GE2025 Je, uchawa au kujipendekeza kwa wagombea ndicho chanzo pekee kinachovuruga demokrasia na haki za wapiga kura?

GE2025 Je, uchawa au kujipendekeza kwa wagombea ndicho chanzo pekee kinachovuruga demokrasia na haki za wapiga kura?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Wakuu!

Tuko kwenye joto la uchaguzi, lakini kuna wimbi la baadhi ya watu mashuhuri kujipendekeza — au kwa lugha nyepesi, uchawa. Tabia hii binafsi siipendi, kwa sababu ina madhara makubwa kwenye mfumo wa uongozi na mustakabali wa taifa letu.

Kilicho hatari zaidi ni kwamba hawa “machawa” wanaonekana kuwa na nguvu ya ushawishi na uwezo wa kuwaathiri wale walio nyuma yao, hasa kwenye maamuzi ya kwenye sanduku la kura.

Umaarufu wao, majina yao au nafasi walizonazo zinatumika kama chombo cha kusukuma ajenda fulani, hali inayowafanya wapiga kura wapoteze uhuru wa kuchagua kwa misingi ya sera na uwezo, na badala yake naona kama wanaingizwa kwenye mkumbo wa ushawishi wa kiitikadi au kihisia.
 
Tunapoelekea chawa wenyewe wataanza kufanyiana fitina
 
Ndugu hapo ulipopagusa ndio penyewe, siasa za Tanzania zimekuwa ni unafki mtupu, siasa ya ya Tanzania saivi napenda kuiita ASS KISSING POLITICS yaani watu nikuyaangalia matumbo yao tu, watu wamekuwa wanafki, watu niwaongo ilimradi tu washibishe matumbo yao. Mbaya zaidi ni hizi tabia kweli zinapotosha wananchi, na hao hao wananchi wanaishia kutumia huko.mbeleni. SIASA ZAKUBISU MATAKO NA WABUSU MATAKO


ASS KISSING POLITICIANS WITH THEIR ASS KISSING POLITICS

#Siasambovuzabongo
#upuuziunaendelea
#tanzaniaAmka
#backbenchers
 
Back
Top Bottom