Je, ulishawahi kulazimisha mpenzi au rafiki aendelee kubaki maishani mwako?

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,686
106,810
images (23).jpeg

Salute mates...

Kwenye mizunguko yetu ya maisha kuna wakati unakua upo very attached na mtu Fulani either ni rafiki wa kawaida kama Man to man au Man to woman, pengine ni mpenzi wako umpendae sana sana. Yaani unakuta una mpenzi roho yako imetokea kumpenda sana husikii wala huoni juu yake, kila muda unatamani uwe nae karibu au kuwasiliana na nae. Au kama ni rafiki yako wa kiume unakua kila ukitaka kufanya kitu Fulani unamstua mshikaji wako, yaani kama kuna ishu unatka kufanya mshikaji wako bila kuwepo unaona unaifanya kimagumashi. Kiuhalisia unakua upo mentally attached to that person, unakua umempa nafasi kubwa sana mpenzi wako au mtu huyo kwenye akili yako na maisha yako kwa ujumla.

Je huo upendo na nafasi kubwa uliyompatia kwenye maisha yako ushachunguza kama naye anakupatia nafasi hiyo? Jibu ni No! na kama ni Yes basi nafasi hiyo amekupa kwa muda, kuna muda utamtext atakujibu kwa wakati wake, utatamani kuongea nae ila yeye ataona unaboa tu, utataka uonane nae yeye atakuona msumbufu.
FB_IMG_16226657897141411.jpg

Ikifika hatua unaona mtu yupo online unamtext pm ana like tu, unamtext wasap ana soma then anakaa kimya sana au unamtext kwa sms halafu yeye kaka kimya wakati unajua hiyo sio kawaida yake jua kwamba huna chako hapo, utakua unalazimisha mawasiliano, mapenzi au urafiki ambao mwenzako hautaki tena.
FB_IMG_16477608029012993.jpg


Kwanini ulazimishe mawasiliano au mapenzi ? Kila kitu chatokea kwa sababu. Unajua unapompenda na kumjali mtu sana kiasi asicho stahili utaishia kupata maumivu usiyo stahili..

Subconscious mind hutenda kazi ikishirikiana sambamba na Nature, kuna hali Fulani unawez kua nayo katika maisha labda ni upweke,huzuni,kukosa faraja kiufupi unakua huna furaha au amani ya maisha. So kinachotokea ni kwamba
Subconcious mind inawasiliana na Nature kua mwanadamu huyu (yaani wewe) una matatizo Fulani maishani inaiamuru nature kutafuta mtu wa kuja maishani mwako ambae ataendana na hali ile uliyonayo.

Baada ya muda mfupi utajikuta umepata rafiki ukawa nae anakuliwaza kweli hadi ile hali ikawa imeisha..Mind ikishaona mentally ya huyu mtu iko stable inamuamuru nature kuruhusu yule mtu kuondoka au akaendelea kubaki. Hapo sasa ndio utaona umepata rafiki labda ni mwanamke au mwanaume akawa anakupa company sana kwa hali uliyonayo kwa muda Fulani (hata mwaka mzima. Unajikuta umekua attached sana na mtu huyo then inafika muda bila sababu yoyote ile ya msingi unaona mawasiliano na urafiki unapungua taratibu then unaisha kabisa. Hapo nature inakua ishafanya yake..
4d23851d92974d52deee387c457157a6--japan.jpg


Nachotaka kusema ni kwamba watu ambao mpo kwenye mahusiano jifunzeni kusoa alama za nyakati, so unaona hapa mapenzi au urafiki unaanza kuisha ila wewe ndio bado unazidi kuongeza kupiga simu na kumfuata ili aendelee kubaki…Kijana kila kitu kinakuja kwa muda na sababu Fulani, hutakiwi kutumia nguvu kubwa kumfanya mtu aendelee kubaki kwenye maisha yako. Mtu kama ni muhimu kwenye maisha yako atakuja mwenyewe na kukaa nawe daima, huna haja ya kulazimisha.

Kwanini ulazimishe mahusiano? Watu wote hawa waliojaa duniani au unadhani yeye ndio bora pekee kuliko wote, mwache aende labda alikua sio riziki ya maisha yako! Utapata mwingine. Kikubwa zaidi ambacho hutakiwi kukifanya maishani mwako ni kupuuzia ubaya wa mtu anaokufanyia kwakua unahitaji mtu huyo aendelee kubaki maishani mwako, train your mind to be stronger than your feelings.

