bila shaka hujui unachokiongea,mi naliongelea kama taifa na nalinganisha na mataifa mengine kama afrika kusini ufaransa, libya,misrina nchi nyingine nyingi,angalia watawala wetu hata bungeni tu wanaingiza kiingereza,mikutano mingi ya hapa kama kuna kiongozi wa nje utaona wanatumia kiingereza.nakumbuka jack shirak wa ufaransa aliwahi kutoka nje ya mkutano wa umoja wa ulaya kisa waziri wake kaongea kiingereza na huu ndio mfano ninaotaka uigwe na watawala wetu,kama kweli tunaulinda utamaduni wetu kwanini lugha ya kufundishia tunapotaka iwe kiswahili liwe lina mjadara tena mrefu namna hii?Tanzania ina utamaduni wake na inaulinda kwa dhati nao ni Kiswahili. Mfano wa mahakama ni mfu kwa sababu lugha ni optional nako ni Mahaka za juu tu. Mahakama za Mwanzo na Wilaya ni Kiswahili pia kwa Hakimu mkazi mkoa ni kiswahili. Mteja ana uhuru wa kuchagua lugha. Asilimia mia moja ya Wabongo wanaongea Kiswahili. Unataka ID gani? Chuo kikuu tunafundishwa kwa Kiingereza nk lakini tunafanya discussion kwa Kiswahili na kujibu kwa Kiingereza nk, hivyo lugha inatumika ngazi zote za Elimu, UPO! Je ni watu wangapi umewaona wanasoma magazeti ya Kiingereza kama si kiswahili hadi kwa graduates!
Kitambulisho cha Mtanzania ambacho ni Peculiar ni Kiswahili.
Tanzania ina utamaduni wake na inaulinda kwa dhati nao ni Kiswahili. Mfano wa mahakama ni mfu kwa sababu lugha ni optional nako ni Mahaka za juu tu. Mahakama za Mwanzo na Wilaya ni Kiswahili pia kwa Hakimu mkazi mkoa ni kiswahili. Mteja ana uhuru wa kuchagua lugha. Asilimia mia moja ya Wabongo wanaongea Kiswahili. Unataka ID gani? Chuo kikuu tunafundishwa kwa Kiingereza nk lakini tunafanya discussion kwa Kiswahili na kujibu kwa Kiingereza nk, hivyo lugha inatumika ngazi zote za Elimu, UPO! Je ni watu wangapi umewaona wanasoma magazeti ya Kiingereza kama si kiswahili hadi kwa graduates!
Kitambulisho cha Mtanzania ambacho ni Peculiar ni Kiswahili.
nilihisi kuwa wanoosoma tovuti hii ni waelewa kumbe sivyo wengine wanabisha tu ili waonekane wanabisha haya mkubwa'bila shaka hujui unachokiongea,mi naliongelea kama taifa' Tafakali maelezo yangu ni Scientific to ur views. Sijarejea maamuzi ya kijiji ni ya kitaifa. "Mfano wa mahakama ni mfu kwa sababu lugha ni optional nako ni Mahaka za juu tu. Mahakama za Mwanzo na Wilaya ni Kiswahili pia kwa Hakimu mkazi mkoa ni kiswahili. Mteja ana uhuru wa kuchagua lugha" Tazama ulichoongea-"utaona ni kichekesho mtu kutoka kijijini anapohukumiwa kwa kiingereza, yaani tumeshidwa kabisa kulinda utamaduni wetu!" Au wewe ndo hujui ulichopresent kama mada??!! Umefanya research ngapi zinazoonyesha kuwa anayefikishwa/fika mahakamani akitokea kijijini hajui kiingereza? Au umekuwa myopic circumveted na kijiji cha kwenu utokako, ukazani Tanzania yote haina wanaojua kiingereza vijijini? Tanzania tunalinga na utamaduni wa lugha ya Kiswahili na Kimombo chamwagwa hadi VIJIJINI ambako kuna maafisa Ugani, walimu, waganga na wauguzi,maafisa wastaafu nk. Kuwa INTEGRATIVE ndugu!
Mkuu naona sasa wewe umekwenda mbali sana... hivi Marekani wanapozungumza kiingereza ina maana wao ni waingereza na hawana haki ya kudai kuwa lugha hiyo ni ID yao..Hivi nani kasema na imepitishwa wapi na lini?..Nani aliyepitisha hata kiingereza kuwa lugha ya mawasiliano duniani! wapi na lini maanake hata sikuelewi kwa sababu lugha hiyo inazungumzwa na watu kibao wa mataiufa kibao kama kiswahili unachokihoji hapa..Hapa USA nimekutana na Wacongo toka Goma wanapiga kiswahili saafi nao ni Watanzania?
Kuna Waganda toka North Uganda wanaongea kiswahili kama wameishi Tanzania vile lakini bado si watanzania.
Wako Wanyarwanda wanaongea kiswahili kizuri sana kwa kukipenda kama lugha nao ni Watanzania?
Wakenya wa Mombasa na Lamu wanakirudi kiswahili kama kuria kata ya mbege.
Wasomali toka visiwa vya kismayu wanaongea kiswahili safi kama wapemba, hata sura na tabia zao wanafanana na wapemba lakini bado si Watanzania.
Kiswahili siyo Kitamburisho cha Mtanzania yeyote labda kwa kujidanganya tukiwa ndani ya mipaka ya Tanzania.
Tukubali ukweli kwamba hicho kitamburisho hakikuwepo tangu zamani. Uongo namba moja, tulijidanganya kwamba tunacho kitambulicho cha kitaifa na sasa tunasema uongo namba
mbili kwamba sijui utanda wazi au sijui tumeshindwa kukilinda!!!
Ni lini tulitamka wazi kwamba Kiswahili ni Kitambulisho cha MTanzania?
Tamko hilo lilitolewa au kupitishwa na nani na pia wapi huko lilipitishwa?
Unaweza kulinda kitu kisichokuwepo???
lakini taifa haliwezi kuwa taifa bila utambulisho ambao ni utamaduniMuanzisha maada, maada yako ni nzuri na very critical, ambayo, matatizo mengi sana yanayotokea hivi sasa ni kuwa hatuna utamaduni, hatuna maandiko, miiko, hatuna kitu.
Je viongozi wetu wakila rushwa na kutuhumiwa wanaachia madaraka?
nini adhabu ya wala rushwa?
....
.....
je tunalinda mali zetu?
kwa kiasi gani mali zetu zinakuwa na wananchi na si za watu wachache?
je elimu yetu inaendana na hali halisi ya taifa letu na mahitaji yetu..
Swali lako ni basic, na msingi wa haya yoooote tunayoyapigia kelele hapa, to be honest, inahitaji greath thinkers to go to thoe basics, ama sivyo tutajaza post humu, kila mtu atatushangaa
Je utamaduni wetu unasemaje kuhusu waliotuhumiwa na rushwa, tuwapokee kwa mazuri mekundu, ukieeenda mbali ungundua tatizo si viongozi tu bali hata wale wanaowaongoza,
Ila title kidogo kali?
Ni taifa hai lisilo na utamaduni , utamaduni unakuwa hai kwenye taifa linalopractise huo utamaduni.