Umeweka link ya mtu ambaye hajui hata Kiswahili, mimi nimekupa neno la Kiswahili linalounganisha neno "mizungu" na "Miungu/Mungu".Nimekuwekea link inayoonyesha asili ya white people kupewa jina la wazungu. Wewe unaniletea origin ya neno "mizungu"
Niwekee link ulipotoa hiyo information kuwa wazungu walipewa hilo jina kwasababu wako kama miungu. Weka hiyo link nijisomee then nirudi hapa
natamani sana kufahamu,formula ama huo uwezo ambao watu wanao.kwamba wamepewa na Mungu au shetani,maana kubadili kiumbe hai kukifanya utakavyo sio rahisi ivo.nafahamu binadamu tunatengeneza na kubadilisha vitu visivyo na uhai.ila uchawi wa kumfanya nyoka amuue,binadamu au kutumika kwa kazi hizo ni ngumu kuamini.Hayo ndo maswali ambayo hata Mimi nilikuwa najiuliza,hivi inakuwaje mtu anadai nyoka kiumbe ambacho ni hatari kwa binadamu
critical thinker
hapo hapana shaka kabisa mkuu,sababu unaelezea kituambacho kipo au kinawezekana...shida ipo,kwenye misingi ya imani au hao watu wanaotumia wanyama kiuchawi hapo ndo kuna shida.utakuta mtu anakwambia amemkuta nyoka ndani au sehemu ambayo haiwezi kupitika kabisa,sasa huyo kaingiaje au hapo kafundishwa vp....hapo ndo nataka kufahamu uchawi unafanya kazi vp na kubadili vile vitu ambavyo physically tunaona haviwezekani.Mazee, unaaminikwamba mbwa anawezakufundishwa kurukia mpira? Au tembo anaweza kufundishwa kucheza mpira?
Kuna videos You Tube wanyama wanafundishwa kucheza michezo ya ajabu ajabu. Wengine wanafundishwa mpakakufanya hesabu.
Ukipeleka shows kamazile vijijini huko,ukawaambia watumimi nina nguvu za kichawi za kuwasiliana na wanyama, wanakuamini.
Kuna m South Africa anacheza na Simba. Watu wa vijijini wakiona zile video watasema huyu mchawi.
Bibi wa watu pengine kwao wana utamaduni wa kucheza na nyoka miaka mingi, watu wanasema mchawi.
Ukiangalia movie ya majoka kwenye giza, mtu akija kwanyuma akakugusa mguuni tu unaruka kwa kufikiri umeguswa na nyoka.
Ndicho kinachotokea kwenye jamii zetu.
Tumesimuliwa sana stories za uchawi, kikitokea kitu kidogo tu chenye mazingira yanayoweza kuelezekakwa nadharia ya uchawi,tunasema uchawi.
Akitokea kibibi ana machomekundu anatembea uchi kwa magonjwa ya akili na ana decorations za kiasili, watu wanasema mchawi, wanamuua.
Hawataki kumchunguza.
Kumbe ukimpeleka Muhimbili kwa Profesa Kilonzo akampimaakili anakwambia huyu ana severe schizophrenia au magonjwa mengine ya akili, alitakiwa kwenda therapy na kupata dawa tangu mtoto,ilakwetu hamna hayo mambo. Ugonjwa wa kilinimpakauokote makopo.
Yaani kila mtu alikuwa na maswali mengi yasiyo na majibu,Hivi kama wewe mfano unadaiwa huyo nyoka unamtoa wapiNingemuuliza tu huyo bibi ana kibali cha kufuga wanyamapori hapo kwenye shamba lake mpaka ifike hatua ya yeye kufuga nyoka hapo?
Mkuu walimfanyia nini Magu hapo ikulu? hebu tupe uhondo kidogo.Nasikia wamemfanyia hiyo Magufuli Ikulu mpaka anataka kuhamia Dodoma.
Ila mimi siamini uchawi. Inawezekana ni sayansi isiyojulikana tu.
Nikupe mfano.
Ukimchukua mtu wa miaka ya 1600 huko, ukamuonyesha jinsi ndege inavyopaa, jinsi mawasiliano ya internet na redio yanavyofanya kazi,etc, halafu ukamwambia huu uchawi, most probably atakubali ni uchawi.
Kwa sababu kwake ni vitu vya ajabu.
Kumbe ni vitu vinavyoweza kuelezeka naturally tu,huhitaji supernatural powers kuvielezea.
Kuna muandishimmoja nampenda sana wa science fiction, anaitwa Arthur C. Clarke, alisema "Any sufficiently advanced technology is indistiguishable from magic".
Teknolojia yoyote iliyoendelea sana haitofautiani na uchawi.
Sasa mtajuaje mnachoita uchawi ni uchawi (i.e, supernatural powers) au ni kitu kinachotumia sayansi na teknolojia ambayo hamjajijua tu (i.e natural powers but unknown at the time) ?
How do you tell the difference?
