Je, Ufaransa Inaheshimu Uhuru wa Kujieleza?

Joined
Nov 23, 2018
Posts
97
Reaction score
205
Salaam wanajamvi

Kwa wafuatiliaji wa siasa za Ulaya bila shaka tumeshangazwa na kauli za hivi karibuni za viongozi wa Ufaransa kuwa ati nchi yao imejengwa kwenye misingi ya kuheshimu haki za Binadamu. Baada ya jarida la kifaransa, Charlie Hebdo kuchapisha katuni za dhihaka kwa mtume Muhammad, rais wa nchi hiyo Emmanuel Macron aliwatetea wahariri kuwa wanatimiza uhuru wao wa kujieleza. Wiki chache zilizopita yaani Agosti 31,2020 rais Macron alizuru nchi ya Lebanon kwa ziara ya siku mbili. Akiwa huko alikutana kwa siri na kiongozi wa kundi la Hezbollah, Hassan Nasrallāh na kufanya naye mazungumzo. Mwandishi wa habari George Malbrunot akatumia uhuru wa habari na kujieleza kwa kuripoti mkutano wa Macron na Nasrallāh. Hata hivyo rais alimshambulia na kumtisha bwana George Malbrunot kwa kuchapisha habari hiyo.[FRENCH PRESIDENT EMMANUEL MACRON VERBALLY ATTACKS A JOURNALIST WHO EXPOSED HIS SECRET MEETING WITH A HEZBOLLAH LEADER DURING LEBANON VISIT
https://t.co/JnCTIXMN]

Laiti Macron angekuwa anaheshimu uhuru wa kujieleza kama anavyojinasibu, tulitaraji asimtishe mwandishi huyo bali amtetee sawa na alivyowatetea wahariri wa Charlie Hebdo. Lakini ndio kama walivyosema wahenga kuwa njia ya mwongo ni fupi.

Mfano wa Ukiukwaji wa Uhuru wa Kujieleza nchini Ufaransa:[emoji116]

Kadhia ya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa ujumla na uhuru wa kujieleza kimahususi kwenye nchi ya Ufaransa ni ya kitambo kabla ya rais Macron. Licha ya kujinasibu kuwa Ufaransa ni kinara wa kulinda haki za Binadamu, mwenye kutafuta ukweli atagundua kwamba kuheshimiwa haki za binadamu hasa Uhuru wa kujieleza kwa nchi hii ni maneno matupu(merely a slogan). Mfano mahususi wa ukandamizaji wa uhuru wa kujieleza unamhusu Mwanafalsafa na msomi nguli wa Ufaransa, Roger Garaudy(17 Julai 1913 – 13 Juni 2012). Huyu alikuwa msomi, mshairi, mwanafalsafa na mwanafikra wa kifaransa. Anatazamwa kama mwanafalsafa mkubwa zaidi wa kimagharibi kwa sasa baada ya akina Plato. Ameandika vitabu vingi ambavyo vimetafsiriwa kwa lugha mbalimbali za Ulimwengu.Misukosuko kwa Roger Garaudy ilianza pale alipoandika kitabu cha uchunguzi alichokiita ˝Les Mythes fondateurs de la politique Israélienne”(Uongo wa kutengeneza wa Sera ya Israeli). Katika kitabu hicho alitumia nadharia ya 'Conspiracy' kuelezea uzushi wa mauaji ya maelfu ya wayahudi baada ya vita ya pili ya dunia(holocaust). Bwana Garaudy alihoji ikiwa tukio la 'holocaust' ni ukweli wa kihistoria au uwongo tu wa Israeli katika kuvuta huruma ya walimwengu ili hatimaye waweze kuhalalisha ukaliaji kimabavu ardhi ya Wapalestina. Kama kulikuwa na shida kwenye hoja na ushahidi wa Bwana Roger Garaudy basi ilitarajiwa atokee mtu mwingine wa kuandika kitabu cha utafiti kufafanua uongo wa Bwana Garaudy kwa kuwa utafiti hujibiwa kwa utafiti. Hata hivyo mamlaka za Ufaransa ziliamua kukipiga marufuku kitabu hicho jambo linalokwenda kinyume na uhuru wa Kujieleza kama ilivyo kwenye Ibara ya 27 kifungu cha pili cha Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu(Universal Declaration of Human Rights) kisemacho:
"Every one has the right to the protection of the moral and material interests resulting from any scientific, literary or artistic production of which he is the author”
Yaani, "Kila mtu ana haki ya ulinzi wa utu wake na vitu vyake anavyopendelea vinavyotokana na sayansi, fasihi, vitu vya sanaa ambavyo yeye ndio mwandishi wake”

