TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 6,551
- 20,259
Challenge ya Dola Milioni Moja (Tsh 2.5b) ilikuwa zawadi maarufu iliyotolewa na James Randi Educational Foundation (JREF) kwa mtu yeyote ambaye angeweza kuthibitisha uwezo wowote wa kisaikolojia, kimiujiza au wa kichawi chini ya mazingira ya kisayansi yaliyodhibitiwa (controlled environment).
Maelezo Muhimu:
Challenge hii ilianza mwaka 1964 (awali ikiwa na zawadi ndogo), na mwaka 1996 ikafikia dola 1,000,000.
Waliohitajika: Watu wote waliodai wana nguvu za ajabu — wahubiri, manabii, wachawi, waganga wa jadi, watu wanaodai kusoma nyota, wapiga ramli, na wengine — waliruhusiwa kushiriki.
Masharti: Mshiriki alipaswa kukubaliana na jaribio la kisayansi lililoandaliwa pamoja na JREF ili kupima huo uwezo wa ajabu. Jaribio hili lilibuniwa kuwa rahisi, la wazi na lisilo na mianya ya udanganyifu.
Matokeo: Hakuna mtu yoyote aliyewahi kufaulu hata kwenye hatua za awali, achilia mbali kushinda kitita hicho! Maelfu waliomba kushiriki, lakini hakuna aliyeweza kuthibitisha hizo nguvu za ajabu chini ya usimamizi wa kisayansi.
Mwisho: Changamoto hii ilisitishwa rasmi mwaka 2015, ikiwa ni miaka 50 bila kupatikana mshindi na James Randi kustaafu.
Mshana Jr na wenzio mngetoboa?