Je, unajua? Biblia ndiyo Kitabu kilichoandikwa kabla ya Vitabu vyote vya Kidini

Je, unajua? Biblia ndiyo Kitabu kilichoandikwa kabla ya Vitabu vyote vya Kidini

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,527
Reaction score
7,121
Biblia ni kitabu cha kwanza kuandikwa kabla ya vitabu vingine vyote vya kidini duniani. Sehemu ya kwanza ya Biblia — yaani Agano la Kale — iliandikwa maelfu ya miaka kabla ya vitabu au maandiko mengine ya kidini. Hii inatufundisha kuwa Biblia ndiyo chanzo cha kwanza kabisa cha ufunuo wa Mungu kwa wanadamu.

Na hii ndiyo sababu, Biblia imekuwa msingi wa maadili na sheria nyingi duniani. Amri Kumi za Mungu, (Kutoka 20:1–17) ni "uti wa mgongo" wa sheria za mataifa mengi, zikikemea wizi, uongo, uzinzi, uuaji, na ibada ya sanamu. Hata watu wasio na dini wanakiri kwamba mafundisho ya Biblia yana busara na nguvu ya kuongoza maisha yenye haki.

Kwa hiyo, kwa kuwa Biblia ni ya kwanza, ina ukweli wa kwanza na wa mwisho. Kuiweka pembeni na kuamini vitabu vingine, ni sawa na kumweka Mungu pembeni.

Katika Yohana 12:48 tunaambiwa kwamba anayemkataa Yesu na kuyakataa maneno yake; maneno aliyoyasema Yesu yenyewe ndiyo yatamhukumu siku ya mwisho.

Moja kati ya maneno aliyosema Yesu - katika Biblia ni kwamba ,Yeye(Yesu) ndiye njia, kweli na uzima. Hakuna awezaye kwenda mbinguni kwa Baba, bila kupitia kwa Yesu (Yn 14:6).

Na tukumbuke kuwa Yesu Kristo ndiye atakayewahukumu wanadamu wote siku ya mwisho (Mdo 17:31). Siku ya mwisho imekaribia sana kwa jinsi dalili zinavyoonyesha. Shetani anaujua ukweli huu, ndiyo maana anahangaika mchana na usiku kuwashawishi watu wasisome Biblia. Anajua kwamba wakiisoma wataujua ukweli, na ukweli huo utawaweka huru na kuwaokoa kutoka dhambini, na kwa njia hiyo watapata tiketi ya kuingia mbinguni. Shetani anataka watu waangamie pamoja naye motoni.

Usimpe nafasi Shetani. Kataa uongo wake na maajenti wake wanaopindua ukweli wa Biblia. Soma Biblia, na uishi kulingana na yote aliyoyaagiza Yesu. Kumbuka tena: Biblia ndiyo itakayokuhukumu siku ile ya mwisho.
Yohana 12:48
"...yule anayenikataa mimi na kuyakataa maneno yangu; yale maneno niliyoyasema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho."
 
Biblia ni kitabu cha kwanza kuandikwa kabla ya vitabu vingine vyote vya kidini duniani. Sehemu ya kwanza ya Biblia — yaani Agano la Kale — iliandikwa maelfu ya miaka kabla ya vitabu au maandiko mengine ya kidini. Hii inatufundisha kuwa Biblia ndiyo chanzo cha kwanza kabisa cha ufunuo wa Mungu kwa wanadamu.

Na hii ndiyo sababu, Biblia imekuwa msingi wa maadili na sheria nyingi duniani. Amri Kumi za Mungu, (Kutoka 20:1–17) ni "uti wa mgongo" wa sheria za mataifa mengi, zikikemea wizi, uongo, uzinzi, uuaji, na ibada ya sanamu. Hata watu wasio na dini wanakiri kwamba mafundisho ya Biblia yana busara na nguvu ya kuongoza maisha yenye haki.

Kwa hiyo, kwa kuwa Biblia ni ya kwanza, ina ukweli wa kwanza na wa mwisho. Kuiweka pembeni na kuamini vitabu vingine, ni sawa na kumweka Mungu pembeni.

Katika Yohana 12:48 tunaambiwa kwamba anayemkataa Yesu na kuyakataa maneno yake; maneno aliyoyasema Yesu yenyewe ndiyo yatamhukumu siku ya mwisho.

Moja kati ya maneno aliyosema Yesu - katika Biblia ni kwamba ,Yeye(Yesu) ndiye njia, kweli na uzima. Hakuna awezaye kwenda mbinguni kwa Baba, bila kupitia kwa Yesu.