Ulipofika mwaka 1998, Garaudy alishtakiwa kwa mujibu wa sheria ya Ufaransa kwa kuwaudhi Wayahudi na kutozwa faini kubwa kama adhabu ya kupinga mauaji ya Wayahudi milioni sita nchini Ujerumani na sehemu nyingine (holocaust).

Chakushangaza zaidi ni ni pale mchapishaji Mjerumani ambaye alitafsiri kazi ya Garaudy kwa Kijerumani kulazimishwa kuiuza kampuni yake ya Uchapishaji na hatimaye kampuni hiyo kufutwa rasmi kwenye orodha ya makampuni ya Uchapishaji ya Ujerumani. Upande mwingine wa shilingi Salman Rushdie alipoandika kitabu cha kuukashifu Uislamu alichokiita "Satanic Verses"(Aya za shetani), alipongezwa kote Magharibi, akapokea tuzo na kazi yake kutafsiriwa kwenda lugha mbalimbali za Ulaya.

Ufaransa iliyojengwa kwenye misingi ya kuheshimu haki za Binadamu pia ina sheria inayopiga marufuku vazi la stara ya wanawake wa kiislamu(burqa na niqāb). Kwa nchi inayothamini uhuru wa na haki za Binadamu ilitarajiwa kadhalika kuheshimu uhuru wa kujichagulia mavazi(Freedom in the choice of attire and dressing) kwa kuwa hiyo ni haki muhimu ya Binadamu. Badala yake Ufaransa imepiga marufuku hata vazi la heshima la ufukoni(bukini) na askari huwalazimisha wanawake wa kiislamu wanaotaka kubarizi ufukoni kuvaa bikini.

Kwakweli kinachoonekana Ufaransa na nchi zingine za Magharibi, uhuru ni ule unaoendana na tamaduni zao kama kuruhusu ushoga na kumvunjia heshima Mungu. Sio katika uhuru mtu kufanya yale yanayokinzana na misingi yao ya kishetani. Na huo ndio undumilakuwili wa Uhuru wa nchi za Magharibi.

Ushauri wangu kwa Waislamu wa Tanzania [emoji1241]

Inapotokea akatukanwa mtume wetu, Mola wetu au matukufu mengine ya dini yetu ni heri tutafute ufumbuzi wa hilo kwa kurejea kwenye mafunzo sahihi ya dini yetu. Ifahamike sio katika mafunzo ya kiislamu kuwatukana wasio waislamu kama anavyosema Allāh kwenye Qur'ān :

وَلَا تَسُبُّوا الَّذِينَ يَدْعُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ فَيَسُبُّوا اللَّهَ عَدْوًا بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ كَذَٰلِكَ زَيَّنَّا لِكُلِّ أُمَّةٍ عَمَلَهُمْ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِمْ مَرْجِعُهُمْ فَيُنَبِّئُهُمْ بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ
“Wala msiwatukane hao wanao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, wasije na wao wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila ya kujua. Namna hivyo tumewapambia kila umma vitendo vyao. Kisha marejeo yao yatakuwa kwa Mola wao Mlezi, naye atawaambia waliyo kuwa wakiyatenda.”
[Al-An'ām, 6:108]

Vile vile tunapojadiliana na watu wa kitabu(Wakristo na Wayahudi) tutumie njia nzuri kama tulivyoamrishwa na Allah:
وَلَا تُجَادِلُوا أَهْلَ الْكِتَابِ إِلَّا بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ إِلَّا الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْهُمْ ۖ وَقُولُوا آمَنَّا بِالَّذِي أُنْزِلَ إِلَيْنَا وَأُنْزِلَ إِلَيْكُمْ وَإِلَٰهُنَا وَإِلَٰهُكُمْ وَاحِدٌ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ
“Wala msijadiliane na Watu wa Kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa, isipo kuwa wale walio dhulumu miongoni mwao. Na semeni: Tumeyaamini yaliyo teremshwa kwetu na yaliyo teremshwa kwenu. Na Mungu wetu na Mungu wenu ni Mmoja. Na sisi ni wenye kusilimu kwake.”
[Al-Ankabūt, 29:46]

