Je, umewahi kukutana na binti mnayejuana lakini akukeletea dharau kutokana na alivyo?

Shida na raha

JF-Expert Member
Aug 8, 2014
3,773
3,471
Tabia hii imekolea sana miongoni mwa vipusa wanaodhani kuwa wanapofanya hivi basi wanajiongeza hadhi huku wakikupunguzia.
Unakutana na binti njiani lakini kutokana na sababu umevalia mavazi ya kupendeza, nywele zako ni nadhifu au pengine sura au umbo lako la kupendeza badala ya kukupongeza, anatumia dharau kukufanya uhisi duni.
Lakini umewahi kujiuliza ni nini hasa kinachowapa vipusa wa aina hii nguvu za kukudunisha? Pengine ni kutokana na sababu kuwa wewe pia haujioni kufaa kila unapofanyiwa vituko vya aina hii.
Iwapo wewe ni mmoja wa hao vipusa wenye mazoea ya kulia au kujionea huruma kila unapokenuliwa, futa machozi na ukumbuke kuwa wivu ndio unawachochea kwani bila shaka una kitu fulani wasichokuwa nacho. Pengine ni urembo, umbo, tabia njema, subira au hata ukarimu, sifa wasizokuwa nazo na hivyo wanatumia mbinu hii kujifanya wahisi vyema.
Pia kuna wale wanaodhani kuwa eti kwa sababu amepiga hatua fulani maishani basi wengine walio chini yake ni taka. Naam! kipusa anayedhani kuwa elimu yake ya ziada, mavazi yake ghali au gari la kifahari analoendesha vinampa tiketi ya kumdunisha mwenzake.
Usimpe nafasi na ikiwezekana usimuachie mwanya wa kupata nafasi ya kukudunisha.
Kuna wale ambao ili ukubalike katika kundi lao basi sharti lazima ufikie viwango vyao vya mavazi, maisha na kielimu.
Wasipokukubali ulivyo waache
Usikubali kuingia kwenye madeni katika harakati za kutaka kuwafurahisha wenzako. Ikiwa hawawezi kukubali jinsi ulivyo basi haina haja ya kuendelea kujumuika nao.
Hii inanikumbusha binti mmoja aliyeishia kusakamwa na madeni baada ya kujitwika mikopo mbali mbali katika harakati za kufanana na wenzake. Binti huyu alishia kupoteza kila kitu nyumbani baada ya benki kuanza kumdai.
Nijuavyo kila mtu ameumbwa na sifa zake za kipekee na hivyo hauhitaji kujidhihirisha kwa wenzako kwa kuvaa mavazi ya bei ghali au kuandamana nao katika mikahawa ya kifahari ili kukubaliwa.
Iwapo kujikubali jinsi ulivyo kutakupelekea kutengwa na wanaotaka ubadilike ili kufikia viwango vinavyowafaa basi binti ni heri uwe mpweke.
Kando na hayo kaa mbali na wanaoonekana kukerwa na uwepo wako na kamwe usiwape nafasi ya kutumia dharau dhidi yako ili kujituliza.
 
Daa neelewa Sana hii, hasa point namba moja, unakutana na binti, wew umependeza Sana tu, lakin yeye ana act kama hakuon wala hakupi sifa zako, zaid zaid anaweza kumsifia rafik yako wa pemben ili we uumie. Sijui kwa nn hii
 
Kuna binti mmoja alipomaliza form 6 majibu hayakuwa mazuri akawa kitaani. Tukishusha vinywaji tunamnunulia,nauli tunampa,vocha sana na stori kwa wingi hakuna aliyemtamani maana mama yake alikuwa mtata sana.
Mungu si mzee mkumba binti akaingia mamlaka ya forodha, Kibosile mmoja juu akamkamata akamshika mkono.
Binti akapigishwa shule nje ya nchi ofisini akapanda cheo mpaka akamilili maghorofa hamadi ukikutana nae anaangalia pembeni
 
Point hapa nini, nisaidieni ni kutaka kusifiwa, kupewa kipaumbele, kushobokewa au heshima.

Sijaelewa...
 
Back
Top Bottom