Na tukumbuke kuwa Yesu Kristo ndiye atakayewahukumu wanadamu wote siku ya mwisho — siku ambayo imekaribia sana kwa jinsi dalili zinavyoonyesha. Shetani anaujua ukweli huu, ndiyo maana anahangaika mchana na usiku kuwashawishi watu wasisome Biblia. Anajua kwamba wakiisoma wataujua ukweli, na ukweli huo utawaweka huru na kuwaokoa kutoka dhambini na kwa njia hiyo watapata tiketi ya kuingia mbinguni. Shetani anataka watu waangamie pamoja naye motoni.

Usimpe nafasi Shetani. Kataa uongo wake na maajenti wake wanaopindua ukweli wa Biblia. Soma Biblia, na uishi kulingana na yote aliyoyaagiza Yesu. Kumbuka tena: Biblia ndiyo itakayokuhukumu siku ile ya mwisho.
Yohana 12:48
"...yule anayenikataa mimi na kuyakataa maneno yangu; yale maneno niliyoyasema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho."
Mmh kweli hilo mkuu?
Maandiko ya kale zaidi kuliko Biblia yapo

Maandiko ya Kihindu (Vedas):
-Rig Veda (sehemu ya Vedas) iliandikwa karibu karne ya 15–12 KK, kabla ya baadhi ya vitabu vya Agano la Kale kama Isaya au Danieli.

Hii inafanya maandiko ya Kihindu kuwa miongoni mwa maandiko ya kidini ya zamani zaidi yaliyoandikwa.

Maandishi ya Wamisri na Mesopotamia: Epic of Gilgamesh (kuhusu gharika) iliandikwa takriban 2000 KK kabla ya uandishi wa kitabu cha Mwanzo.
Wamisri walikuwa na maandiko ya dini na maadili (kama The Book of the Dead) kabla ya Torati.

Biblia yenyewe iliandikwa kwa awamu Sehemu ya kale ya Biblia (Torati au Vitabu 5 vya Musa) iliandikwa takriban karne ya 15–12 KK (kulingana na baadhi ya wataalamu), lakini vitabu vingine viliandikwa baada ya karne ya 6 KK. Kwa hiyo, haikuwa kitabu kimoja kilichoandikwa mara moja mapema kuliko vyote.

Ufunuo wa Mungu haukubanwa kwa Biblia pekee Wenyeji wa mataifa mengi ya kale walidai kupokea ufunuo kutoka kwa miungu yao, hata kabla ya Biblia kuwepo.
Biblia ilikumbwa na udhsaifu mwingi kama kuingiza mawzo ya watu mgongano nk.

Qur'an ilikuja kama mwongozo wa moja kwa moja kutoka kwa Mungu, uliopangiliwa kwa mtiririko wa kimungu na si hadithi za binadamu. Qur'an inaahidiwa kulindwa na Allah mwenyewe (Qur'an 15:9).

Qur'an ilishushwa kurekebisha na kuthibitisha ukweli wa maandiko ya awali, lakini pia kufuta upotoshaji, kuondoa dhana za kibinadamu juu ya Mungu, na kulinda ujumbe wa tauhidi kwa ukamilifu. Ndo ufunuo wa mwisho kwa binaadamu.
 
Mungu muumba wa mbingu na Ardhi na vilivyomo,Mungu Mkuu ambaye hana mfanano na chochote katu hajawahi kuleta kitabu kinaitwa Biblia/Bible.

Vitabu alivyoshusha ni Zaburi,torati,Injili org na Quran tukufu.
Hiyo biblia/bible kaja nayo Mtume yupi?
 
Vitabu alivyoshusha
Vitabu havikushushwa, my friend. Soma historia. Biblia iliandikwa na watu lakini kwa uongozi wa Mungu.
2 Timotheo 3:16
Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki.”
 
Mungu muumba wa mbingu na Ardhi na vilivyomo,Mungu Mkuu ambaye hana mfanano na chochote katu hajawahi kuleta kitabu kinaitwa Biblia/Bible.

Vitabu alivyoshusha ni Zaburi,torati,Injili org na Quran tukufu.
Hiyo biblia/bible kaja nayo Mtume yupi?

Bro, kwa taratibu tu. Je alishushaje hivi vitabu?.

Na Kwa lugha ipi ? Ya mbinguni?

Au Na Kwa kupitia nani?.
 
Umekaririshwa, au hujachimba historia ya dini. Umewahi kusoma kiitabu cha ' the book of the dead' ? Kimeandikwa miaka mingi kabla ya hiyo biblia uisemayo. Hata Musa yajulikana amri 10 alizitoa humo.
 
Umekaririshwa, au hujachimba historia ya dini. Umewahi kusoma kiitabu cha ' the book of the dead' ? Kimeandikwa miaka mingi kabla ya hiyo biblia uisemayo. Hata Musa yajulikana amri 10 alizitoa humo.
Asante kamwamu kwa maoni yako. Ngoja nikudadavulie utaelewa tu.