Ushauri wangu kwa majirani zetu Wakristo wa Tanzania [emoji1241]

Historia inaonesha Uislamu ulianza kuingia Tanzania kabla ya Ukristo kwa karne 10 sawa na miaka 1000. Licha ya kwamba dini yenu ililetwa na Wakoloni bado watawala wa Kiislamu kama Sayyid Said wa Zanzibar aliruhusu kujengwa kanisa la kwanza kwenye ardhi ya Waislamu Zanzibar kisha Bagamoyo na penginepo. Tangu hapo wazee wetu waliishi kwa kuheshimiana pamoja na sera ya kikoloni ya kuwagawa Waafrika (Divide and Rule Policy). Hata baada ya Uhuru tunaendelea kuvumiliana kiimani japokuwa wachache wanachafua taswira yetu ya tangu kale. Katika harakati za kidini, wakristo mnayo haki ya kututangazia imani yenu na hata kukosoa yale mnayoona si sawa kwenye misingi ya imani yetu. Katika kufanya hivyo zingatieni udugu,ujirani na ushahidi wa maandiko. Tukikosoana kistaarabu kama tufanyavyo mara nyingi, hakuna damu itakayomwagwa. Vinginevyo hayo tunayoyasikia kwa wenzetu yatabisha hodi na huku.

Usidanganywe na mtu ukamtusi mtume wetu Muhammad صلى الله عليه وسلم ,au ukachana nakala ya Qur'ān ati kwa kisingizio cha Uhuru wa kujieleza. Waislamu wamefunzwa kumpenda mtume wao Muhammad kuliko wanavyojipenda wao na familia zao. Amesema Mtume Muhammad ﷺ:
«َ ﻟَﺎ ﻳُﺆْﻣِﻦُ ﺃَﺣَﺪُﻛُﻢْ ﺣَﺘَّﻰ ﺃَﻛُﻮﻥَ ﺃَﺣَﺐَّ ﺇِﻟَﻴْﻪِ ﻣِﻦْ ﻭَﻟَﺪِﻩِ ﻭَﻭَﺍﻟِﺪِﻩِ ﻭَﺍﻟﻨَّﺎﺱِ ﺃَﺟْﻤَﻌِﻴﻦَ»
“Hawi muumini mmoja wenu mpaka niwe kipenzi kwake kuliko watoto wake, wazazi wake na watu wote”
[Rejea : Sunan an-Nasa'i 5013]

Kumzungumzia mtume kwa kutumia vibonzo na matusi sio uhuru, sio urafiki bali uchokozi wa wazi na uadui. Ikiwa hivyo ndivyo yakikukuta ya kukukuta huna wa kumlaumu kwani utakuwa ni Mwana kulitafuta, mwanakulipata".

Mwl Longino AR
[emoji2398]2020
Liwale Lindi
 
Mkuu nimekuelewa sana. Ila macaroni anachokitafuta from islamic state ni cha hatari sana. Ni bora aachane nao kabisa.

kama ufaransa haina uhuru wa kujieleza ni nchi zipi zenye uhuru huo hebun zitaje basi hata tano ili tujifunze
 
Nifanyaje nami niwe na uelewa wa Mambo ya kimataifa?..
Umeuliza swali zuri, hongera kwa kuwa nashauku ya kuongeza ufahamu kunako uga wa kimataifa. Kwakweli vijana wengi wa Tanzania tumekua hatuna interest ya kufuatilia siasa ya kimataifa na kama itafanyika study yawezekana tukawa chini zaidi kati ya hizo nchi. Utafiti uliowahi kufanywa zamani ulionesha kuwa Marekani ni kinara wa umbumbumbu wa Mambo ya nje(woefully ignorant of foreign affairs) [Almond 1960; Kriesberg 1949] Katika study hiyo, Ujerumani iliongoza kwa watu wanaojua mambo ya kimataifa huku Ufaransa ikiwa na hali ya wastani. Iwapo Tanzania tukihusishwa sidhani kama hatutoshika mkia.

