Je, Unatafuta Programu kwa ajili ya Kikundi chako cha ViCoBa ?

Kibaba MFS

Member
Oct 1, 2016
14
6
3934065757.png


Kuhusu Kibaba MFS
Kibaba ni Program yenye uwezo wa kurahisisha kazi zinazofanywa na Vikundi ya Kuweka na Kukopa yaani ViCoBa, MFI na Upatu. Ukiwa na Programu hii utahitaji Kompyuta au simu au Tableti ili uweze kuweka kumbukumbu mbalimbali za wanachama. Hii itasaidia Kikundi kuachana na utegemezi pekee wa Kadi, Vitabu vya hesabu na Excel (Spreadsheet).

Vipengele kwenye Kibaba MFS (Features)
Vipengele vinavyounda Mfumo wa kibaba MFS.
  • Wanachama
    Kibaba inakuwezesha kuhifadhi taarifa za wanachama wako, Taarifa bifsi za wanachama zitakazowezesha kumtambua wakati wowote.

  • Mfuko wa Jamii
    Mfumo utakuwezesha kuandikisha Mifuko mbalimbali ya Jamii, kama Bima ya Afya, Elimu na mingineyo

  • Mikopo Hisa / Jamii
    Rekodi mikopo yote ya Wanachama, pata kumbukumbu ya kuchukuliwa mkopo na Tarehe ya Kurudisha mkopo

  • Miamala ya Kifedha (Transactions)
    Tunza kumbukumbu zote za Mapato na Matumizi kupitia kipengele hiki cha Miamala, hapa utaweza kurekodi tarifa za fedha.

  • Hamisho la Fedha
    Unaweza kufanya hamisho la Fedha kutoka akaunti moja kwenda nyingine. Kama vile simu pesa kwenda Akounti yenu ya Benki

  • Matangazo
    Mfumo unawezesha wanachama kuweka nakusambaza Matangazo / Ujumbe kwenye mtandao wa Kibaba, na wanachama wote wakaona.

  • Urithi / Inheritance
    Mfumo unaruhusu kuhifadhi taarifa za Warithi wa Mwanachama, unaweza kuweka hadi warithi 5 kwenye Databezi
  • Ununuzi wa Hisa
    Tunza taarifa na kumbukumbu za ununuaji wa Hisa za wanachama wa kikundi chako. Taafizi hizi hutumika kwnye mgao wa Mapato

  • Michango Maalum
    Unaweza kuanzisha na kukusanya Pesa kwa kutumia mfuko maalum, kuchangia mambo kama msiba, sherehe na N.K

  • Marejesho ya Mkopo Hisa / Jamii
    Rekodi marejesho ya mikopo ya Wanachama, Tarehe na Kiasi. Mpaka mkopo uishapo, na mfumo kukujilisha.

  • Akaunti za Fedha
    Unaweza kufungua Akaunti za fedha na kumbukumbu zake, inaweza kuwa Sanduku, Simu au hata Akaunti ya Benki.

  • Mgao (Dividend)
    Mfumo huu utakusaidia kufanya hesabu za mgao wa pesa, hesabu hufanyika kutokana na ununuzi wa hisa.

  • Upigaji Kura
    Ukitumiamfumo wa Kibaba, kufanya maamuzi ya pamoja ni rahisi, mfumo unaruhusu wanachama kuanzisha na kupigia kura jambo fulani.

  • Kujitoa Uanachama
    Mfumo unaruhusu kujitoa kwa Mwanachama, Taarifa zake zitabaki, ila Akaunti yake itakua sufuri.
Taarifa zaidi juu ya Programu hii tembelea portal yetu www.kibaba.co.tz
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom