Je unafurahia ndoa/mahusiano yako?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je unafurahia ndoa/mahusiano yako?!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Eiyer, Apr 27, 2012.

 1. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Tukubali tukatae wapo ambao wanatamani dunia irudi nyuma ili ndoa zao zife,kwani wanashindwa kufanya hivyo sasa kwa sababu ya kidini au za kutokujiamini!Ngoja nikwambie kitu,hakuna Mungu atakaekuchoma moto au kukuadhibu kwa kuvunja ndoa yenye ufujaji au mateso ya aina yoyote.Mungu anataka ufurahie ndoa yako.Jisikie fahari kuwa na mkeo/mumeo.Kama ni kinyume hebu fikiria kama kuna ulazima wa kuwepo kwenye ndoa hiyo.Wanawake ndo wahanga wakubwa wa matatizo ya ndoa..Wengi huvumilia mateso ya ndoa kwa kuhofia usalama wa watoto,ngoja nikuambie,unapoendelea kukaa kwenye ndoa ya mateso unamharibu mwanao mpenzi kihisia na kimwili pia,kile unachoepuka kumpata mwanao ukiondoka,ndicho anakipata ukibaki.Usihofu kuhusu ugumu wa maisha,hata hapo unateseka pia.Ndoa ni furaha kwa mke ,mume na watoto,kama ni kinyume haina uhalali wa kuwepo!
   
 2. Primitive

  Primitive JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 223
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  • :target:
   • :target:
   • :target:it sounds like imekutokea!! najaribu kufikiri tu!!

   • :target:
   • :target:


   
 3. DERICK2000

  DERICK2000 JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 204
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama haikufurahishi ya nini kujikaza mkuu,kama ndoa sawa,lakini mahusiano kabla hamjaoana.unaangalia ustaarabu mwingine,kuna jamaa aliliaga siku ya honeymoon yake.kaoa mwanamke ambae hakumpenda sana,ila kwa ajili ya muda ndo ulifika wa kuoa.ikabidi afanye hivyo na ndo huyo aliekuwa nae karibu.Umakini unatakiwa cna,kabla hujaingia ndoani.
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Eiyer ndugu yangu, haya mambo ya ndoa kutokuwa na furaha na kuendelea kukaa katika ndoa inategemea unaongelea kundi gani hasa kwa akina mama.

  Kuna kundi linalojitambua na limejiwezesha kiuchumi kiasi cha kuweza himili kujikimu kwa mahitaji madog, hawa wanaweza kuwa na mtazamo wa kutoka ndoani na kufurahia maisha.

  Kuna kundi kubwa la akina mama wa nyumbani ambao wategemea 100% waume zao, huyu utamwambiaje atoke kwenye ndoa kisa hana furaha? Tena ukute ana watoto akiwaza aondoke waje walelewe na mwanamke mwingine ambaye hana hakika kama atawapenda na kuwatendea haki ama la!
  Na mwanamke wa aina hii ana woga mkubwa wa kwenda kuanza maisha peke yake.

  Hii ishu sio rahisi kama inavyopchukuliwa jamani.
   
 5. Ndetirima

  Ndetirima JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 898
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 60
  Sijakuelewa umeanzisha hii mada kwa ajili ya kuelimisha au kwa ajili ya kuwashauri watu waachane. Nakuomba uwe muangalifu sana na mada kama hii, watu wamesomea kazi ya kuelimisha kuhusu maisha ya ndoa na jinsi ya kuingia kwenye ndoa. Madhehebu yote ya Dini yanafundisha kuhusu ndoa, wanajamii wote wenye ufahamu na uzoefu wanashauri kuhusu mambo ya ndoa, kuwa makini ndugu na mada za namna hii usije ukawa kikwazo kwa kuingilia mambo usioyajua.
   
 6. k

  kibali JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 315
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Eiyer nadhani una mantiki,hakuna sababu ya kufa na tai shingoni kama mapenzi yamefikia ukomo!
   
 7. k

  kibali JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 315
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Jaribu kumsoma EIyer vizuri umuelewe,hana maana ya kuachanisha watu! anatamani sana ndoa ziwe kama lilivyo kusudi la Mungu,alichojaribu kuasa ni ile hali ya mtu kuteseka maisha yake yote akiwa kny ndoa ilhali,kila aina ya suluhu imeshatafutwa bila mafanikio! hujawahi ona au sikia ndoa ambazo wazazi,friends,washenga,dini, mahakama wameplay part yao wameshindwa?lazma tukubali kuwa kuna solution nyingine ambayo ni chungu sana:doh:
   
 8. k

  kisukari JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,763
  Likes Received: 1,052
  Trophy Points: 280
  mimi sioni tatizo la maelezo yake.kuna ndoa nyengine hata ujaribu kuzisuluhisha vipi,inakuwa bure tu.kwa hiyo kuelezea upande mwengine wa shilingi sio vibaya.
   
 9. k

  kisukari JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,763
  Likes Received: 1,052
  Trophy Points: 280
  jee wewe yalishakukuta?na kama yalikukuta ulichukua uamuzi gani?maana wakati mwengine unaweza uka advice kitu,na yakija kukutokea,yale uliyoshauri kwa upande wako,huyatekelezi
   
 10. The dirt paka

  The dirt paka JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kwakweli sina hata wakusingiziwa so naomba niwe wakuhesabu wanaofurahia na wasiofurahia.
   
 11. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #11
  Apr 27, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuu inawezekana wewe ni ndugu yangu eeh kwenye nyekundu!
   
 12. m

  mtotomzuri Member

  #12
  Apr 27, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  currently siko kwenye uhusiano,2 yrs back nlikuwa kwenye uhusiano,it was just a relationship though tulikuwa tumepanga kwamba tutaoana na mambo mengine mengi tu,i never enjoyed that relation, i was always a victim,sijui yule mkaka alitaka uhusiano na mimi kwa ajili gani kwa sababu yan me ndo nlikuwa chombo chake cha kutolea hasira,kila siku ilikuwa kudharauliwa kutukanwa, mwisho nlichoka nkaona isiwe tabu,it was so difficult kutoka,so so difficult coz he was my first and my only he was supposed to be my fare tale,bt he never was bt thank God nlifanikiwa kuachana nae,he,kept coming back n i pushed him away,coz i came to realize that he is not worth of my love,i have moved on with my life,natarajia kufunga ndoa next month,aliposikia hivyo eti anakuja kuomba msamaha tena ooh ule ulikuwa utoto,ooh nikirudi nyumbani najiua,sababu kibao, i dont listen to him coz am happy with my new man n life is full of colors for me,Mungu aliliona chozi langu amekuja kunikumbatia na kunifuta machozi,hii ni kwa akina dada wanaoteseka kwenye mahusiano yao,even if its marriage usiruhusu mwanaume akuonee eti kwa hofu kwamba ukimwacha wewe hutapata mwingine,hiyo siyo kweli. well,usiogope jamii itasemaje mkiachana,kumbuka unayeteseka ni wewe na hiyo jamii inakucheka,siku ukifa kwa ukimwi watakuita malaya na kwenda kukuzika na kukusahau,WOMEN THIS IS YOUR LIFE DONT LET ANYONE PLAY WITH IT,BE THE DRIVER OF YOUR OWN LIFE!
   
 13. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #13
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Kongosho,hebu rudia kusoma threa yangu halafu ucommet upya!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #14
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Asante sana ndugu yangu!
   
 15. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #15
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Bado sijaoa ndugu,una swali?
   
 16. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #16
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  mtotomzuri,si umesema hauko kwenye uhusiano?Vp tena ndoa?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #17
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  mh!umesema hauko kwenye uhusiano afu next month unaolewa how can that be posible? mtotomzuri
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #18
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  well said Eiyer some people wanakubali kua watumwa wa mapenzi eti kisa kuhofia jamii itamchukuliaje?.to me its diferent kabisa hua ni mwepesi wa kuchukua hatua where necesary hua sifugi maradhi..
  Wengine unakuta ni mahusiano tu ya kawaida na sio ndoa but unakuta mtu anavumilia hata yasiyofaa eti kisa mapenzi,akhaa mie siwezi..
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #19
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa ndugu hata mtotomzuri nae alikua na tatizo hili.Nae alikua kwenye uhusiano tu akawa anaogopa kutoka humo!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #20
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa ndugu hata mtotomzuri nae alikua na tatizo hili.Nae alikua kwenye uhusiano tu akawa anaogopa kutoka humo!Sijui tatizo hasa hua nini,wanawake ndo wana majibu haya!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...