Je, Tutafika????

Trust None

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2018
Posts
1,260
Reaction score
4,421
Kama JF mods watakuwa wanafuta NYUNDO zinazoponda na kusawazisha JIWE; Je, tutafika? Nyumba itajengwaje bila nyundo kuponda jiwe?Au tuponde dogo?


Kama viongozi wetu hawasikilizi maoni ya raia, malalamiko ya watumishi, wafanyabiashara, wanasiasa, wakulima na wananchi kwa ujumla; Je, tutafika? Tembea kifua mbere!.


Kama hatufuati katiba, kanuni na sheria; Je, tutafika? We a on ze rait tirak!


Kama hatuwapi nafasi wateule wetu kutumia taaluma yao, elimu, busara na uzoefu; Je, tutafika? Uongozi wangu!, tutakuwa dona kantri.


Kama tutaendelea kubana kitaifa na kimataifa; Je, tutafika? Tuitakie mema nchi yetu.


Kama tunafanya kazi ili tupate sifa badala ya maslahi ya taifa; Je, tutafika? Mimi sipangiwi, wataishi kama mashetani.


Kama tutafanya kazi siku zote bila kupumzika; Je, tutafika? Hapa Kazi Tu. Tupumue kidogo.
 
Unahatari wewe, nimefurahi sana. Ingawa uhakika wa kula sina, bora nina bandu maana ingekuwa tabu sana.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…