Wale mababu zetu walioona wazungu wanajua kutabiri kupatwa kwa jua waliwaona wazungu wachawi (ndiyomaana wakawaita wazungu,wazungu maana yake ni miungu - ukichukua mzungu ukatoa z unapata mungu -).
Sasa tutajuaje kwamba tunachofikiri ni uchawi si sayansi tofauti tu ambayo hatujaijua?
If at all the suspicion is authentic.
Ngende habari nyingine.Mkuu ngende masasi au?hakuna makanisa ya kilokole?
Sent from my TECNO W5 Lite using JamiiForums mobile app
Maswali yako yanafikirisha mkuu...Kuna watu wanaamini mitini miungu yao, wanaomba kwenye miti.
Walikuwa wanaheshimumazingira,na leo tunajuakwamba mitiinasaidia kutunza mazingira na kuleta mvua.Wao waliiabudu mitina kukataza isikatwe. Wakiomba mitiiwatunze. Na kwaaina fulani ya kufikiri, walikuwa sawa, kwa sababu mitiilisaidia kuwatunza.
Sasa ule uanamazingira wa asili nao utaitwa uchawi nao?
...
Wale mababu zetu walioona wazungu wanajua kutabiri kupatwa kwa jua waliwaona wazungu wachawi (ndiyomaana wakawaita wazungu,wazungu maana yake ni miungu - ukichukua mzungu ukatoa z unapata mungu -).
....
Kwenye "mzungu" upo tayari itolewe "z" ili iwe "mungu" ila kwenye "zunguka" unaulizia "ka" imeenda wapi.
Kuna maneno yanabadilika kadri muda unavyoenda na wakati mwingine hata maudhui ya neno husika huweza kuhama kabisa.
Wazunguka kubaki wazungu ni inawezekana. Ni kama neno mwanamume kuwa mwanaume.
Jamani tuwaache wazungu, karne zilizopita wazungu walikuwa wanajua wachawi kama sisi tunavyoua Leo. Na criteria walizozitumia ni kama sisi tunazozitumia Leo.wao walikuwa wanasema Mzee mwenye macho mekundu na ambayo ana uzito mdogo below sikumbuki kana ni 50 au 60 kg which means atakuwa mwepesi kupaa na fagio waliuwawa. Uzuri wao wametengeneza mpk museums kwa ajili ya kumbukumbu kwa vizazi vijavyo. Tunavyovipitia Leo wao walishavipitia may be tumechelewa kimaendeleo lakini naamini tutafika haya mambo ya uchawi wa kulogana hatutayasikia tena
Kurogwa hakuombwi bali kuna sababu zake hadi kufikia hatuya ya kutogwa.Hivi we unadhani wale walio act movie za kichawi walibuni tu or there are something behindHakuna kitu kinachoitwa uchawi.
Hizi ni imani tu ambazo hazina ukweli wala uhalisia wowote.
Nilishaomba kurogwa toka miaka mingi lakini hakuna kitu kama hicho.
Nadhani hukumwelewa vizuri ila alichokwambia kuwa hizi imani hazikuwa Africa tu hata Ulaya pia zilikuwepo lakini baada ya kuingia kwa ustaraabu wa middle East ndo wakaziachaKwa hiyo unakubali kuwa tuwaue mama zetu au baba zetu wembamba (ambao hatuwatunzi vizuri) na hii ni kutokana na matoto ya siku hizi yakifika mjini yanawasahau wazee wa kule kolomije?? Tuwaue kwa sababu wanaruka kwa fagio?? Haya nayaita mawazo mgando man.
Sio kila mwenye macho mekundu ni mchawi wala sio kila mwembamba ni mchawi. Kulogana kupo na kutaendelea kuwepo. Hakuna mchawi mkubwa kama anayekuchongea kwa boss wenu kila kakosa kadogo huku akiutumia mwili wake kumpumbaza boss. Nimewahi kufukuzwa kazi kwa kosa ambalo sikulitenda kumbe kisa ni mwanamke alimtaka boss amwandike kazi mdogo wake.
Kuna mchawi mbaya kama huyo?? Mama yangu alikufa na zaidi ya miaka 100 tuseme alikuwa mchawi?
Kwa hiyo unakubali kuwa tuwaue mama zetu au baba zetu wembamba (ambao hatuwatunzi vizuri) na hii ni kutokana na matoto ya siku hizi yakifika mjini yanawasahau wazee wa kule kolomije?? Tuwaue kwa sababu wanaruka kwa fagio?? Haya nayaita mawazo mgando man.
Sio kila mwenye macho mekundu ni mchawi wala sio kila mwembamba ni mchawi. Kulogana kupo na kutaendelea kuwepo. Hakuna mchawi mkubwa kama anayekuchongea kwa boss wenu kila kakosa kadogo huku akiutumia mwili wake kumpumbaza boss. Nimewahi kufukuzwa kazi kwa kosa ambalo sikulitenda kumbe kisa ni mwanamke alimtaka boss amwandike kazi mdogo wake.
Kuna mchawi mbaya kama huyo?? Mama yangu alikufa na zaidi ya miaka 100 tuseme alikuwa mchawi?