Siku nyingi nimekuwa siamini kama kweli kuna uchawi katika Tanzania hii, achilia mbali huko kwa wengine. Nimekuwa siamini makosa yote hapa nchini yana adhabu zake ispokuwa la uchawi hii ikimaanisha kuwa Serikali inaamini kuwa hakuna uchawi. Hatahivyo, siku za hivi karibuni imani yangu imeanza kupungua baada ya Kingozi mmoja katika Serikali hiyo hiyo inayoamini kuwa hakuna uchawi kudai kuwa amegundaua mbinu kuwa anarogwa ili awe zoba auwawe kirahisi. Sasa nikajiuliza, huyu mtu yumo ndani ya Serikalini inayoamini kuwa hakuna uchawi, akiwa pekee yake kuna uchawi, inakuwaje hapa?
Aidha, jana tarehe 28/03/2011 nilikuwa nasikiliza Redio Wapo FM kuanzia saa 1.30 jioni kipindi cha "yaliyotufikia" nikasika kuwa kuna fisi ameshambulia watu huko Mto wa Mbu, akawauwa na askari wa wanyama pori, baada ya kuauwa, wakakuta ametobolewa masikio kama alikuwa anawekewa hereini.
Je, huyu fisi alikuwa anashiriki mashindano ya "Miss Mto wa Mbu" au ni fisi wa wachawi?
Sasa wana JF wenzangu ni kweli kuna uchawi? Au ni njama za wajanja kutishia wenzao.
Uchawi upo mkuu,ila fisi kutobolewa masikio kama vile alikuwa aikivaa hereni inawezakana sio uchawi,kwa sababu watafiti na wanasayansi mbalimbali wa viumbe huwa wanawawekea viumbe monitors au kamera klingana na utafiti wanaotaka kufanya.Inawezekana fisi huyo alishawahi kufanyiwa utafiti huo,ndo maana alikuwa ametobolewa masikio,sio masikio tu wanaweza kuweka vifaa hivyo maalum sehemu yoyote kulingana na aina ya kiumbe
kwani serikali ni nini? Inakuwaje serikali haiamini katika dini lakini viongozi wana dini? Haya yakipata majibu, hata la uchawi majibu yatapatikana
serikali lazima iseme haitambui uchawi kwani kesi ya uchawi ushaidi wake hauwezi kuwa rahisi kutolewa waziwazi lazima matendo ya kichawi yatumike sasa unafikiri hakimu atkubali kushuhudia vimbwanga mahakamani?
Amini usiamini uchawi upo ila imani yako ndiyo itakuongoza katika hilo unaweza ukauamini au usiuamini, uchawi ni nguvu za ngiza
... Nimekuwa siamini kwa sababu makosa yote hapa nchini yana adhabu zake ispokuwa la uchawi hii ikimaanisha kuwa Serikali inaamini kuwa hakuna uchawi....
CHAPTER 18
_______
THE WITCHCRAFT ACT
An Act to provide for the punishment of witchcraft and of certain acts connected
therewith.
[28th December, 1928]
1. This Act may be cited as the Witchcraft Act.
2. In this Act unless the context otherwise requires–
"court" includes a local court as defined in the Magistrates Courts Act;
"instrument of witchcraft" means anything which is used or intended to be used or is commonly used, or which is represented or generally believed to possess the power, to prevent or delay any person from doing any act which he may lawfully do, or to compel any person to do any act which he may lawfully refrain from doing, or to discover the person guilty of any alleged crime or other act of which complaint is made, or to cause death, injury or disease to any person or damage to any property, or to put any person in fear, or by supernatural means to produce any natural phenomena, and includes charms and medicines commonly used for any of the purposes aforesaid;"police force" means the Tanzania Police Force;
"public officer" means any employee of Government or of a local government authority;
"witchcraft" includes sorcery, enchantment, bewitching, the use of instrument of witchcraft, the purported exercise of any occult power and the purported possession of any occult knowledge.
Shria ipo tena nadhani it is one of the oldest legislations in Tz that is has yet to to repealed:
Agalia wakati mwingine spelling zaweza kuaribu maana ya kile ulichokusudia. Hebu hii " akawauwa na askari wa wanyama pori, baada ya kuauwa, wakakuta ametobolewa masikio kama alikuwa anawekewa hereini" Hii haijatulia.
Uchawi upo, kuna simba alivamia mbagala akajeruhi mtu mmoja alivyouawa tu ndani ya sekunde chahce walikuta kanyofolewa zehemu zake za siri jamani zilipelekwa wapi? nilishangaa sana. You never know huyo fisi walimvisha hiyo hereni ili fsi wengine wasijitokeze mitaa hiyo kila watu wana imani yao.
Uchawi upo.