OK, nisikuchoshe ipo hivii!
Ili kujua mambo ya kimataifa inahitaji mambo matatu yafuatayo :
1.Kusoma(vitabu, majarida na machapisho mengine kuhusu mambo ya kimataifa)
2.Kusikiliza(redio za kimataifa k.v DW, BBC n.k)
3.Kutazama (documentary, Tv shows na audiovisual nyinine).

Kwakukusadia anza na hii package kam utaweza:

1.Converse, Philip E. 1975. “Public Opinion and Electoral Behavior.” In Handbook of Political Science, ed. Nelson W. Polsby and Fred I. Greenstein . Vol. 4.
Reading, MA:
Addison-Wesley.
Google Scholar |

2.Converse, Philip E. 1990. “Popular Representation and the Distribution of Political Information.” In Information and Democratic Processes, ed. John A. Ferejohn and James H. Kuklinski . Urbana:
University of Illinois Press.
Google Scholar |

3.Converse, Philip E. , with Richard E. Niemi . 1971. “Non-voting among Young Adults in the United States.” In Political Parties and Political Behavior, ed. William J. Crotty , Donald M. Freeman , and Douglas G. Gatlin . Boston:
Allyn and Bacon.
Google Scholar |

4.Curtice, John , Anthony Heath , and Roger Jowell . 1994. “The Cross-National Election Project. First Results: Media Influence in Britain.” Presented at the annual meeting of the American Political Science Association, New York, September 1-4.
Google Scholar |

5.Dalton, Russell J. 1993. Politics in Germany. Second Edition. New York:
Harper Collins.
Google Scholar |

6.Fletcher, Frederick J. , and Daphne Gottlieb Taras . 1988. “The Mass Media and Politics: An Overview.” In Canadian Politics in the 1980s, ed. Michael S. Whittington and Glen Williams .
Second Edition.
Toronto: Methuen.
Google Scholar |

7.Graber, Doris A. 1993. Mass Media and American Politics. Fourth Edition.
Washington, DC:
C.Q. Press.
Google Scholar |

8.Graber, Doris A.
1994. “Why Voters Fail Information Tests: Can the Hurdles Be Overcome?” Political Communication 11(2):331-346.
Google Scholar |
Graham, Thomas W. 1994. “Public Opinion and U.S. Foreign Policy Decision Making.” In The New Politics of American Foreign Policy, ed. David Deese . New York: St. Martin's.
Google Scholar |

9.Heinderyckx, François . 1993.
“Television News Programmes in Western Europe: A Comparative Study.” European Journal of Communication 8🙁2)425-450.
Google Scholar |

10 Holsti, Ole . 1992.
“Public Opinion and Foreign Policy: Challenges to the Almond-Lippmann Consensus.” International Studies Quarterly 11(3):412-423.
Google Scholar |

11.Hyman, Herbert H. , and Paul B. Sheatsley . 1947.
“Some Reasons Why Information Campaigns Fail.” Public Opinion Quarterly 11(3):412-423.
Google Scholar |

12.Inglehart, Ronald . 1990. Culture Shift in Advanced Industrial Society.
Princeton, NJ:
Princeton University Press.
Google Scholar |

13.Iyengar, Shanto . 1991. Is Anyone Responsible? How Television Frames Political Issues.
Chicago: University of Chicago Press.
Google Scholar |

14.Jennings, M. Kent .
1983. “Gender Roles and Inequalities in Political Participation.” Western Political Quarterly 36(3):364-385.
Google Scholar |

15.Johnston, Richard , André Blais , Henry E. Brady , and Jean Crête . 1992. Letting the People Decide: Dynamics of a Canadian Election. Stanford, CA: Stanford University Press.
Google Scholar |

16.Kleinsteuber, Hans J. , and Peter Wilke . 1992. “Germany.” In The Mass Media in Western Europe: The Euromedia Handbook, ed. Bernt Stubbe Østergaard .
London: Sage.
Google Scholar |

17.Kornberg, Allan , and Harold D. Clarke . 1992. Citizens and Community: Political Support in a Representative Democracy.
Cambridge:
Cambridge University Press.
Google Scholar |

