingia.
 
Sawa Nimekuelewa mkuu

Sent using Infinix hot 4
 
CaptainDunga

JF-Expert Member
Jul 17, 2009
1,559
2,000
Habari wadau katika pita pita zangu nimekutana na makala moja inayozungumzia huu ubao unaoitwa Ouija. Hii ni kile kidogo nilichokipata unaweza ukaongeza nondo pia, twende pamoja:

Mwaka 1891 kulizuka fununu nyingi kuwa kuna ubao mdogo tu wenye uwezo wa ajabu kwani ulikuwa una uwezo wa kujibu maswali ya kipindi kilichopita, kipindi cha sasa hivi pamoja na kipindi kijacho kwa uhakika na usahihi mwingi sana. Kwa wakati huo ubao huu ulinunuliwa mpaka dollar 1.50 za kimarekani.

Ubao umechorwa herufi za alfabeti 26 zilizopangwa kwenye mfumo wa nusu duara, pia kuna namba 0 mpaka 9. Maneno Yes na No yapo kwa kuu kabisa ya pande mbili za ubao. Neno goodbye lipo kwa chini. Kuna kifaa kimoja kinachoitwa Planchette kina tobo katikati kifaa hiki hutumika kwenye kuonesha herufi zile wakati wa mawasiliano.

Ufanyaji kazi wake:
Watu wawili au zaidi hukaa kwa kuzunguka ubao huu huku wakiwa wameweka vidole vyao kuu ya Planchette, kisha wanaweza kuuliza swali na hii Planchette uonesha majibu kwa kuanza kutembea kuanzia herufi moja mpaka nyingine.

Kuna theories nyingi kuhusu existence ya ubao huu:

1. Business Expertises wanadai kuwa hii haina uhusiano wowote na nguvu za giza bali ni mbinu ya kibiashara tu ya Businessman Elijah Bond ambaye ndo mbunifu wa kitu hii.

2. Ni hawa jamaa wa Paranomal activities ambao wanadai Kuna Ouija ina uhusiano wa moja kwa moja na nguvu za giza kwa zaidi ya asilimia 90 kwani kile kitendo cha kuwasiliana na mapepo tayari inakuwa sio business tena bali ni ishu ya spiritual.

NB: mpaka sasa kuna video clips nyingi zinazoonesha mambo ya kutisha kuhusu jambo hili kwani inaonekana wazi kuwa unaweza kuwasiliana na roho ya wafu kupitia Ouija Board.

Asante sana wakuu
#Mshana_jr #Malcom_Lumumba na wengine.

View attachment 1039185

Sent using Infinix hot 4
myth

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
896
1,000
Ukianza kutumia ubao huu, ambao hupaswi kuwa peke yako, lakini kwa vyovyote, unafungua mlango au uhalali wa mapepo na roho chafu kuwasiliana na wewe na hata kuanza kutawala maisha yako. Ubao huu una herufi na namba ambazo mapepo hutumia pale unapoyauliza maswali mbalimbali ya uaguzi.

Kimsingi huu ni uaguzi kama ulivyo uaguzi mwingine isipokuwa inakuwa wewe mwenyewe ndio mwaguzi ukiwasiliana moja kwa moja na pepo la uaguzi. Kwa kawaida yeyote afanyaye uaguzi ana ushikirika na mapepo ya uaguzi kwa makubaliano maalumu na anajua namna ya kuweka mipaka ya ushirikiano huo kwa mkataba maalumu.

Lakini watu wachezao na ubao wa Oija wengi ni wageni na wasiojua namna ya kuwasiliana na ulimwengu wa giza na hawana kinga yoyote kimkataba. Hivyo ulimwengu dhalimu wa giza hutumia upenyo huo kuingia kwenye maisha ya mtumiaji wa Oija board na kuharibu maisha yake ikiwa ni pamoja na kuleta mauzauza, kupagawa na kumilikiwa kipepo kitu ambacho ni kibaya sana,

Weka ubao huu mbali kabisa na udadisi wa watoto kwani watoto hupenda kudadisi mambo ya kiroho kupitia ubao huu. Wala tusijaribu kuingiza udadisi huu wa Oija hapa Tanzania kama haujaingia.
Lakini pia hii kitu nimesoma sehemu wanadai kuwa ina nguvu sana ya ushawishi aka convincing power yaani mtu akishapata introductory Info anatamani na yeye afanye hivyo ndo maana wengi wana kuwa watoto wa adolescents

Sent using Infinix hot 4
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom