Je, unajua ni kwanini ndoa hazidumu?

Je, unajua ni kwanini ndoa hazidumu?

saddyy

Member
Joined
Dec 28, 2014
Posts
58
Reaction score
54
Je, unajua ni kwanini ndoa hazidumu?

Ndoa hazidumu kwa sababu kabla ya kufunga ndoa watu wanakuwa Obssesed na Wedding Ceremony Imaginations, bila kujua Ndoa inaenda mbali zaidi! Kuna ndoa na kuna harusi.

Wengi mnapenda zaidi harusi na mnapowaza ndoa picha inayowajia ni Suti kali, Boonge la Shela kutoka Uturuki, Make Up ya ukweli ya bibi harusi kutoka Maznat Mikocheni, mashosti kuingia ukumbini na wimbo wa Alingo.

Wanafiki kukomeshwa kwa jinsi pati yako itakavyokuwa kali pale Karimjee Hall.Je, umewahi kuwaza mmeo au mkeo akiumwa miaka 5 mfululizo utaweza kumvumilia?

Umewahi kuwaza watoto watakapozaliwa na ulemavu utawa-care namna gani?? Mtakapokosa watoto miaka 6 ya ndoa utahimili maneno ya Mama Mkwe na Mawifi kwamba unawajazia Choo cha kaka yao na huna kizazi?

Ndoa ni zaidi ya sherehe ya Harusi. Baada ya yale Matarumbeta kuzimika usiku kifuatacho ni Majukumu mazito na Kiapo kisichovunjika. Achana na fantasy za kwaito, waza mbali kidoogo.

Je, Uko tayari kuwa mme au mke wa mtu mmoja tu au Ma-x watarejea kidogo kidogo kama hupati Satisfaction ya kutosha kama ya Ex wako? Huwa mnawaza hayo au mnawaza zawadi ya kama ti itatoa Benzi ya kuanzia maisha.
 
Je! UNAJUA NI KWANINI NDOA HAZIDUMU??
Ndoa hazidumu kwa sababu kabla ya kufunga ndoa watu wanakuwa Obssesed na Wedding Ceremony Imaginations, bila kujua Ndoa inaenda mbali zaidi!
Kuna Ndoa na kuna Harusi...Wengi mnapenda zaidi harusi, na mnapowaza Ndoa picha inayowajia ni Suti kali, Boonge la Shela kutoka Uturuki, Make Up ya ukweli ya bibi harusi kutoka Maznat Mikocheni, Mashosti kuingia ukumbini na Wimbo wa Alingo,Wanafiki kukomeshwa kwa jinsi pati yako itakavyokuwa kali pale Karimjee Hall.. Je, umewahi kuwaza Mmeo au mkeo akiumwa miaka 5 mfululizo utaweza kumvumilia?? Umewahi kuwaza Watoto watakapozaliwa na ulemavu utawa-care namna gani?? Mtakapokosa watoto miaka 6 ya ndoa utahimili maneno ya Mama Mkwe na Mawifi kwamba unawajazia Choo cha kaka yao na huna kizazi?? Ndoa ni zaidi ya Sherehe ya Harusi. Baada ya yale Matarumbeta kuzimika usiku kifuatacho ni Majukumu mazito na Kiapo kisichovunjika. Achana na Fantasy za Kwaito,waza mbali kidoogo... Je, Uko tayari kuwa Mme au Mke wa mtu mmoja tu au Ma-Ex watarejea kidogo kidogo kama hupati Satisfaction ya kutosha kama ya Ex wako??? Huwa mnawaza hayo au mnawaza Zawadi ya Kama ti itatoa Benz ya kuanzia maisha
 
Mkuu umetoa mawazo mazuri kabisaa, Mara nyingi kwa waliowengi hawayakumbuki hayo, binafsi nimeipenda maada ya Leo ! Wakati nikitaka kuoa ntajitahitidi kuyakumbuka hayo
 
upo sahihi, kumbuka wakati huo unakuwa na familia tano kwa pamoja
 
Umenena vyema mkuu, ni kweli wengi wanawaza hizo fantasy na kusahau life after wedding ceremony. Ahsante kwa kutukumbusha.
 
Mi bado nipo nipo sana maana nishajeruhiwa kwenye kutest
 
Tatizo tunataka funga ndoa na watu ambao twajua kabisa hawawezi tulia hata siku moja
 
kuna mwanaume nilimuuliza kwanini huoi? anasema "ah nikifikiria tu frustrations za harusi sitamani kuoa. na sipendi harusi"

sikuhizi couples either wanaishi pamoja bila harusi au hata kama hawaishi pamoja lakini bado wako tu kama married couple. marafiki wanawajua. wanaambiana matatizo ya familia. wanasadiana kifedha. unyumba.

kuna hollywood movie inaitwa "He's Just Not That Into you". ETI couple imeishi pamoja miaka nane. familia na marafiki wanawajua. mwanaume alienda hata kumuuguza mkwe. lakini mwanamke kila siku anajiuliza kwanini haolewi. mwanaume naye.anasema kwanini tuoane wakati tunaishi vizuri tu. hadi baadaee mwanaume akaamua wafanye harusi kwakuwa alikuwa anamoenda mwanamke huyo.

sasa swali: Kwani Ndoa ni Harusi??
 
Movie ni burudani na kujiliwaza tu !! lakini hali halisi unakutana nayo mnapo kuwa mshafunga pingu mke na mme!! Maisha yawejee ?!
 
me toka zamani nilijua sitokuja kufanya harusi kwakuwa nilijua ndugu hawangenifurahia. harusi ni kufurahia na uwapendao sasa kama unajua wao wataenda tu kukusikitikia kwenye harusi yako, what for?

kadri muda ulivyoenda nikaAdapt kutopenda harusi. sasa nazichukia kabisa. tena hizi za kuchangishana kiwango cha chini laki wakakti mimi mwenyewe laki.

ni kweli watu wengi wakifikiria ndoa hufikiria harusi tu. sio wasichana wa chuo sio maLate 30s. unakaa na "single ladies" wa late 30s nao wanawaza kuvishwa shela tu. sio kwamba hawastahili. nilifikiri angalau ukifika huko hata.mzuka wa kuvalishwa shela unaisha baada ya kuona ndoa za harusi za watu.
 
Movie ni burudani na kujiliwaza tu !! lakini hali halisi unakutana nayo mnapo kuwa mshafunga pingu mke na mme!! Maisha yawejee ?!

the point is kuna watu wako kwenye uhusiano ya muda mrefu, wanaishi pamoja na ndugu wanawajua. wengine hata plan za mtoto wanazo. lakini huku nje hatusikii cha harusi wala nini.

hali halisi mnaikuta mkishafanya harusi?? haha . elaborate.

uhusiano utadumu kama wote mkiwa commited kuudumisha whether kuna harusi or not.
 
the point is kuna watu wako kwenye uhusiano ya muda mrefu, wanaishi pamoja na ndugu wanawajua. wengine hata plan za mtoto wanazo. lakini huku mje hatusiki cha harusi wala nini.

hali halisi mnakutana mkishafanya harusi?? haha . elaborate.

uhusiano utadumu kama wote mkiwa commited kuudumisha whether kuna harusi or not.
Wengine husema ndoa ni karatasi !! Lamuhimu maisha yenu ni muruwa au madongo poromoko ?!!
 
Wengine husema ndoa ni karatasi !! Lamuhimu maisha yenu ni muruwa au madongo poromoko ?!!

eeh....watu bila kusign makaratasi wanaona hawajaoana. kama unampenda mwenzako anayetamani kusign karatasi mtimizie tu pale kwa mku wa wilaya? hata kama hutaki harusi....
 
Aaaa, Sisi kwetu ndoa bila sherehe na harusi kutangazwa rasmi ...Mmmh mambo hayaendi kbs !!!!
 
Back
Top Bottom