Je! Tanzania kuna utawala bora ?

Je! Tanzania kuna utawala bora ?

MZEE WA USSOKE

Senior Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
120
Reaction score
42
Amani kwenu wana JAMII FORUM

Baada ya kutafakari mambo mbalimbali yanaendelea katika nchi yetu nimeona nitumie nafasi hii tujadili kuhusu nchi yetu inazingatia utawala bora?

Kabla ya kuuacha mjadala huu kwa wana JF kuuchangia,naomba nieleze mambo machache kuhusu utawala bora.

Utawala bora ni uongozi wenye mwelekeo wa maendeleo yanayoongozwa na wananchi wenyewe kwa uwezeshwaji wa serikali.

a]Utawala bora unataka kuwepo na serikali SIKIVU ambayo inasikiliza mahitaji na malalamiko ya
watu.Watawala ambao wamepewa dhamana na wanachi,wanapaswa kuwasikiliza hao waliowa
pa dhamana.

b]Utawala bora unahitaji kuwepo na UWAZI ambapo mambo yanafanywa bila kificho

c]Utawala bora unahitaji kuwepo kwa serikali inayofuata matakwa ya watawaliwa kwa maana ya
kuwajibika kwa wananchi

d]Ili nchi iweze kuwa na utawala bora ,inatakiwa iwe na serikali ambayo imepatikana kwa ridhaa
ya wananchi .Viongozi wanatakiwa wapatikane kwa uchaguzi ulio huru na wa haki.

e]Utawala bora unahitaji kuwepo kwa vyombo mbalimbali vya habari visivyomilikiwa KIUKIRITI
MBA na serikali au kikundi kingine chochote.vyombo vya habari vinapaswa kutoa habari kwa wa
nanchi na wale walioko madarakani.Vyombo hivi vinatakiwa vifanye kazi kwa uhuru lakini kwa
kufuata misingi ya sheria na maadili ya kazi/taaluma zao.

Nimejaribu kwa ufupi kutoa mwanga ambao najua wana JF,walio wengi mnao,

Tujadili suala hili la utawala bora kwa ueledi.JE!TANZANIA KUNA UTAWALA BORA

Naomba kuwasilisha.
 
Utawala bora CCM wa*nye wapi? Hizi thread zinatuongezea hasira tu, ebu muwe mnapitisha siku japo moja bila kutujaza mihasira!
 
Utawala bora haupo kabisa hapa tz. Kuna utawala wa bora liende aka utwana.
 
Mkuu jibu ni hapana.Huhitaji hata kufikiri wa kutafakari kupata jibu.
 
Utawala bora upo ila hakuna Uongozi Bora.Waasisi walimaanisha Uongozi Bora na wala si utawala bora.
Rejea.......'Siasa Safi na Uongozi Bora'.
 
UONGOZI NA UTAWARA BORA VYOTE VIPO ndo maana wale wa EPA walirudisha mijihela walioiba!
 
Utawala Bora ulikuwepo Tanganyika kwani tulikuwa kila kitu tunakuwa tunatimiziwa, tofauti na Tanzania ya leo ambayo haki zetu za msingi tumeshanyan'ganywa wamechukua watu wachache na wakati walipa kodi tumeachwa bila maji, Elimu na miundombinu ikiwa hoi rushwa ndo hiyo ni nambari wani
 
Back
Top Bottom