Ad majorem
JF-Expert Member
- Aug 11, 2018
- 1,101
- 1,650
Kwa Wananzengo wenzangu.
Kama mnavyofahamu kipenga cha kufungua Michuano ya Fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani maarufu kama CHAN kwa mwaka 2025, kinapulizwa leo kwenye ardhi ya Kambarage wa Butiama. Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa fainali hizi.
Lakini katika hali ya kushangaza, hakuna shamrashamra zozote kuelekea michuano hiyo. Ukiachana na Tamasha la Singeli, hakuna amsha amsha zile za kuhamasisha watu kuelekea fainali hizo. Hamasa ya National timu, inazidiwa na hamasa ya Ndondo Cup. Juzi nimesafiri kutoka Posta mpaka Mbezi, sikuona Billboard hata moja inayoonyesha Tangazo la fainali hizo. Ni kweli wizara imeshindwa kufanya organisation ya hamasa?
Simba na Yanga huwa wanafanikiwaje kuhamasisha mechi zao?
Au kila mmoja yuko busy na Maandalizi ya Uchaguzi?
Ukipita kwenye vijiwe vya kahawa mjini, hakuna anayezungumzia fainali hizo. Vyombo vya habari na influencers nao hawajafanya vizuri. Je, wamekosa mtu wa kuwaorganise au wamesusa? Je, watu wamekosa uzalendo kwa nchi kiasi hiki? Au ni hujuma kwa serikali ionekane haifanyi kazi yake vizuri?
Mbona watu wa Chama wameweza kuweka Mabango njia zote na mengi kweli. Tunashindwaje kwa jambo la nchi?
TUJISAHIHISHE.