Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Kwenye kipindi mashuhuri cha Je, Tutafika? kinachorushwa na Chanel 10 , jana usiku kiliutanabahisha umma kuwa tatizo la Zanzibar hasa ni la kibaguzi linatokana na muundo wa chama cha ASP unaoashiria ubaguzi ambao mpaka leo unauendelezwa.
Wanajapo hao waliotambulishwa kuwa wasomi wa hitoria kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam, walidadisi sababu zilizopelekea kuwa chama cha ASP kilianzishwa kama cha kibaguzi kilichounganisha makabila mawili (Shirazi na wahamiaji kutoka bara) na si chama cha kitaifa. Wakati ZNP ( Zanzibar Nationalist Party) na ZPPP (Zanzibar&Pemba Peoples Party) ambavyo vina sura na mtizamo wa kizalendo na kujuumuisha watu wote na wenye asili tofautiwaliopo Zanzibar
Vyama hivi viwili ZNP na ZPPP hatimae viliunda UKAWA na kuibwaga ASP kwenye uchaguzi na kuweza kuunda Serikali ya pamoja 1963 Mohd Shamte kutoka ZPPP akiwa Waziri Mkuu. Serikali hiyo baadae ilipunduliwa na watu(wengi wao) kutoka bara wakiongozwa na John Okello kutoka Uganda!Mauaji makubwa yalitokea na wahanga waliolengwa kuwa wafuasi wa kawaida wa vyama vya ZNP na ZPPP.
Mauaji yaliendelea baada ya Mapinduzi chini ya utawala wa Karume na watu wasiokuwa na hatia kuendelea kupotea na hali ilibadilika hadi kufikia kuwageukia viongozi wenzake ( mawaziri) na kuwaua kama vile Abdalla Kassim Hanga, Twala, Othman Sherif, orodha ni refu.
Walisema hatua ya kubeba mabango ya uchochezi na kibaguzi kwenye sherehe za Mapinduzi ni kuonesha sura zao kamili za ubaguzi.
Hata hivyo kipindi kilimalizika bila ya kupendekeza nini kifanyike ili hali hii imalizike