Je Tanzania yetu ina wepesi gani kwenye kukabiliana na magonjwa ya milipuko?

Naren

JF-Expert Member
Apr 22, 2016
692
425
_Jioni hii nimekuwa nikitafakari juu ya mambo ambayo yahitaji wepesi wa wananchi kuyakabili na kuyaondosha, swala moja linaloniacha na alama ya kuuliza ni wepesi wa nchi yetu kwenye kuyakabili magonjwa hasa yale ya milipuko maana hakuna mwenye kuijua kesho!
Hivi ni kweli tuna wepesi katika kuyakabili haya na si tu wepesi bala hata dhana zakutumia ili kukabiliana na dharura za namna hii?
 
Sidhani hata tuna utaalamu na vifaa vya kukabiliana na hayo magonjwa. Ukweli kwamba hata tahadhari ya kunawa mikono, kuvaa gloves ni wa mbinde, sembuse vifaa vya kuwatenga (quarantine) walioathirika ili wasisambaze madhara kwa wengine. Kuna madawa, na vifaa vinavyohitajika kila siku katika mahospitali na zahanati au maduka ya dawa, na yanakosekana, fikiria sasa vitu au madawa yanayohitajika wakati wa mlipuko, ambao kwa mawazo yetu hata hatufikirii uwezekano wa kutokea, je yatakuwepo?
 
Back
Top Bottom