Kingine maishani mwako usionyeshe wema au uzuri wako ili uwafanye wavutiwe nawe, waonyeshe ule upande wako ambao ni mbaya uone kama watakuvumilia au wataondoka. Wakiondoka usijali jua ni watu fake. Be real that’s beautiful enogh kijana.
Mwaka mpya,misimamo mipya..Uliumbwa mwenyewe! Huyo mpenzi au rafiki yako umpendae sana ambae unaona huwezi fanya kitu bila yeye ni wa kupita tu.

Hamishia nguvu zote kwa mama yako ndio the best one ambae hatakuja kukusaliti. Jiamini katika uwezowako, unaweza kufanya makubwa bila mpenzi wako huyo ambae unaona huwezi fanya kitu kikafanikiwa bila yeye.If you Doubt your power, you power your doubt.

Binafsi hua sijali wala kujutia chochote maishani mwangu, ukinipenda Ahsante na karibu, ukiondoka hamna shida pia.. you weren't meant to stay in my life, if you were! You will stay in my life forever
A guy has said, It’s up to you To choose me or to loose coz I’m not a second choice
With or Without you, I shine!
FB_IMG_16496251534422957.jpg


Da'Vinci
-Excelsior
 
Binafsi ninahisi nina Phobia ya kuogopa kua attached kwa mtu fulani, Maana najua tu mwanzo atanionyesha wema na upendo ila mwisho ndio atanionyesha upande wake wa shillingi..mmhh. Ila wanasema maisha ni kutake risk, if you can't take you loose a chance
 
Ukitengeneza mazingira ya kupata faraja kwa wengine jiandae kulia! Kila mtu ajitambue mtu wa kwanza kujiweza ni yeye mwenyewe.. Ni vigumu mtu kujisaliti ana kujidanganya mwenyewe hivyo be the first to handle the best of you.
 
Nafikiri huu ni mtihani mgumu sana kwa mwanadamu, hisia ni kitu cha ajabu sana, kuhisi furaha, raha, amani,utoshelevu huwa kunakufanya ujione umekamilisha kitu kikubwa sana, halafu ukiachilie hicho kitu kirahisirahisi tu kiende duuuh moyo wangu💔
Yaani kuandika tu haya moyo unanienda kasi
Seems like upo attached sana kwa mtu unahisi yy ndio kashikilia pumzi na riziki yako.
Hiyo nguvu si ungeelekeza kwa Mungu maana ndio anagawa pumzi na riziki
 
dah, imenitokea mara mbili, kumpenda mwanamke ki urafiki kupita kiasi, mmoja tumekua marafiki for 9 years , akaanza kubadilika since mwaka jana mwishoni sijamtafuta tena, mwingine tumedumu miezi 4 tu


Sent from my iPhone using JamiiForums
Pole sana kijana.. Never beg for friendship, never beg to be loved. Things that are belong to you will come and stay. Hizo ndio falsafa zangu!
 
Kijana kila kitu kinakuja kwa muda na sababu Fulani, hutakiwi kutumia nguvu kubwa kumfanya mtu aendelee kubaki kwenye maisha yako. Mtu kama ni muhimu kwenye maisha yako atakuja mwenyewe na kukaa nawe daima, huna haja ya kulazimisha.
Haya maneno hayafanyi kazi kwa mtu anayempenda mtu kweli.
Wanasema "if you love something, fight for it".
Yaani ukae uache kupambana ukidhani kwamba atakuja mwenyewe?.
 
Haya maneno hayafanyi kazi kwa mtu anayempenda mtu kweli.
Wanasema "if you love something, fight for it".
Yaani ukae uache kupambana ukidhani kwamba atakuja mwenyewe?.
Mimi sijui ila Nadhani maybe sijapenda au nimeukomaza moyo wangu kwa mitazamo ya kua mpweke pweke.
Mfano..
Hua najisemea I'm useless one, nobody needs me! So kwa mentally hii hata mpenzi akiniacha najua tu I'm no tdestined to he loved.
 
Mimi sijui ila Nadhani maybe sijapenda au nimeukomaza moyo wangu kwa mitazamo ya kua mpweke pweke.
Mfano..
Hua najisemea I'm useless one, nobody needs me! So kwa mentally hii hata mpenzi akiniacha najua tu I'm no tdestined to he loved.
Maisha hayana kanuni, ukimpenda mtu wako pambana hadi umpate, hata asipojibu msg pambana. Mwanaume "kupambania kombe" eti. Usikubali kushindwa juu ya kitu unachokitaka kirahisi.

Sio kwenye mahusiano tuu, hata kwenye maisha kiujumla. Pambana , usiseme tuu kama riziki ni yangu ni yangu tuu na itakuja. Utasubiri riziki ijilete hadi mwisho wa dunia.
 
Back
Top Bottom