18.Kriesberg, Martin . 1949. “Dark Areas of Ignorance.” In Public Opinion and Foreign Policy, ed. Lester Markel .
New York: Harper.
Google Scholar |

19.Lambert, Ronald D. , James E. Curtis , Barry J. Kay , and Steven D. Brown .
1988. “The Social Sources of Political Knowledge.” Canadian Journal of Political Science 21(2):359-374.
Google Scholar |

20.Larson, James F. 1984. Television's Window on the World: International Affairs Coverage on the U.S. Networks.
Norwood, NJ:
Ablex.
Google Scholar |
Lippmann, Walter . 1955. Essays in the Public Philosophy.
Boston: Little, Brown.
Google Scholar |

21.Luskin, Robert C.
1990. “Explaining Political Sophistication.” Political Behavior 12(4):331-361.
Google Scholar |

22.Martinelli, Kathleen A. , and Steven H. Chaffee . 1995.
“Measuring New-Voter Learning via Three Channels of Political Information.” Journalism and Mass Communication Quarterly 1(1):18-32.
Google Scholar |

23.Mondak, Jeffery J.
1995. “Newspapers and Political Awareness.” American Journal of Political Science 39(2):513-527.
Google Scholar |

24.Morgan, David .
1991. “Media-Government Relations: The Right to Manage Information versus the Right to Know.” Parliamentary Affairs 44(4):531-540.
Google Scholar |

25.Murray, Douglas J. 1994. “Canada.” In The Defense Policies of Nations, ed. Douglas J. Murray and Paul R. Viotti . Third Edition. Baltimore:
Johns Hopkins University Press.
Google Scholar |

26.Nadeau, Richard , Richard G. Niemi , and Timothy Amato . 1995. “Emotions, Issue Importance, and Political Learning.” American Journal of Political Science 39(1):558-574.
Google Scholar |

27.Neuman, W. Russell . 1986. The Paradox of Mass Politics.
Cambridge, MA:
Harvard University Press.
Google Scholar |

28.Neuman, W. Russell . 1991. The Future of the Mass Audience.
Cambridge:
Cambridge University Press.
Google Scholar |

29.Neuman, W. Russell , Marion R. Just , and Ann N. Crigler . 1992. Common Knowledge: News and the Construction of Political Meaning.
Chicago: University of Chicago Press.
Google Scholar |

30.Palmer, Michael and Claude Sorbets . 1992. “France.” In The Media in Western Europe: The Euromedia Handbook, ed. Bernt Stubbe Østergaard .
London: Sage.
Google Scholar |

Ahsante, wengine wataongezea.
 
kama ufaransa haina uhuru wa kujieleza ni nchi zipi zenye uhuru huo hebun zitaje basi hata tano ili tujifunze
Nimeizungumzia Ufaransa kwakuwa imejipiga kifua kujivuna kuwa ipo mstari wa mbele kwenye uhuru wa kujieleza na habari na nimetoa ushahidi wangu kwa case chache tu zinazothibitisha kuminywa huo unaoitwa uhuru wa kujieleza hivyo Sipo kwenye kufanya comparison study. Ikiwa unaona sijaitendea haki ufaransa na nimekuwa biased kwenye maelezo yangu, you're welcome here on Jamii Forums where we dare to talk openly.
 
hata marekan na mataifa mengine ya magharibi yanaposhutumu china au iran kuminya uhuru wa kujieleza huwa wanakuwa wamecompare na kwao ndio wakaona kuwa hao jamaa hawana uhuru wa kujieleza, tunaposema yemen hakuna amani ni kwasababu tumecompare na nchi zingine ambazo zina amani direct au indirect ndio tukaona kuwa yemen hakuna amani, huwezi kusema nchi fulani haina uhuru wa kujieleza halafu eti we mwenyew hauna mifano ya nchi ambazo zina uhuru wa kujieleza mkuu, au unaogopa ukitoa mifano ya nchi zenye uhuru mkubwa wa kujieleza zaidi ya france utakua umefungua milango ya maswali yanayoweza tatiza mada yako? huu ujumbe uliotuandikia utaeleweka zaidi kama utajibu maswali yetu
 
Back
Top Bottom