The Book of the Dead sio kitabu cha kidini kama Biblia. The Egyptian Book of the Dead ni mkusanyiko wa maneno ya mazishi na dua za kiibada, zilizokuwa zinawekwa katika makaburi ya Wamisri wa kale kwa ajili ya kuandaa roho ya marehemu kwa maisha baada ya kifo. Hicho sio kitabu cha mafundisho ya imani kwa jamii nzima, bali ni nyaraka za maziko na ushirikina wa kale kwa sababu hakina mpangilio wa kihistoria, kimaadili, wala kimaisha kama Biblia. Jina tu lenyewe "the book of the dead" linajieleza. Hakikuandikwa kwa ajili ya watu walio hai.

Biblia ni tofauti. Ni mkusanyiko wa vitabu 66 vyenye historia, sheria, unabii, mashairi, na mafundisho ya kimaadili kwa watu wote. Ndicho kitabu cha kwanza cha kidini kilicho na mfumo wa kufundisha jamii nzima kuhusu Mungu aliye hai.

Kuhusu hoja yako kwamba Musa alitoa amri 10 humo, hiyo sio kweli. Amri Kumi (Kutoka 20) zililetwa na Mungu kwa sauti na maandishi ya moja kwa moja juu ya mlima Sinai, sio kwa kusoma the book of the dead.

Musa mwenyewe alikulia katika nyumba ya Farao na alijifunza hekima zote za Wamisri, lakini alipotumwa na Mungu, hakutegemea elimu ya Kimisri bali mafunuo ya moja kwa moja kutoka kwa Mungu.

“Na Bwana akasema na Musa uso kwa uso, kama vile mtu asemavyo na rafiki yake.” (Kutoka 33:11)

Kwahiyo ndugu yangu, usidanganyike. Biblia ni kitabu cha kipekee, cha kwanza, na cha kweli.
 
Kwa kukusaidia tu, dini za kwanza na mwanzo kabla ya hiyo dini yako kuundwa kuna hizi

1.Anciet Mesopotamian religion (3500-500BCE)

2- Ancient Egyptian religion (3100-300 BCE)
Dini iliyohusu Miungu ya kimisri kama Ra (Sun God au original God ambaye wagiriki na warumi walibadiri stories za huyu Mungu mwana jua na kuunda kiumbe yesu/jesus miaka ya baadae sana)
Pia ktk dini hii kuna Miungu mingine kama Osiris na ISis.

3. Hinduism (1500BCE - till today)
4. Zoroastrianism (1200 - 600 BCE)
5. Judaism (1000- 500BCE)
6. Greek&Roman ( 800 BCE-400)
7. Buthism (500BCE)
8. Taoism (500BCE)

Na hapo sijaorodhesha dini na mafundisho mengine mengi ambayo si famous sana ulimwenguni na yalishakuwepo kabla ya kuundwa kwa biblia na ukristo kiujumla.

Dini ya ukristo imekuja juzi tu wakati huo kuna mamia ya imani na nakala zao zilishakuwepo zamani sana, huo uislamu ndio wakae kimya kabisa maana hawa kila mtu anajua wamekuja juzi juzi hapo baada ya urumi kushirikiana na muarabu kuunda hiyo dini mpya ya uislamu.

Dunia ya sasa si ile ya wajinga ambao mliwaaminisha kila takataka zenu za kidini kuwa ni sahihi, wakati huu kuna sources nyingi za kupata information za mambo ambayo yalifichwa, nawashauri wafia dini, someni sana msitegemee uongo wa vitabu vyenu ufunge fahamu zenu kuyajua mambo nje ya dini zenu.

Ukristo na hiyo biblia umecopy hadithi kutoka ktk asili ya imani za kimisri au Afrika ya kale, na kuunda huo upuuzi wa akina yesu sijui akina yehova na TAKATAKA zingine mnazoka
lilishana makanisani.
 
Biblia ni Kitabu pekee cha Kale cha Kweli kilicho na mafundisho ya Mungu Mwenyezi:
 
Shida yako ume-copy na ku-paste aliyokuandikia chatGPT bila kutafakari ameandika nini. Mimi mada yangu haizungumzii dini za kale. Nimezungumzia kitabu cha kwanza cha kidini chenye mafundisho mazito kwa jamii na ambacho kimetumiwa na mataifa mbalimbali kuandika sheria.
 
Unazungumzia hii quran ambayo imenakiliwa 1924 tena hapo misri? Mpaka hii leo hakuna ushahidi unaoonesha ni ipi qurani iliyochapishwa na khalifa wa kwanza akiitwa abubakar
 
Unazungumzia hii quran ambayo imenakiliwa 1924 tena hapo misri? Mpaka hii leo hakuna ushahidi unaoonesha ni ipi qurani iliyochapishwa na khalifa wa kwanza akiitwa abubakar
Nimezungumzia Biblia, sio Qur'an
 
Binafsi nachojua ni kuwa biblia ni mkusanyiko wa vitabu... Hii kunasema biblia ni kitabu😖
 
Back
Top Bottom