Je, una tatizo la kukosa usingizi?

Je, una tatizo la kukosa usingizi?

jabirj864

Member
Joined
Nov 22, 2019
Posts
9
Reaction score
13
Tatizo la kukosa usingizi (Insomnia - Sleep Disorder).

Usingizi ni muhimu katika maisha ya mwanadamu kama ilivyo kula mlo kamili na kufanya mazoezi.

Kukosa usingizi kunachangiwa na mabadiliko ya kimwili, kiakili, na kihisia.
Kukosa usingizi kunaweza kuathiri afya kwa ujumla pamoja na ubora wa maisha.

- Karibia watu milioni 40 wanasumbuliwa na tatizo la kukosa usingizi.

- Kiafya unashauriwa kulala angalau:
• Masaa 10 kwa siku kwa mtoto mdogo rika la kwenda shule
• Masaa 9 hadi 10 kwa siku kwa vijana, na
• Masaa 7 hadi 8 kwa siku kwa watu wazima.

- Kukosa pumzi ukiwa umelala ni tatizo hatari ambapo pumzi zinasimama kwa muda ukiwa umelala.

Kuwa na uzito uliokithiri kunachangia kwa kiasi kikubwa mtu kukosa pumzi wakati akiwa amelala.

- Kulala muda mchache kunachangia mtu kupata Kisukari.

- Kulala usingizi wa kutosha kunazuia kupata magonjwa ya kushindwa kufikiri na kupoteza kumbukumbu wakati wa uzee wako.

- Tafiti zinabainisha kuwa kuuvuruga usingizi kunapelekea kupata Shinikizo la Juu la Damu, Magonjwa ya moyo, Msongo wa mawazo, Unene uliokithiri, pamoja na Kisukari.

- Wanaofanya kazi kwa kubadilishana muda (Shift workers), ambao hawapati muda wa kutosha wakulala usingizi, wako hatarini kupatwa na magonjwa sugu ya moyo pamoja na magonjwa sugu kwenye mifumo yao ya tumbo na utumbo.

- Matumizi ya chai na kahawa kwa wingi, hasa hasa masaa machache kabla ya kulala, yanakuzuia kupata usingizi wakutosha.

- Wanawake wenye matatizo ya homoni za kike, wanashida ya kupata usingizi.

- Kukaa masaa 17 pasipo kupata usingizi kunapelekea kuvuruga utendaji kazi wa ubongo, na kuwa sawa na mtu aliyekunywa pombe yenye kilevi cha asilimia 0.05%.

- Tafiti zinaonesha kuwa kutopata usingizi wakutosha (pungufu ya masaa 6) kunahusianishwa na asilimia 12% kuwa kwenye hatari ya kufa.

- Kufanya mazoezi pamoja na kuzingatia chakula bora
 
Back
Top Bottom