Ufundishaji katika shule nyingi za sekondari za kata hauendani na haufuati mpango wa Maandalio ya Somo. Nadhani, sasa ni wakati mwafaka wa kuachana nazo. Kuna sababu hizi za kusema hayo.
Mosi, aina ya wanafunzi wanaojiunga na shule hizi wanahitaji nguvu na mbinu za ziada ili kuwawezesha kuelewa masomo ya sekondari.
Pili, walimu wengi wamekataa tamaa ama kutokana na maslahi duni ama kutokana na aina ya wanafunzi wanaowapokea toka shule za msingi ama kutokana na maneno ya viongozi kila uchao kuwashambulia na kuwadhalilisha walimu.
Tatu, walimu wengi kutozingatia kabisa uandaaji na utumiaji wa maandalio ya somo.
Mwisho, wakaguzi wa elimu kuwa na maelekezo ya kujikanganya kuhusu namna ya kujaza maandalio ya somo.