Je, tewuta wanatumiwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, tewuta wanatumiwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mpingo1, Jun 7, 2009.

 1. M

  Mpingo1 Member

  #1
  Jun 7, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 91
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wafanyakazi TTCL waisusia management.
  Imeandikwa na Veronica Mheta; Tarehe: 7th June 2009 @ 08:16 Imesomwa na watu: 114; Jumla ya maoni: 0
  Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Mtandao wa Simu (Tewuta), wamekataa mapendekezo ya uongozi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), yaliyowasilishwa juzi jijini Dar es Salaam katika kikao cha kunusuru mgogoro unaotaka kuibuka katika kampuni hiyo.

  Aidha wafanyakazi hao wametaka mapendekezo waliyokubaliana na uongozi huo Novemba, 2008, yatumike ili wafanyakazi wapewe nafasi kubwa ya uongozi katika Baraza la Wafanyakazi hao.

  Wakizungumza na 'HabariLeo Jumapili' baada ya majadiliano kati ya uongozi wa TTCL na viongozi wa chama hicho kutoka mikoa mbalimbali, Katibu Mkuu wa Tewuta, Junus Ndaro, alisema Menejimenti ya TTCL haikuwasilisha ajenda za nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi zaidi ya 1,424.

  Alisema badala yake viongozi wa TTCL waliwasilisha ajenda ya wafanyakazi ambao hawafiki 40 kati ya 1,424 kupandishwa vyeo. Alisema baada ya uongozi kuwasilisha ajenda hizo viongozi wa Tewuta kutoka mikoa mbalimbali walizijadili na kugundua kuwa bado zina makosa kwani hazikuhusisha ajenda ya wafanyakazi kulipwa mishahara yao inayofikia zaidi ya Sh bilioni 10.

  Pia alisema mapendekezo ya menejimenti ya TTCDL hayaonyeshi njia nzuri ya kutatua migogoro. Naye Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa TTCL, Amin Mbaga, alisema kutokana na kasoro zilizojitokeza katika mkutano huo uongozi wa kampuni hiyo unayafanyia kazi marekebisho hayo ili Juni 9 watakapokutana wayajadili. “Hata wabunge wanajadiliana kwa hoja na kufikia uamuzi na sisi pia tumejadiliana kwa hoja hivyo tutatoa mapendekezo yetu siku hiyo kisha yatajadiliwa na kufikia mwafaka ili wafanyakazi wafanye kazi bila migogoro,” alisema Mbaga
   
Loading...